Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

Hivi kwa kikosi alichokikuta Pablo mlitegemea maajabu gani?
ukikichambua kikosi kilichopo simba licha ya wachezaji kudrop viwango sio kikosi chakushindwa kucheza at least mpira wakueleweka pablo nabutuabutua yake hatufai...tena simba wasirudie kutuletea coach ambae aweki mpira chini,simba inastyle yauchezaji wake sio kupigapiga tu mipira mbele....hata falsafa ya pablo haieleweki toka kakabidhiwa timu yeye hana hata first eleven...
 
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Credit, MwanaSpoti

Updates,
View attachment 2245636 Matola miaka nenda miaka rudi anabaki hapo klabuni huku makocha wakuu wakiepa na kumuacha. Au kuna mbinu za siri huyu jamaa anazifahamu nini.
 
Ushawahi kupiga hata danadana?

Nimeanza safari ya mpira toka nipo kinda, kipindi hicho Hata shule sijaanza, kipindi tunacheza mipira ya makaratasi barabara I au uwanja wa nyumbani (uwani), ni katika kipindi kicho ndo nikajizoeza kupiga miguu yote.
Nilipoanza shule nikaendelea kukiwasha, zile match za madarasa vs madarasa (let's say for example: std iii vs std iv )au mikondo vs mikondo (A vs B) nilikuwa nakiwasha balaa. Kumbuka hapo napiga peku peku.

Kuanzia darasa la 5 hadi darasa la 6 mimi ndo nikawa mlinzi namba 4 tegemeo wa shule. Kamwili kadogo,ila wepesi, speed, akili na passion vilinifanya nikawa beck ninaewadhibiti washambuliaji wakali. Tackling, acrobatics,kutibua mipango, vilinifanya kuwa maarufu sana
pale shuleni na kijiji kizima. Ni katika kipindi hicho 2005-2006+ ndiyo nilianza kufanya mazoezi na wakubwa kwenye timu ya kijiji.

Match ya kwanza kupangwa kwenye timu ya wakubwa ilikuwa 2006, nipo darasa la 6 hapo, nilipangwa beki 2, niliboronga sijui woga!!! Nikatolewa.

Kuanzia mwaka 2007 nikiwa darasa la 7, mimi na mwili wangu mdogo,ndiye niliekuwa full back tegemezi wa shule na kijiji.

Kuanzia 2008-2010(form 1-3) mimi ndiye niliekuwa mlinzi tegemezi wa darasa, wa shule (sekondari) na timu ya kijijini (walikuwa wananifata kila kukiwa na match.

Kuanzia mwaka 2010-2011 (form 3-4) mimi ndiye niliekuwa mlinzi tegemeo wa darasa, shule, timu ya kijiji na timu ya kijiji cha pale shule ilipokuwepo.

Nilianza kuacha mpira 2012 baada ya kwenda advance.

SAMAHANI MKUU KWA KUKUPA JIBU REFU SANA. NIMEJIKUTA NAWAZA MBAAAALI SANA!! ENZI ZANGU, KAMA HENOCK INONGA MTUPU!! ka mwili kadogoooo ila ninaowazuia watu wanabaki wanasema natumia madawa kumbeee chini ya kapetii......siri ya mchezo ni NILIKUWA NAFANYA MAZOEZI SANAAAAAAAAA
 
Simba SC head coach Pablo Franco Martín has officially part ways with the Tanzanian club on a mutual agreement.

African Sports Today can confirm that Pablo is currently in negotiations with Amazulu FC 🇿🇦 and Raja Casablanca 🇲🇦 with Raja seems like the most preferred move.

Raja have offered the former Getafe coach $500,000 annual salary with other benefits while Amazulu is offering $25,000 Net monthly salary with a house, club car (with monthly fuel) and 2 business class tickets return (home) per season.
Aise wazungu wanakula batabsana wakija africa...mihela yote hiyo. Ila utakuta mzawa wanamkopa🤣🤣🤣🤣🤣
 
nabi kuanzia Sudan simba walimtaka ila alikuwa hajamaliza mkataba wake ,ile anamaliza simba wameshamchukua Gomes ,ndo maana Nabi alipofika Dar anahojiwa nawaandishi anasema Simba is the best club ,akaanza kukumbushwa upo Yanga. Hata hizi holidays alizokuwa anaenda wanasema anakwepa kurenew kwa sababu kuna ishu ya chini chini na Simba.
Inawezekana ni tetesi za kweli, maana kwenye mechi zote za Simba (za kwa Mkapa) NABI anakuwepo uwanjani, anaangalia sehemu ya kufanyia marekebisho.
 
Kumchinja kobe inahitaji timing, hapa simba tumefanya timing nzur sana kocha anayekuja atapata muda mzur wa kufanya usajili wake sasa next season moto utawaka
 
Sasa tunasubiri panga la wachezaji.
Mugalu
Wawa
Kagere
Lwanga
Dilunga
Boko
Mhilu
Gadiel

OUT

George Mpole
IN
Utashangaa bocco anakwepo hapo msimu ujao ,alaf et Wana malengo ya kufika mbali kimataifa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Credit, MwanaSpoti

Updates,
View attachment 2245636
Ni jambo jema. Kwa maana hajafikia malengo ya timu kwa asilimia 80 kafikia tu 20% ya malengo aliyopewa. Ila isiishie tu kwa kocha warudi kwa wachezaji mwisho wa msimu waache wale wazew wote kuanzia:-
1. Bocco
2. Mugalu
3. Nyoni
4. Wawa
5. Bwalya
6. Lwanga
7. Mhilu
8. Morrison
9. Gadieli
10. Jimyson
11. Kisubi
12. Kagere
13. Ally salum
14. Abdwasamadu kassimu
Nk
 
Back
Top Bottom