P.Funk majani amekataza nyimbo za Ngwair kupigwa CloudsFm

Anazuia nyimbo zisipigwe kupitia twitter?
 
Duh!Mara ya Kwanza nilikuwa nafikiri watu wanawaonea wivu Cloudsfm kutokana na mafanikio wanayoyapata, lakini kama na kwa hili wamehusika basi naanza kupata wasiwasi na mwenendo wao.
 

Wakati Ngwea anabaniwa Majani alikuwa wapi na alifanya nini kumsaidia?leo ndio anajifanya ana uchungu sana mbona marhemu alipokwa hai hakuonyesha hayo machungu?Majani naye ni walewale tu
 
Hawa Clouds sasa inaonyesha kuwa ni janga kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii wanatakiwa kuungana kupambana
 
tunahitaji heshima ya kweli...hakukataza mwanzoni ili ngwear aendelee kuishi na kula mjini c unajua kuwa mwana kafa akiwa na hela zisizoendana na jina lake..!? au niaje wewe unajifanya hauelewi kuwa clouds ni wanyonyaji coz wameshikilia game...ilihitaji isipigwe marufuku ili mchizi apte hata hicho kidogo apatacho c unajua ni bora kupata kidogo kuliko nil?acha habari hizo
 
haya kweli jide alisema ruge asishuhudie mazishi yake na njimbo zake zisipigwe clouds,leo yamejirudia kweli ngwea alikuwa na bifu na clouds iweje leo wajitie wa kwanza kubeba bango la msiba wake na kupiga sana nyimbo zake hatuwaelewi hawa jamaa au ndio wasaga sumu ?
 
klauzi ef em...!WAZEE WA FURSA HAWA...kiama chao almost kimewadia......deeeekiii
 
Mh!sasa clouds kuna haja ya kujipanga upya maana mashambulizi yanazid kwao inamaanisha kuna jambo liko ndan ya clouds.

Mh hakuna kitu kama hicho huo ni wivu tu Clouds hawawanyonyi wasanii,kwani hao wasanii ni mbumbu kiasi gani hadi wanyonywe au hawawi na mikataba,mi naona wasanii wanaisiliba tu Clouds mbona wanapochukuliwa vichochoroni na Clouds hawalalamiki,na hadi wanakuwa ma supastar hatuwasikii kulalamika,mi nahisi wasanii wengi wanashindwa kuendena na viwango vilivyowekwa na Clouds,hao wasanii utakuta wapo na Clouds kwa miaka na miaka je huo ubaya walikuwa hawauoni ?leo hii ndio waanze kupiga kelele,akina Lady JD miaka na miaka walikuwa hapo na hatukusikia hizo porojo wanazozitoa hivi sasa,na pia kwani stesheni ni moja tu hadi eti mtu upate stress?huo ni uvivu wa kufikiri nje ya uwigo,hata matamasha yapo mengi tu na sio lazima yale ya akina Ruge& Co,tuache porojo kula unga hakutokani na stress,kwani hizo stress wanazo wasanii tu,kubwia Azam sembe ni uamuzi binafsi,acheni kila kitu kinachohusu kuporomoka kwa wasanii kuwasingizia Clouds,kifupi starehe na kulewa sifa ndio kunawaponza hawa wasanii wetu na si Kusaga na Ruga,visingizio havisaidii,sasa ishakuwa fasheni kila msanii anayeporomoka au anapata matatizo husingizia Clouds,au ndio mti wenye tunda ,kila mtu anataka kulipopoa?
 
Huu unaitwa unafiki wamemdidimiza kwa lipi? Nchi ina vituo vya redio zaidi 80
Hivi kama msanii mkali mkali tu, yaani ina maana clouds wakipiga nyimbo ndio mtu atang'aa? Ngwear kaanza kutumia.madawa miaka kibao namfaham vizuri jamaa yule, jamaa sana nlikuwa nakutana nae mitaa ya area c dom au sunrise pale,anakuja na washkaji zake muda wote wanatumia madawa leo eti imekuwa clouds,
 
Huyo f.ala mtoto wa mama mwambieni apige marufuku nyimbo zake zote alizoshiriki kuzitengeneza kutokupigwa na Clouds. Asiishie kwa wimbo wa Mikasi tu.

We ni f.ala mara kumi hamuoni hata aibu kupiga nyimbo za Marehemu wakati mlikuwa hamzipigi wakati yupo hai...yaani mnanyonya mpaka marehemu...
 
Kwa jinsi wanavyolalama mitaani kuhusu CLOUDS, utadhani ni redio pekee TZ

Sikiliza Bro,

Naona unaropoka ropoka tu,kwanza hakuna mtu anayelazimisha nyimbo zake zipigwe na wafu tatizo ni kwamba hawa wafu wanataka wamiliki hili gemu yaani bila wao wewe huwezi fanikiwa,muziki ni pamoja na shows na shows ni wadhamini na hawa wadhamini ni ndugu moja na wafu hapo msanii anatokaje?

Kwanini wasiache wasanii wafanye mambo yao bila kuwaingilia au kuwafuata fuata nyuma na wao wakafanya yao watapungukiwa nini?kila tamasha hapa mjini wanataka watie mikono yao wao ni nani?

Wadhamini nao hawasomi mchezo wanapelekwa pelekwa tu na hawa wafu wa Magorofani

Wakina Rick Ross wanakuja bongo wanabeba mamilioni ya hela wasanii wa bongo wanakuja kwenye shows na "daladala" na wanaambulia vilaki kadhaa!na bado wanatukanwa matusi makubwa na vitisho juu

KAMA MSANII AKIAMUA KU-HUSTLE KIVYAKE WAMUACHE AENDELEE NA SIO KUMFATA KILA KONA!....
 
Dah! Nimefatilia mijadala mingi ya Sanaa hapa JF kuhusu Clouds, kama hujui kuhusu Clouds au wasanii bora ukae kimya, Hivi mnajua kuwa Ruge anaitwa Rais wa Bongo fleva? Ni hivi kuna kipind kama nyimbo yako isipopigwa Clouds huwez kutoka, Clouds walikua wanaamua nani atoke Mwezi huu na atatoka, wakiamua nan wamshushe na atashuka, mara ngapi mnajiuliza mbona kuna wasanii wakali na hawasikiki tena? Clouds wanajua kuucheza mchezo wao, Clouds wangeweza kusema wamshushe Diamond ili msanii wao wa Vibe smooth atoke na ingekua hivyo, wasanii wengi wazuri waliamua kuacha Muziki, kidogo leo eatv na DTV vinaondoa Ukiritimba wao kwani Clouds tv haina Quality.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…