Ukiliangalia suala la kuvaa hereni katika upana wake, sijui kwanini kuvaa hereni kunahusishwa na ushoga! Katika tamaduni za baadhi ya makabila Tanzania (wasukuma, wamaasi, wagogo?, n.k.), wanaume uvaa mahereni tena makubwa na usuka pia. Kwa kweli uwa sielewi uvaaji huo kuhusishwa na ushoga.
Ukisema Mungu hakumleta duniani na sikio lilitoboka, je Mungu aliwaleta wanawake na masikio yaliyotoboka duniani? Je, Mungu alituleta duniani na kutuvisha suruali kwa wanaume na sketi/gauni kwa wanawake?
Ushoga ni tabia na hulka za mtu husika. Kwa mtazamo wangu mitindo (ambayo imekuwa defined na mwanadamu na siyo Mungu) haihusiani na ushoga, haswa ukizingatia baadhi ya mitindo hiyo imekuwa sehemu ya utamaduni wa kitanzania na hata kiafrika kwa baadhi ya makabila.