Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Tetesi: P Diddy ahusishwa na kifo cha Notorious B.I.G

Akilihuru

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2022
Posts
1,512
Reaction score
2,980
Msaani maarufu wa Marekani na producer wa label ya Bad Boy record, anaejulikana kwa jina maarufu la P diddy, sasa tumbo joto baada ya mama yake na Christopher Wallace almaarufu Notorious B.I.G kumuhusisha msaani huyo na kifo cha mwanae kilichotokea mwaka 1997 huko Los Angeles, CA.

Inasemekana kwamba mama huyo amefanya uchunguzi wa kutosha na kujiridhisha kuwa huenda manager huyo wa Bad Boy record amehusika pakubwa na kifo cha mwanae, hivyo anapanga kufungua kesi ili ukweli ujulikane na kila aliehusika na kifo cha mwanae aweze kuchukuliwa hatua za kisheria kutokana na mauaji hayo.

Ngoja tusubiri kitachotokea, maana kwa R Kelly ilianza hivi hivi kimzaa mzaa matokeo yake mpaka leo bado mfalme huyo wa R&B ananyea debe.
 
Dah!,kila nikifikiria hao majamaa walivyoondoka wakiwa machalii naumia sana
Vifo vyao vilipangwa ndomana vilifanana.
2pac gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita 2pac.. 2pac.. 2pac... basi 2pac ile kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo akaanza kushambuliwa na gari ya majamaa waliokuwa ubavuni kwao.

Big nae gari yao ilipofika kwenye traffic light mataa ya kuruhusu upande wao kwenda yakafunga hivyo ikawalazimu kusimama. Ghafla pia wakatokea mabinti pembeni ya barabara wakaanza kuita Big.. Big.. Big.. basi ile Big kushusha kioo awapungie mkono hapo hapo na yeye akaanza kushambuliwa na gari iliyokuwa pembeni yao hadi kusababisha umauti wake.

Picha ya kwanza ni ya gari aliyoshambuliwa nayo 2pac.

Na picha zingine ni za gari aliyoshambuliwa nayo Big. Na chini kabisa ni madem waliomwita Big kabla ya shambulizi ili afungue dirisha. Na alipofungua tu akashambuliwa.
 
Attachments

  • IMG-20230326-WA0008.jpg
    IMG-20230326-WA0008.jpg
    34.4 KB · Views: 60
  • IMG-20230326-WA0005.jpg
    IMG-20230326-WA0005.jpg
    35.2 KB · Views: 58
  • IMG-20230326-WA0007.jpg
    IMG-20230326-WA0007.jpg
    29 KB · Views: 22
  • IMG-20230326-WA0009.jpg
    IMG-20230326-WA0009.jpg
    44.4 KB · Views: 55
Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.

BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.

Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
 
Yes ni visasi vyao tu ,2pac naye alivuka mipaka ,utasemaje wazi wazi kwamba umemtafuna mke wa BIG?
 
Dah!,kila nikifikiria hao majamaa walivyoondoka wakiwa machalii naumia sana
Theory zipo nyingi juu ya vifo vyao.
Wengine usema ni wazee wa suti nyeusi,waliwapaisha,wakawatengenezea bifu wakawapoteza,walianza kumua tupac alipotaka kujitoa kama Michael Jackson ushahidi alipoanza imba nyimbo za kuwatukana KISHA wakampoteza BIG Ili kuonekana kama kulipiza kisasi kupitia bifu zao.
Bifu lao lilikuwa la kutengezwa
 
Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.

BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.

Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
Uvumi ni mwingi lakini mpaka recently imeshathibitishwa aliyemuua 2pac ni Orlando Anderson,yule jamaa aliyepigwa na 2pac mapema siku ile kwenye pambano la Tyson na Bruce Seldon.

Na alikuwa mtu wake wa karibu.BIG alikufa sababu wapambe wa 2pac waliamini ye ndo alimuua.Kimsingi theories zipo nyingi Kuna hadi wanaoamini waliuawa na serikali ya marekani sababu ya bad influence Kwa vijana na makundi Yao ya east side na west side.

Na Kuna wengine wanaoamini pia hakufa sababu hawakuona mazishi yake.
 
Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.

BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.

Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....

