Angalau wewe umeandika vinavyoeleweka. Wengine walikuwa wanaposti longo longo tu, mara illuminati mara sijui FBI ...
KWANINI TUPAC ALIMCHUKIA SANA BIGGIE MPAKA KIFO ? (4)
_______________
Inaendelea......
Kutokana na Tupac kuhitaji bosi wa Death Row, Marion 'Suge' Knight apambane kumtoa ndani ili waweze kufanya biashara pamoja, Suge aliangaika huku na huko mpaka kufanikiwa kumchomoa Tupac jela.
Kiasi cha Dola Milioni 1.4 kilitolewa na Suge hivyo kufanikiwa kumtoa jela Tupac mwaka 1995, achilia mbali Dola 15,000 ambazo Suge alizitoa kumsaidia 'kishkaji' Tupac wakati akiwa jela.
Kimsingi Suge alikubali kujipukutisha fedha kwa sababu alijua kumwandika Tupac mkataba wa kumsimamia kupitia Death Row Records italipa. Knight alijua nini anafanya kwenye makubaliano hayo.
Makubaliano ya Tupac na Suge yakawa mazuri. Tupac akakubali kutengeneza albamu 3 chini ya Death Row Records lakini muda wote akihitaji Suge awe upande wake kwenye vita vyake dhidi ya Biggie.
Nyimbo ya kwanza ya Tupac kuitoa chini ya Death Row Records ikawa California Love. Kombinesheni ya Tupac, Dr Dre na Roger Troutman kwenye chorus ukawa unyama wa kufa mtu. Kwa hakika "The King was back from Jail''.
Ujio wa California love ulimtikisa kila mtu. Tupac alikuwa amejerea kuusimika upya ufalme wake uliotishiwa kuondoshwa kwa mtutu wa bunduki na vijana kutoka Pwani ya Mashariki (East Coast).
Marion Suge Knight na Tupac Shakur wakafanikiwa 'kuupika' mgogoro wa East Coast na West Coast ukapikika, mgogoro ambao chimbuko lake haswa ni chuki baina ya wasanii wawili, Notorious Big na Tupac Shakur.
Matatizo binafsi ya Biggie na Tupac yakajikuta yakirithiwa na hata wengine 'yasiyowahusu'. Wasanii wa East na West wakaonekana kuchukiana katika kiwango kilichotisha kabisa.
Wakati mgogoro huu ukikua na kuzidisha uhasama kwa wasanii, Serikali mwanzo ilionekana kama kupuuza, lakini kadiri hali ilivyozidi kuwa mbaya na viongozi walilazimika kusema chochote.
Lakini kabla ya kusema chochote, huko nyuma Tupac alikuwa ameshaingia kwenye mgogoro mara kadhaa na serikali kutokana na misimamo yake, harakati zake na maisha yake.
Nyimbo zake kupitia albamu yake ya 2Pacalypse ziliichefua sana serikali. Tupac alizungumzia zaidi Siasa, Ubaguzi na umasikini katika namna ambayo ilionekana kama kuchochea chuki kwa raia.
Mshtuko mkubwa ulitokea baada ya kijana mmoja mdogo kumpiga risasi polisi na kumuua kisha baada ya kukamatwa na kuhojiwa akathibitisha kufanya hivyo baada ya kusikiliza albamu ya Tupac iitwayo 2Pacalypse.
Tukio hilo lilikuwa gumzo nchini Marekani. Aliyekuwa Makamu wa Rais wakati huo, Bw Dan Quayle akatangaza kupigwa marufuku kwa nyimbo za Tupac kusikilizwa kwenye Jamii ya wamarekani.
Bw. Quayle alisema Tupac ni msanii asiyefaa kabisa kusikilizwa. Nyimbo zake zimejaa chuki na kuchochea uovu kwenye jamii. Akaanzisha kampeni za kuhakikisha jamii inamchukia na haipati nafasi ya kumsikiliza Tupac.
Masikini Quayle hakuwa amejua kuwa wakati anasema hayo, Tupac alikuwa ameshaiteka sehemu kubwa ya jamii ya wamarekani kuliko anavyodhani. Mahojiano yake na MTV ya mwaka 1993 yamlitosha kabisa kumfanya asimjibu lolote.
"Siwezi kuitawala dunia wala siwezi kuubadilisha ulimwengu, bali nichoweza kufanya ni kutema cheche zitakazofanya bongo za watu kuibadilisha dunia"..hii ndiyo kazi yetu tunayopaswa kufanya, kuamsha mtu mwingine anayetutazama".
Tupac alikiambia kituo cha televisheni cha MTV mwaka 1993 katika moja kati ya mahojiano yake yanayoendelea kukumbukwa mpaka leo. Quayle alishindwa vibaya katika kampeni ya kumaliza Tupac, lakini inaelezwa alichangia mno kupromoti mauzo ya kazi zake bila ya yeye kujua.
Watu mashuhuri mbalimbali waliyataja maneno hayo machache ya Tupac kama maneno bora zaidi kuwahi kutolewa na mtu "asiyetegemewa" na wengi kusema hivyo. Wengi waliyatumia kama rejea kwenye maeneo yao mbalimbali.
"Inawezekana baadhi yetu tusiwe watu wa kuibadilisha dunia, lakini tunapaswa kujaribu kila wakati kushawishi mtu mwingine kuchukua hatua zitakazoweza kuibadili dunia".
Maneno haya ya Tupac hata kwangu binafsi bado yanaishi sana.!
Itaendelea........[emoji3578]
#Balozi