Mh hakuna kitu kama hicho huo ni wivu tu Clouds hawawanyonyi wasanii,kwani hao wasanii ni mbumbu kiasi gani hadi wanyonywe au hawawi na mikataba,mi naona wasanii wanaisiliba tu Clouds mbona wanapochukuliwa vichochoroni na Clouds hawalalamiki,na hadi wanakuwa ma supastar hatuwasikii kulalamika,mi nahisi wasanii wengi wanashindwa kuendena na viwango vilivyowekwa na Clouds,hao wasanii utakuta wapo na Clouds kwa miaka na miaka je huo ubaya walikuwa hawauoni ?leo hii ndio waanze kupiga kelele,akina Lady JD miaka na miaka walikuwa hapo na hatukusikia hizo porojo wanazozitoa hivi sasa,na pia kwani stesheni ni moja tu hadi eti mtu upate stress?huo ni uvivu wa kufikiri nje ya uwigo,hata matamasha yapo mengi tu na sio lazima yale ya akina Ruge& Co,tuache porojo kula unga hakutokani na stress,kwani hizo stress wanazo wasanii tu,kubwia Azam sembe ni uamuzi binafsi,acheni kila kitu kinachohusu kuporomoka kwa wasanii kuwasingizia Clouds,kifupi starehe na kulewa sifa ndio kunawaponza hawa wasanii wetu na si Kusaga na Ruga,visingizio havisaidii,sasa ishakuwa fasheni kila msanii anayeporomoka au anapata matatizo husingizia Clouds,au ndio mti wenye tunda ,kila mtu anataka kulipopoa?