Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Msaani maarufu wa Marekani na producer wa label ya Bad Boy record, anaejulikana kwa jina maarufu la P diddy, sasa tumbo joto baada ya mama yake na Christopher Wallace almaarufu Notorious B.I.G kumuhusisha msaani huyo na kifo cha mwanae kilichotokea mwaka 1997 huko Los Angeles, CA.

Inasemekana kwamba mama huyo amefanya uchunguzi wa kutosha na kujiridhisha kuwa huenda manager huyo wa Bad Boy record amehusika pakubwa na kifo cha mwanae, hivyo anapanga kufungua kesi ili ukweli ujulikane na kila aliehusika na kifo cha mwanae aweze kuchukiwa hatua za kisheria kutokana na mauaji hayo.

Ngoja tusubiri kitachotokea, maana kwa R Kelly ilianza hivi hivi kimzaa mzaa matokeo yake mpaka leo bado mfalme huyo wa R&B ananyea debe.
Hii si inajulikana kabisa mkuuu sio jipya hii
 
Vifo vyao vilipangwa ndomana vilifanana.
2pac gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita 2pac.. 2pac.. 2pac... basi 2pac ile kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo akaanza kushambuliwa na gari ya majamaa waliokuwa ubavuni kwao.

Big nae gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla pia wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita Big.. Big.. Big.. basi ile Big kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo na yeye akaanza kushambuliwa na gari iliyokuwa pembeni yao hadi kusababisha umauti wake.
Suge knight pia anahusika sana usimsahau jay z

Namnukuu kanye west 😳😳😳
 
Vifo vyao vilipangwa ndomana vilifanana.
2pac gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita 2pac.. 2pac.. 2pac... basi 2pac ile kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo akaanza kushambuliwa na gari ya majamaa waliokuwa ubavuni kwao.

Big nae gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla pia wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita Big.. Big.. Big.. basi ile Big kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo na yeye akaanza kushambuliwa na gari iliyokuwa pembeni yao hadi kusababisha umauti wake.
Wangeanza na hao mabinti wangeweza kupata chochote, lakini inaonekana police wanahusika au hawakutaka kufanya uchunguzi wowote wa maana, tukubali hii kesi ubaguzi umechangia sana isichunguzwe vizuri
 
Pddy hawezi kumuu BIGGIE nakataa,kwenye gari alipokuwepo BIGGIE Kulikua na ndugu yake wa damu..

Eugene deal ambae ni bondia wa pddy(Mtoto wa kaka yake)
Lil cease mjomba wa B.I.G na member wa JUNIOR M.A.F.I.A wote walifia humo..

labda bimkubwa ameona mwanae amesahaulika anataka kumrudisha kwenye trend ya vichwa vya habari...
pia inaweza kuwa ni mpango wa SUGE KNIGHT kama rivarls kwa PDDY...

Pddy ndio power control kwenye kesi ya SUGE Na anamchomekea kweli,halafu mwezi uliopita mama yake B.I.G Alikutana na SUGE mahakamani na waliondoka pamoja..

BEEF YA SUGE KNIGHT NA P.DIDDY HAIWEZI KUISHA
Ubaya suge knight ana cv chafu hela hana na influence hana


Kuna video flani niliona mtandaoni kuwa anadai sijui shs ngapi benki eti pressure na kisukari kikapanda akazimia daah 😅😅😁
 
Suge naye sasa kapigwa miaka 28 ya kutosha na sioni akitoka mapema na ana kesi na maadui mia kidogo wanamsubiri huku nje, Suge amehusishwa na mauaji mengi sana bora akae ndani tuu
Hii ni kweli na ubaya zaidi ni jamaa hana hela mkuuu kuwa apeche alolo alafu maarufu at the same time ni shida kwelikweli mkuuu 😨
 
Ugomvi wa 2pac na Big haukuanza kwenye wimbo.

