Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.
BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.
Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
Ugomvi wa 2pac na Big haukuanza kwenye wimbo.
Ni hivi.. 2pac na Big walikuwa marafiki wakubwa sana maana wote ni wazaliwa wa New York, japo mazingira ya kimaisha yalisababisha waishi miji na maeneo tofauti yani 2pac akiishi LA California na Big akiendelea kuishi alipozaliwa New York.
2pac alimchukulia Big kama mdogo wake, hivyo mara nyingi alipokuwa anaenda kupiga show kadhaa maeneo mbali mbali ya nchi alimpa Big shavu na yeye aimbe ili kumtengenezea jina.
Mwaka 1994 2pac akiwa New York alipanga kwenda kumtembelea rafiki yake Big katika studuo yao ya Bad Boyz. Kama ilivyo ada ya marafiki, kabla 2pac hajaenda alimpigia sim Big na kumtaarifu kuhusu ugeni wake huo ambapo Big alikubali aende atampokea. 2pac alipofika katika jengo la studio wakati akapewa address na Big kwamba apande ghorofa ya ngapi kwa kutumia lift ya mjengo huo.
Wakati 2pac akiingia ndan ya lift ghafla wakaingia vijana wengine watatu ambapo wakati lift ikiwa katika michakato ya kupanda wakatoa bastola na kumtaka 2pac achojoe kila alichonacho. 2pac japo aliona jamaa wana bastola na wako serious kwa kile wanachoongea, lakini alikataa unyonge na kuamua kutoa bastola yake aliyokuwa ameificha kiunoni nyuma ya mgongo (kumbuka 2pac ameanza kutembea na bastola akiwa na umri wa miaka 12 kutokana na maisha ya kitaa na mshike mshike aliyokulia) wale jamaa walipoona 2pac anatoa bomba ndo wakaaona wamuwahi kwani wangefanya mzaha kidogo wangeangushwa wao.
Jamaa wakampiga risasi tano akapoteza fahamu (wao wakajua amekufa) na kuchukua kila alichokuwa nacho zikiwepo mkufu wa dhahabu na pete yake pamoja na hela wakakimbia.
2pac alipozinduka akajikuta yupo hospital afu si Big wala Bod Boyz yoyote aliefika kumuona, kitendo kilichomfanya 2pac ahisi kwamba lile tukio lilipangwa na Big kwani haiwezekani best friend wako apigwe risasi wakati akija kukuona afu wewe ushindwe kufika hospital na usimpigie hata simu. Kibaya zaidi wakati Big anatoa nyimbo yake fulan alivaa pete inayofanana na ile aliyoibiwa 2pac.
Hilo likamfanya 2pac aamini kuwa rafiki yake huyo alim set up hivyo na yeye hakupenda unafiki akaamuwa kuweka wazi kuwa kuanzia siku hiyo yeye na Big urafiki basi na kwamba sasa ni maadui rasmi. Kama hiyo haitoshi 2pac alipotoka jela tu akam seti mke wa Big watoe nae nyimbo inayoitwa You wonder why i call ya bi...t ch.
Mke wa Big (Faith Evans) pamoja na kwamb alifahamu ugomvi wa mumewe na 2pac lakini alikubali kwenda kuingiza kurecord nyimbo hiyo, na 2pac akatumia mwanya huo kufanya yake. Inasemekana 2pac alikuwa na ulimi fulan ambao akiongea dem yoyote hachomoi. we fikiria mtu kagombana na mumewe lakini katengenezwa hadi katengenezeka kwenda ku record 😂😂😂.
Baada ya ku record na kutafuna 2pac ndo akaweka bayana kila kitu hivyo uadui ukazidi na wale waliokuwa na malengo yao wakatumia chance hiyo kufanya yao. 2pac kabla ya ugomvi wake na Big alikuwa na ugomvi na serikali kwa kuwatukana wazi wazi viongozi wa nchi kutokana na ubaguzi wao wa rangi, alikuwa na ugomvi na polisi, FBI nk kwa sababu mama yake alikuwa katika list ya watu waliounda kundi la Black Panther lililokuwa vuguvugu la kudai haki za watu weusi.
Kwahiyo huenda serikali (FBI) walitumia mwanya huo kufanya yao, maana nyimbo zake ni kama vile zilikuwa zinawashtua na kuwafungua macho watu weusi wadai na kujua haki zao kitu ambacho serikali iliyokuwa inaongozwa na wazungu hawakukipenda.
Chini ni picha ya 2pac akitoka hospital, baada ya shambulio lake la New York.