Na sio wimbo tu,kuna siku 2pac alikwenda kwenye jengo maskani ya Big nadhani studio,akamjulisha big kuwa nipo chini nakuja lkn alipo ingia kwenye lift kuna jamaa wakamshambulia vibaya mnoo na kumpiga risasi ya bega….Big akawa anashangaa jamaa hatokei ndio akamtuma chawa wake akamcheki ndio akakuta sekeseke linaishia akarudi mbio na kumwambia Big.Baada ya hilo tukioa ndio 2pac akaanza kwenda kwenye media na nakusema big amehusika.baadae akatoa ule wimbo wa https://jamii.app/JFUserGuide them up nadhama kama sijakosea jina lake.

Sijui ni mazingira gani yalitokea 2pac akapiga picha na mke wa Big na ile picha ikawekwa kwenye jarida maarufu huko kwao na 2pac kudai kamla.
 
Pddy hawezi kumuu BIGGIE nakataa,kwenye gari alipokuwepo BIGGIE Kulikua na ndugu yake wa damu..

Eugene deal ambae ni bondia wa pddy(Mtoto wa kaka yake)
Lil cease mjomba wa B.I.G na member wa JUNIOR M.A.F.I.A wote walifia humo..

labda bimkubwa ameona mwanae amesahaulika anataka kumrudisha kwenye trend ya vichwa vya habari...
pia inaweza kuwa ni mpango wa SUGE KNIGHT kama rivarls kwa PDDY...

Pddy ndio power control kwenye kesi ya SUGE Na anamchomekea kweli,halafu mwezi uliopita mama yake B.I.G Alikutana na SUGE mahakamani na wakati anarudishwa jela waliondoka pamoja..

BEEF YA SUGE KNIGHT NA P.DIDDY HAIWEZI KUISHA
 
Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.

BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.

Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
Ugomvi wa 2pac na Big haukuanza kwenye wimbo.

Ni hivi.. 2pac na Big walikuwa marafiki wakubwa sana maana wote ni wazaliwa wa New York, japo mazingira ya kimaisha yalisababisha waishi miji na maeneo tofauti yani 2pac akiishi LA California na Big akiendelea kuishi alipozaliwa New York.

2pac alimchukulia Big kama mdogo wake, hivyo mara nyingi alipokuwa anaenda kupiga show kadhaa maeneo mbali mbali ya nchi alimpa Big shavu na yeye aimbe ili kumtengenezea jina.

Mwaka 1994 2pac akiwa New York alipanga kwenda kumtembelea rafiki yake Big katika studuo yao ya Bad Boyz. Kama ilivyo ada ya marafiki, kabla 2pac hajaenda alimpigia sim Big na kumtaarifu kuhusu ugeni wake huo ambapo Big alikubali aende atampokea. 2pac alipofika katika jengo la studio wakati akapewa address na Big kwamba apande ghorofa ya ngapi kwa kutumia lift ya mjengo huo.

Wakati 2pac akiingia ndan ya lift ghafla wakaingia vijana wengine watatu ambapo wakati lift ikiwa katika michakato ya kupanda wakatoa bastola na kumtaka 2pac achojoe kila alichonacho. 2pac japo aliona jamaa wana bastola na wako serious kwa kile wanachoongea, lakini alikataa unyonge na kuamua kutoa bastola yake aliyokuwa ameificha kiunoni nyuma ya mgongo (kumbuka 2pac ameanza kutembea na bastola akiwa na umri wa miaka 12 kutokana na maisha ya kitaa na mshike mshike aliyokulia) wale jamaa walipoona 2pac anatoa bomba ndo wakaaona wamuwahi kwani wangefanya mzaha kidogo wangeangushwa wao.

Jamaa wakampiga risasi tano akapoteza fahamu (wao wakajua amekufa) na kuchukua kila alichokuwa nacho zikiwepo mkufu wa dhahabu na pete yake pamoja na hela wakakimbia.

2pac alipozinduka akajikuta yupo hospital afu si Big wala Bod Boyz yoyote aliefika kumuona, kitendo kilichomfanya 2pac ahisi kwamba lile tukio lilipangwa na Big kwani haiwezekani best friend wako apigwe risasi wakati akija kukuona afu wewe ushindwe kufika hospital na usimpigie hata simu. Kibaya zaidi wakati Big anatoa nyimbo yake fulan alivaa pete inayofanana na ile aliyoibiwa 2pac.

Hilo likamfanya 2pac aamini kuwa rafiki yake huyo alim set up hivyo na yeye hakupenda unafiki akaamuwa kuweka wazi kuwa kuanzia siku hiyo yeye na Big urafiki basi na kwamba sasa ni maadui rasmi. Kama hiyo haitoshi 2pac alipotoka jela tu akam seti mke wa Big watoe nae nyimbo inayoitwa You wonder why i call ya bi...t ch.