Ni hivi.. 2pac na Big walikuwa marafiki wakubwa sana maana wote ni wazaliwa wa New York, japo mazingira ya kimaisha yalisababisha waishi miji na maeneo tofauti yani 2pac akiishi LA California na Big akiendelea kuishi alipozaliwa New York.

2pac alimchukulia Big kama mdogo wake, hivyo mara nyingi alipokuwa anaenda kupiga show kadhaa maeneo mbali mbali ya nchi alimpa Big shavu na yeye aimbe ili kumtengenezea jina.

Mwaka 1994 2pac akiwa New York alipanga kwenda kumtembelea rafiki yake Big katika studuo yao ya Bad Boyz. Kama ilivyo ada ya marafiki, kabla 2pac hajaenda alimpigia sim Big na kumtaarifu kuhusu ugeni wake huo ambapo Big alikubali aende atampokea. 2pac alipofika katika jengo la studio wakati akapewa address na Big kwamba apande ghorofa ya ngapi kwa kutumia lift ya mjengo huo. Wakati 2pac akiingia ndan ya lift ghafla wakaingia vijana wengine watatu ambapo wakati lift ikiwa katika michakato ya kupanda wakatoa bastola na kumtaka 2pac achojoe kila alichonacho. 2pac japo aliona jamaa wana bastola na wako serious kwa kile wanachoongea, lakini alikataa unyonge na kuamua kutoa bastola yake aliyokuwa ameificha kiunoni nyuma ya mgongo (kumbuka 2pac ameanza kutembea na bastola akiwa na umri wa miaka 12 kutokana na maisha ya kitaa na mshike mshike aliyokulia) wale jamaa walipoona 2pac anatoa bomba ndo wakaaona wamuwahi kwani wangefanya mzaha kidogo wangeangushwa wao.

Jamaa wakampiga risasi tano akapoteza fahamu (wao wakajua amekufa) na kuchukua kila alichokuwa nacho zikiwepo mkufu wa dhahabu na pete yake pamoja na hela wakakimbia.

2pac alipozinduka akajikuta yupo hospital afu si Big wala Bod Boyz yoyote aliefika kumuona, kitendo kilichomfanya 2pac ahisi kwamba lile tukio lilipangwa na Big kwani haiwezekani best friend wako apigwe risasi wakati akija kukuona afu wewe ushindwe kufika hospital na usimpigie hata simu. Kibaya zaidi wakati Big anatoa nyimbo yake fulan alivaa pete inayofanana na ile aliyoibiwa 2pac.

Hilo likamfanya 2pac aamini kuwa rafiki yake huyo alim set up hivyo na yeye hakupenda unafiki akaamuwa kuweka wazi kuwa kuanzia siku hiyo yeye na Big urafiki basi na kwamba sasa ni maadui rasmi. Kama hiyo haitoshi 2pac alipotoka jela tu akam seti mke wa Big watoe nae nyimbo inayoitwa You wonder why i call ya bi...t ch.
Mke wa Big (Faith Evans) pamoja na kwamb alifahamu ugomvi wa mumewe na 2pac lakini alikubali kwenda kuingiza kurecord nyimbo hiyo, na 2pac akatumia mwanya huo kufanya yake. Inasemekana 2pac alikuwa na ulimi fulan ambao akiongea dem yoyote hachomoi. we fikiria mtu kagombana na mumewe lakini katengenezwa hadi katengenezeka kwenda ku record [emoji23][emoji23][emoji23].
Baada ya ku record na kutafuna 2pac ndo akaweka bayana kila kitu hivyo uadui ukazidi na wale waliokuwa na malengo yao wakatumia chance hiyo kufanya yao. 2pac kabla ya ugomvi wake na Big alikuwa na ugomvi na serikali kwa kuwatukana wazi wazi viongozi wa nchi kutokana na ubaguzi wao wa rangi, alikuwa na ugomvi na polisi, FBI nk kwa sababu mama yake alikuwa katika list ya watu waliounda kundi la Black Panther lililokuwa vuguvugu la kudai haki za watu weusi.

