TANZIA Pacha waliotenganishwa, mmoja afariki dunia

TANZIA Pacha waliotenganishwa, mmoja afariki dunia

Hata kabla ya hiyo Op nilishangaa "advertise" nyingi mara,"Tutakuwa nchi ya tatu Africa kufanya Op hii".

Nikajiuliza tu,"Vipi isipofanikiwa? Record itaandikwa hivyohivyo."
Kwani Record inahusu kufanikiwa au kufanya?
Kama ni kufanya basi record itabaki hivyohivyo, kufanikiwa ni different story.
 
Haikufanikiwa mkuu ndio maana amefariki,watoto walikuwa wameungana kwa miezi zaid ya sita,wiki hajaisha tangu wafanyiwe upasuaji
Hivi unauelewa wowote kuhusu watoto walioungana? Au sababu uko huru tu kuongea.
 
Kwa mbwembwe na matangazo kama yote Walikataa kuwapeleka watoto watu India wakajitutumua , ona sasa matokeo yake , mnafanya majarbio kwenye maisha ya watu , hii imetokea pia majuzi , mwamba kaugua ghafla tumefika hospital fulan , daktar amefanya kaz yake , daah Wana tukaona hapa chenga , inabd tumkimbize hospital kubwa Zaid , aisee daktar si akazingua et anasema atakaa fresh tuuu , aisee kufika jion mchizi wetu akakata moto tulijilaumu kinyama kumsikiliza daktar wa mchongo
Yule binti daktari aliezunguka kwenye vyombo vya habari sijui anajisikiaje
 
Hiyo hatua waliyofikia ni kubwa sana.
Hata wright brothers walijaribu mara nyingi na kufail mara nyingi mpaka wakafanikiwa kutengeneza na kurusha ndege ya kwanza, then muendelezo na maboresho ndio leo kuna bombardiers na boeings. Siku zote hakuna straight way na shortcut au kufanikiwa moja kwa moja kwenye chochote kile especially kwenye maswala ya science ni trials and errors.

Kujaribu na kufail na kushindwa au kuanguka ndio njia pekee ya kujifunza makosa na kutorudia, kurekebisha na kuboresha mpaka kufanikisha lengo. Means hapo watajua wapi walipokosea na kosa halitojirudia tena.
Au kama unaogopa kujaribu na kufail au kushindwa basi hautofanya chochote kitakachofanikiwa maisha yako yote hapa duniani.

Watu wanaofanya Programming wanajua huu mchezo wa Trials, Errors na Debugging it's tedious and stagnating lakini mwisho wa siku lazima Code ikubali same kwenye maisha halisi sema ni way worse kama hivyo.

Failure Is the only Seed of Growth and Success / Development. ONLY WAY.
Wangejarbu Kwa sokwe Kwanza , baada ya hapo wangefanya Kwa binadamu tena under care ya wabobezi wa huko nje , next ndo wajisimamie, hata hapo inawezekana hata hawajui tatizo lilikuwa nn , wangemleta hata Ben Carson akawasimamia.. !! Ukweli Sisi wabongo ni wajuaji tupu , haya haya ya kuaminishana kipimo cha MRDT kumbe chenga tupu
 
Wangejarbu Kwa sokwe Kwanza , baada ya hapo wangefanya Kwa binadamu tena under care ya wabobezi wa huko nje , next ndo wajisimamie, hata hapo inawezekana hata hawajui tatizo lilikuwa nn , wangemleta hata Ben Carson akawasimamia.. !! Ukweli Sisi wabongo ni wajuaji tupu , haya haya ya kuaminishana kipimo cha MRDT kumbe chenga tupu
Unajuaje hapo hawakuwa chini ya wasimamizi na wataalamu wenye uzoefu?
Au unajuaje kwamba wao sio wataalamu wazoefu na ilikuwa mara ya kwanza tu kufanya hiyo operation Tanzania na sio kwamba ni mara ya kwanza kwao hao madaktari?

Ukipata majibu ya uhakika wa hayo maswali basi uko sahihi.
 
Nilitaka kushangaa tangu lini Tanzania tukawa serious kiasi hiki na kufanya vitu vikafanikiwa.
Sisi tuko bora sana kwenye kimasihara lakini vitu vya maana mhh...
Msinipopoe mawe wakuu
Ni kama vile ulitaka afe ili uiprove wrong nchi yako
 
1.Hivi wangewaacha ndio ingekuwa mbaya zaidi?
2.Mbona walikuwa na afya nzuri tu kabla ya operation?
3.Sasa wangeachwa wangeishije na kufaje?
Maswali ni mengi kuliko majibu
Sijui sana, ila nilichosikia ni kuwa....
1. Hatma ya maisha yao kiafya huenda ingekuwa mbaya kadri wanavyokuwa kwa kuwa viungo vyao muhimu vya ndani vimeunga kwa namna isiyoweza kuelewekwa vyema (complex conjoint)

2. Ni vyema operation hizo zikafanyika mapema zaidi wakiwa bado wadogo ikiwa tunataka kupata matokeo bora.

"If nothing can be done, take a risk"
Ben Carson.
 
Ndio tufanyie majaribio kwa malaika wetu kweli?
Wee unadhani hata wangeachwa wangeweza kuishi miaka mingapi wakiwa wameshikana. Haya mambo yanatokea kote duniani, tusiwabeze watu wa afya kwa kazi yao nzuri.
 
Procedure kama hizi unakuta kuna wataalamu wenyewe wanakuwa kutoka nje ya nchi wazungu ila wabongo wana assist... kuna kipindi walifanya kidney transplant yani zilikuwa zinareject balaa kibongo bongo mazingira tu yana changamoto sana vifaa hakuna
 
Back
Top Bottom