Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huku usiende sasa ndugu maana sasa hata nikikuuliza ofisi za hao illuminati zipo wapi hautanionesha.Inasemekana pia alitaka kujitoa illuminati, hata nyimbo zake nyingi zilikuwa na message, za kuwaponda ma illuminati, mfano kiliminat, me against the world, nk wakatumia bifu lao na Big wakammaliza.
Suge knight ndie muuaji
Kuna madawa. Hawa wasanii wa miaka hii wapo tayari hata kufanya deal chafu tu ili kutengeneza mamilioni.Ha ha ni sawa na kusubiri meli airport.. ila aongeze jitihada.
Poetic justice.Hivi ile muvi alicheza na Janet Jackson inaitwaje?
Mahakama gani sasa, kisutu au? Khaaaaaah jamani.Shahidi namba 1 ni wewe. Fika mahakamani bila kukosa
Sawa sawa kuna ingine inaitwa Boys in da hood unaipata?Poetic justice.
Haka katakuwa kalisoma gazeti la uwazi. Wakati mtandaoni kuna hadi picha za crime scene kabisa ambapo mauwaji yametokea kenyewe kanasema mtu ameshambuliwa ukumbini, ukumbi gani sasa huo, Diamond Jubilee au?!Hivi ulishawahi kuiona ile movie inayohusu maisha ya Big?
Pia historia ya waliokwepo wenyewe ambayo inasema alipigwa risasi kwenye traffic right.
Sasa hilo la kupigwa risasi kwenye ukumbe wa award umelitoa wapi?
Hivi unajua ulinzi unaowekwaga katika kumbi au maeneo ya umma?
Unafikiri ni kwanini hata 2pac haikuwa rahisi kumuuwa ukumbini mpaka wakasubiri afike barabarani tena usiku.
Hebu fikiria kwanz kabla ya kuandika mkuu.
2pac alikuwa mgovi sana.*uck Mobb Deep, *uck Biggie
uck Bad Boy as a staff, record label and as a mother*ucking crew
And if you want to be down with Bad Boy, then *uck you too
Chino XL, *uck you too
All you mother*uckers, *uck you too..Hapo imetukanwa label ya bad boys na wafanyakazi wake wote hadi wafagiaji,Mobb Deep nao wakaingizwa humohumo na yeyote anayejihusisha au kuihusudu Bad Boy nae kaingizwa ilikuwa hatar sana hii[emoji3]
Nimekwenda kutazama nimegundua sipo sahihi ila siwezi kukubali kushindwa kinyonge ngoja nilete ligi tu na kubadilisha mada.50Cent ndo alipigwa tisa. Pac alichezea tano.
Yeah ile ya akina Ice cube.Sawa sawa kuna ingine inaitwa Boys in da hood unaipata?
Ishu ya vifo vya hawa mastaa vinautata sana na kamwe hatutapata uhalisia,tunafanya kuhisi tu..Msikilize bodyguard wa Big katika mahojiano yake na Vlad Tv anachosema kuhusu Puffy na kuhusu bloods waliohusika kumuua Big,na tuhuma zake direct kwa Puffy siku ile sababu alimwambia kuna bloods wana mpango wa kumuua Big na alichomjibu siku ile ya asubuhi
Hatari sana "then if you're down with bad boy then fu ... you too ..Chino excel... Mle mwamba katukana sana.[emoji23][emoji23][emoji23] yani mle alimtukana Big mpaka mtu aliekuwa anasikiliza nyimbo za Big nae alihusishwa kwenye matusi.
Sawa Mmarekani mmatumbi mimi sikupingi [emoji23]Ugomvi wa 2pac na Big haukuanza kwenye wimbo.
Ni hivi.. 2pac na Big walikuwa marafiki wakubwa sana maana wote ni wazaliwa wa New York, japo mazingira ya kimaisha yalisababisha waishi miji na maeneo tofauti yani 2pac akiishi LA California na Big akiendelea kuishi alipozaliwa New York.
2pac alimchukulia Big kama mdogo wake, hivyo mara nyingi alipokuwa anaenda kupiga show kadhaa maeneo mbali mbali ya nchi alimpa Big shavu na yeye aimbe ili kumtengenezea jina.
Mwaka 1994 2pac akiwa New York alipanga kwenda kumtembelea rafiki yake Big katika studuo yao ya Bad Boyz. Kama ilivyo ada ya marafiki, kabla 2pac hajaenda alimpigia sim Big na kumtaarifu kuhusu ugeni wake huo ambapo Big alikubali aende atampokea. 2pac alipofika katika jengo la studio wakati akapewa address na Big kwamba apande ghorofa ya ngapi kwa kutumia lift ya mjengo huo. Wakati 2pac akiingia ndan ya lift ghafla wakaingia vijana wengine watatu ambapo wakati lift ikiwa katika michakato ya kupanda wakatoa bastola na kumtaka 2pac achojoe kila alichonacho. 2pac japo aliona jamaa wana bastola na wako serious kwa kile wanachoongea, lakini alikataa unyonge na kuamua kutoa bastola yake aliyokuwa ameificha kiunoni nyuma ya mgongo (kumbuka 2pac ameanza kutembea na bastola akiwa na umri wa miaka 12 kutokana na maisha ya kitaa na mshike mshike aliyokulia) wale jamaa walipoona 2pac anatoa bomba ndo wakaaona wamuwahi kwani wangefanya mzaha kidogo wangeangushwa wao.
