Siku zote mashetani na mabwana zenu ndio mnaoamini mwenye ushirikina. Mimi sijawahi kushiriki wala kuamini katika ushirikina katika maisha yangu yote, na kamwe haitakuja kutokea. Japo ni mwanadamu, amvaye hawezi kukosa mapungufu, lakini kamwe mapungufu hayo hayawezi kuwa ushirikina au kumdhulumu mwanadamu mwenzangu, kama yanavyofanya hayo mashetani, dhuluma za kuwateka watu, kuwabambikia watu kesi, ufisadi, na mauaji ya wanafamu. Kama utakatifu ungekuwa unapimwa kwa kutofanya hayo tu, nina hakika ningeitwa mtakatifu. Mimi nakueleza uhalisia: Hakuna padre wa kuua Albino au mwanadamu yeyote. Lakini ufahamu kuwa tangu kale, siyo Tanzania tu, lakini katika nchi mbalimbali, shetani amewahi kupandikiza watu wake kwenye kundi la mapadre eti ili kulipeleleza au kulihujumu Kanisa. Na hao ndio huwa wanafanya mambo ya ajabu yasiyoendana na imani ya ukatoliki. Na hayo yalifahamika tangu kale, ndiyo maana Yesu alisema kuwa mtawatambua kwa matendo yao. Siyo kila asemaye ni padre lazima awe padre, wala si kila asemaye ni mkristo huwa ni mkristo. Kumjua Padre wa kweli na mkristo wa kweli, tazama matendo yake.