Mke wa Big (Faith Evans) pamoja na kwamb alifahamu ugomvi wa mumewe na 2pac lakini alikubali kwenda kuingiza kurecord nyimbo hiyo, na 2pac akatumia mwanya huo kufanya yake. Inasemekana 2pac alikuwa na ulimi fulan ambao akiongea dem yoyote hachomoi. we fikiria mtu kagombana na mumewe lakini katengenezwa hadi katengenezeka kwenda ku record 😂😂😂.

Baada ya ku record na kutafuna 2pac ndo akaweka bayana kila kitu hivyo uadui ukazidi na wale waliokuwa na malengo yao wakatumia chance hiyo kufanya yao. 2pac kabla ya ugomvi wake na Big alikuwa na ugomvi na serikali kwa kuwatukana wazi wazi viongozi wa nchi kutokana na ubaguzi wao wa rangi, alikuwa na ugomvi na polisi, FBI nk kwa sababu mama yake alikuwa katika list ya watu waliounda kundi la Black Panther lililokuwa vuguvugu la kudai haki za watu weusi.

Kwahiyo huenda serikali (FBI) walitumia mwanya huo kufanya yao, maana nyimbo zake ni kama vile zilikuwa zinawashtua na kuwafungua macho watu weusi wadai na kujua haki zao kitu ambacho serikali iliyokuwa inaongozwa na wazungu hawakukipenda.

Chini ni picha ya 2pac akitoka hospital, baada ya shambulio lake la New York.
 
Attachments

  • IMG-20230326-WA0006.jpg
    IMG-20230326-WA0006.jpg
    47.5 KB · Views: 49
Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.

BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.

Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....
I'll be missing you: By Faith Evans moja ya pini iliyo hit sana enzi hizo
 
Uvumi ni mwingi lakini mpaka recently imeshathibitishwa aliyemuua 2pac ni Orlando Anderson,yule jamaa aliyepigwa na 2pac mapema siku ile kwenye pambano la Tyson na Bruce Seldon.Na alikuwa mtu wake wa karibu.BIG alikufa sababu wapambe wa 2pac waliamini ye ndo alimuua.Kimsingi theories zipo nyingi Kuna hadi wanaoamini waliuawa na serikali ya marekani sababu ya bad influence Kwa vijana na makundi Yao ya east side na west side.Na Kuna wengine wanaoamini pia hakufa sababu hawakuona mazishi yake.
Yote yanafanana na ukweli. Huenda kweli Orlando amemuuwa 2pac kwa mission aliyopewa na FBI, mtu, au watu fulan. Au huenda wazee wa suti wamefanya yao na jumba bovu kutegeshwa katikakati ya Big na dogo Orlando ili kuficha ukweli.
 
Na sio wimbo tu,kuna siku 2pac alikwenda kwenye jengo maskani ya Big nadhani studio,akamjulisha big kuwa nipo chini nakuja lkn alipo ingia kwenye lift kuna jamaa wakamshambulia vibaya mnoo na kumpiga risasi ya bega….Big akawa anashangaa jamaa hatokei ndio akamtuma chawa wake akamcheki ndio akakuta sekeseke linaishia akarudi mbio na kumwambia Big.Baada ya hilo tukioa ndio 2pac akaanza kwenda kwenye media na nakusema big amehusika.baadae akatoa ule wimbo wa JamiiForums' Community Engagement Guidelines | Mwongozo wa Ushiriki kwenye Mijadala them up nadhama kama sijakosea jina lake.

Sijui ni mazingira gani yalitokea 2pac akapiga picha na mke wa Big na ile picha ikawekwa kwenye jarida maarufu huko kwao na 2pac kudai kamla.
Swadakta kabisa ulichoandika kinafanana na kile nilichoandika kwenye post ya 14. Ebu isome ili kujua sababu halisi ya ugomvi wao.
 
Tupac alikuwa na hasira baada ya kutokea ugomvi baina yake na BIG kuhusu utunzi wa wimbo fulani, alikwenda kwenye vyombo vya habari na kuanza kujisifu kuwa amelala na Faith Evans mke wa BIG.

BIG akaona isiwe shida ammalize tu. Kundi la Tupac likaamua nalo lilipize kisasi na vijana wawili wadogo wakaondoka kiurahisi sana.

Faith Evans akatoa wimbo mmoja mkali sana wa kumkumbuka BIG chini ya uongozi wa P Didy....

unaitwa i will be missing you
 
Back
Top Bottom