Kwahiyo huenda serikali (FBI) walitumia mwanya huo kufanya yao, maana nyimbo zake ni kama vile zilikuwa zinawashtua na kuwafungua macho watu weusi wadai na kujua haki zao kitu ambacho serikali iliyokuwa inaongozwa na wazungu hawakukipenda.
Asante Kwa ufafanuzi mzuri
 
Wangeanza na hao mabinti wangeweza kupata chochote, lakini inaonekana police wanahusika au hawakutaka kufanya uchunguzi wowote wa maana, tukubali hii kesi ubaguzi umechangia sana isichunguzwe vizuri
Kweli mkuu hii kesi ilipigwa danadana kwa sababu wanazozijua wao.
 
Ubaya suge knight ana cv chafu hela hana na influence hana


Kuna video flani niliona mtandaoni kuwa anadai sijui shs ngapi benki eti pressure na kisukari kikapanda akazimia daah 😅😅😁
Pesa alikuwa nayo, sema wazungu wakiamua kukupukutisha wanakupukutisha kwa kukutengenezea kesi zisizoisha hadi unajikuta umebaki mtupu.
 
Kwa upande wangu naona wazee wa suti nyeusi walifanya yao baada ya kina 2pac na Big kusababisha vijana wa kiamerika hasa weusi kuwa na mienendo isiyofaa na kuuana ovyo. Haiwezekani kitu kidogo tu watu wanatwangana risasi kipuuzi. Vijana wangezidi kuharibika. Kwamba Didy ndo alihusika na mauaji ya BIG ni ngumu kuamini kwasababu BIG alikuwa ni kama ng'ombe wa maziwa kwa Didy kwa maana ya kwamba kupitia BIG huyo Didy alikuwa anapiga hela kwa kumsimamia chini ya label ya BadBoys. Jinsi Didy alivyo mpenda pesa isingekuwa rahisi kumuua mtu ambaye anamtengenezea pesa ndefu. Labda tumsikilize mpwayungu village anaweza kuwa na maoni tofauti.
 
Anakwambia kinyume na Mungu, hakuna binadamu ambae anaweza kumfanya yeye amuogope hapa duniani.
Alimchana hadi baba yake mzazi, baada ya dingi kujaribu kumtafuta Pac ili watumie wote pesa zake, na wakati hakuhusika na malezi yake toka utotoni hadi ukubwani.
Hahahaaaaa ,jamaa alikuwa ni mdogo ila IQ yake ilikuwa juu mno
 
Gene Deal hana undugu wowote na puffy, alikuwa bodyguard na ata sasa amekuwa akimsagia kunguni puff kila siku. Lil Cease pia sio ndugu wa damu, ni rafiki wa utotoni wa karibu sana. Suge aondoke mahakama ipi? We jamaa muongomuongo sana, mwenzio yupo jela ana miaka zaidi ya 25 inamsubiri eti alikutana na mama yake Biggie wakaondoka wote, we ni mzima au umekula kitu wewe? Dah
Suge anakesi zaidi ya 15,na kila inapofika tar huwa anapandishwa mahakamani..
Wakati anafanyiwa escoter ndipo Alionekana akiondoka na mama ake biggie...

Rudi kagoogle tena halafu uje na maelezo yako.
Tafuta documentary za SUGE na 2pac,ndio utanielewa.
sio umesoma udaku TMZ halafu unakuja kupayuka humu
 
Suge anakesi zaidi ya 15,na kila inapofika tar huwa anapandishwa mahakamani..
Wakati anafanyiwa escoter ndipo Alionekana akiondoka na mama ake biggie...

Rudi kagoogle tena halafu uje na maelezo yako.
Tafuta documentary za SUGE na 2pac,ndio utanielewa.
sio umesoma udaku TMZ halafu unakuja kupayuka humu

Shuge si alishafungwa na akatoka bado ana kesi gan tena?
 
Back
Top Bottom