Jamaa wakampiga risasi tano akapoteza fahamu (wao wakajua amekufa) na kuchukua kila alichokuwa nacho zikiwepo mkufu wa dhahabu na pete yake pamoja na hela wakakimbia.
2pac alipozinduka akajikuta yupo hospital afu si Big wala Bod Boyz yoyote aliefika kumuona, kitendo kilichomfanya 2pac ahisi kwamba lile tukio lilipangwa na Big kwani haiwezekani best friend wako apigwe risasi wakati akija kukuona afu wewe ushindwe kufika hospital na usimpigie hata simu. Kibaya zaidi wakati Big anatoa nyimbo yake fulan alivaa pete inayofanana na ile aliyoibiwa 2pac.
Hilo likamfanya 2pac aamini kuwa rafiki yake huyo alim set up hivyo na yeye hakupenda unafiki akaamuwa kuweka wazi kuwa kuanzia siku hiyo yeye na Big urafiki basi na kwamba sasa ni maadui rasmi. Kama hiyo haitoshi 2pac alipotoka jela tu akam seti mke wa Big watoe nae nyimbo inayoitwa You wonder why i call ya bi...t ch.
Mke wa Big (Faith Evans) pamoja na kwamb alifahamu ugomvi wa mumewe na 2pac lakini alikubali kwenda kuingiza kurecord nyimbo hiyo, na 2pac akatumia mwanya huo kufanya yake. Inasemekana 2pac alikuwa na ulimi fulan ambao akiongea dem yoyote hachomoi. we fikiria mtu kagombana na mumewe lakini katengenezwa hadi katengenezeka kwenda ku record [emoji23][emoji23][emoji23].
Baada ya ku record na kutafuna 2pac ndo akaweka bayana kila kitu hivyo uadui ukazidi na wale waliokuwa na malengo yao wakatumia chance hiyo kufanya yao. 2pac kabla ya ugomvi wake na Big alikuwa na ugomvi na serikali kwa kuwatukana wazi wazi viongozi wa nchi kutokana na ubaguzi wao wa rangi, alikuwa na ugomvi na polisi, FBI nk kwa sababu mama yake alikuwa katika list ya watu waliounda kundi la Black Panther lililokuwa vuguvugu la kudai haki za watu weusi.
Kwahiyo huenda serikali (FBI) walitumia mwanya huo kufanya yao, maana nyimbo zake ni kama vile zilikuwa zinawashtua na kuwafungua macho watu weusi wadai na kujua haki zao kitu ambacho serikali iliyokuwa inaongozwa na wazungu hawakukipenda.
Tayari walishakua na bifu ,ukumbuke 2pac alishawahi shambuliwa kabla ya tukio lapili lililomuondoa na mhusika ilikua bigYes ni visasi vyao tu ,2pac naye alivuka mipaka ,utasemaje wazi wazi kwamba umemtafuna mke wa BIG?
Mmmh aiseeNi vile tu TUPAC na BIG walikuwa watu maarufu sana lkn kimsingi Watu Weusi USA kuuana kwa kutumia Chuma ni sehemu ya Utamaduni wao!
Zipo theory zingine zinamtaja Snoopy km mtu alietia mkono wk ktk mauaji ya Pac. Binafsi nilimuona Pac akiwa kitandani Hospital, niliamini Mwamba hatoboi
2Pac alimzingua jamaa mmoja nje ya ukumbi wa lile pambano la boxing la Mike Tyson. Jamaa naye ni gang member. So , baada ya pambano jamaa akaamua amalize mchezo, ingawa kuna hisia za juhusika kwa mamlaka hasa kutokana na mashairi ya kuamsha hisia za kisiasa.Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.
BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.
Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
50cent kayafukua haya makaburi ya Diddy mana alianza kumweka wazi siri zake za ushoga ila sasa alipofikia kwenye hii kesi na kumtafuta LAPD officer aliyekuwa eyewitness wa shambulio kisha kuchukua video za Pac alizokuwa akieleza claims zake na kuwa Ana ushahidi na anajua mhusika wa shambulio tofauti tofauti ni Diddy ila iachwe na ibaki Kati Yao wawili.
Mzigo ukaja kwa Diddy kupigwa maswali kutokana na tuhuma hz..... Diddy anaonekana Ana kitu amekificha kwa muda mrefu kuhusiana na vifo viwili hivyo.
Na wanazidi kumtilia mashaka.
Shida anashikwa na kigugumizi na anaonekana kublock maswali anayoulizwa na kuact usamalia ambao anajulikana hana.Isije ikawa wazungu wanataka wammalize Diddy.