Paco Decor amefariki

Paco Decor amefariki

Status
Not open for further replies.
Sema huu uandishi wa mabloger uchwara huu, eti oh my god. Was he sick or what? Juzi tu nasikia alikuwa ICU Leo naambiwa he is dead!
Sasa kama uliambiwa yuko ICU halafu unashangaa kama kafa ghafla, we unafikiri ICU wanapiga disco Kule?
 
Ukiliangalia suala la kuvaa hereni katika upana wake, sijui kwanini kuvaa hereni kunahusishwa na ushoga! Katika tamaduni za baadhi ya makabila Tanzania (wasukuma, wamaasi, wagogo?, n.k.), wanaume uvaa mahereni tena makubwa na usuka pia. Kwa kweli uwa sielewi uvaaji huo kuhusishwa na ushoga.

Ukisema Mungu hakumleta duniani na sikio lilitoboka, je Mungu aliwaleta wanawake na masikio yaliyotoboka duniani? Je, Mungu alituleta duniani na kutuvisha suruali kwa wanaume na sketi/gauni kwa wanawake?

Ushoga ni tabia na hulka za mtu husika. Kwa mtazamo wangu mitindo (ambayo imekuwa defined na mwanadamu na siyo Mungu) haihusiani na ushoga, haswa ukizingatia baadhi ya mitindo hiyo imekuwa sehemu ya utamaduni wa kitanzania na hata kiafrika kwa baadhi ya makabila.
Nakubaliana na wewe na hasa sisi wasukuma. Kipindi cha nyuma miaka ya 1990 nilikuwa mpenzi sana wa ngoma za kienyeji za kisukuma maarufu kwa jina la beni. Ilikuwa wachezaji wanavaa hereni na mabanio ya nywele wengine wakisuka. Malenga maarufu Ng'wanankome alikuwa hadi anacheza akiwa na perfume huku akiwa kavaa wigi na kujipulizia kila mara. Ushoga no tabia ya mtu na nasikia hata bungeni wamo (sijui watanifuatilia kwa kutaja bunge!!!?)
 
Huyu jamaa alikuwa close na kina dada wengi wa mujini
 
Sioni sababu ya ku justify ujinga. Tunajua hereni zinazovaliwa sasa na hawa vijana masharo wa dar siyo zile za kimasai wala za mababu zetu bali mitindo iliyoigwa Marekani.

Unatofautisha vipi uvaaji wa hereni wa Marekani (haswa kwa watu weusi) na uvaaji wa hereni wa Afrika? Kwa maana hawa wote wametokea katika mzizi mmoja! Na kama kulikuwa na tamaduni za baadhi ya makabila kuvaa hereni, kwanini isiwe kwamba hao wamarekani walibeba hizo tabia na kwenda nazo utumwani? Na kwa kuwa mitindo siyo static, ina evolve, hizo hereni wanazovaa sasa ni matokeo ya tamaduni za uvaaji wa hereni wa kitambo.

Wavaaji wa hereni hata walioko Marekani siyo watu wanaoheshimika sana na mostly kimaadili ni questionable. Iweje sisi huku africa tuwaone watu wa kawaida?.

Ebu weka ushahidi unachokisema. Kama ingekuwa hivyo unavyodai, basi wavaaji hereni wangekuwa hata hawapati ajira Marekani. Unauliza iweje huku Afrika tuwaone watu wa kawaida, wapi wanaonekana siyo watu wa kawaida? Je, unawashangaa pia wamaasai kusuka nywele na kuvaa nusu uchi? Pengine utasema ni utamaduni wao! Na ukiona mzungu kavaa kama maasai utakuwa wa kwanza kumsifia!

ukweli utabakia kuwa uvaaji wa sasa wa hereni kwa wanaume unahusishwa na maadili machafu na hupati heshima popote labda kwa watu wenye silka kama yako.

Ukweli huo nani kaudefine? Maana masuala ya tamaduni ni rahisi sana kuwa na prejudice. Na suala la kupata heshima popote (unamaanisha dunia?) linadhiirisha jinsi ulivyo ndani ya box. Hapo Kenya tu, jaji mkuu wao anavaa hereni! Sasa sijui kuwa jaji mkuu siyo heshima? Maadili machafu unayaona kwa wavaaji hereni tu? Hivi wateja wa hao mashoga nao ni wavaaji hereni? Braza, mbona unafikiri kama mtoto wangu wa miaka 3?!?
Eti silka kama yangu! Mimi siyo mvaaji wa hereni, lakini kutokana na nilichokieleza juu ya chanzo cha utamaduni wa kuvaa hereni, sioni shida wala aibu kulisemea hili suala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom