Pablo atimuliwa Simba SC, mwenyewe agoma kupokea barua

VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Credit, MwanaSpoti

Updates,
View attachment 2245636

Maamuzi magumu Ni Kuvunja kikosi karibia chote . Sio unatimua kocha unamuacha mugalu na boko.
 
Kama kawaida yetu wabongo wanaanza kuvaa viatu, then ndio wanavaa soksi.

Watamwondoa Pablo, then watawaondoa wachezaji na usajili wa wachezaji utasimamiwa na viongozi, baada ya kumaliza kusajili ndipo watakapo msajili kocha mwengine na kumpa malengo ya timu,kupitia wachezaji walio wasajili wao viongozi na kesho watamlaumu kwa matokeo mabovu kipitia wachezaji walio wasajilo wao.

Ndio maana wammtimua kocha mapema ili aje mpya kutengeneza timu mapema.
 
Kamati ya Usajili yatakiwa iondolewe maana wamehusika kwa sehemu kubwa na huu upuuzi

Wasimuache Matola, huyu ndiye Nyoka kwenye Timu
Mudi ndo anatakiwa kuondolewa,unageuzaje timu ya watu kuwa mkeo wa pili?
 
Wahakikishe kwamba this time cv ya kocha wanafanya background check vizuri...wenzetu hawa wanadanganyaga kwenye cv zao....
Tatizo la mpira wa nchi hii sio makocha hata muwalete wa madrid na wa liverpool, wasaidiane , hamtoboi, kocha inakuwaje asihusike kwenye usajiri?kweli kwa wenzetu hao, ni wa kudanganya cv zao?kitu ambacho ni kugumu, kwani cv ya kocha sio kama ya mlinzi
 
Ndio maana wammtimua kocha mapema ili aje mpya kutengeneza timu mapema.
Tupo hapa na kuhakikishia kocha mpya atakuja baada ya viongozi kumaliza kufanya usajili.

Labda kama sio mfuatiliaji wa soka la bongo ila kwa sisi tunao lifuatilia hizio ndio tabia za viongozi wa Simba na Yanga.
 
Kigwangala ni mshenzi sn, mpira wetu unawahitaji akina GSM na MO wa kutosha, Kingwala kipindi Simba ilikuwa imechoka mbona alishindwa kuisaidia?
Wanatakiwa akina GSM na Mo wengi ni kweli lakini hawatakiwi kuzigeuza timu mke wa pili.Kataa wahuni,Mudi ni muhuni.
 
Tupo hapa na kuhakikishia kocha mpya atakuja baada ya viongozi kumaliza kufanya usajili.

Labda kama sio mfuatiliaji wa soka la bongo ila kwa sisi tunao lifuatilia hizio ndio tabia za viongozi wa Simba na Yanga.

Sawa wakifanya hivyo tunarudi kule kule.
 
VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.

Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.

Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.

Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.

"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.

"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.

Credit, MwanaSpoti

Updates,
View attachment 2245636
naona makolo mmeanza kufanyia kazi hoja za kigwangala kimya kimya!hahaha
 
Back
Top Bottom