Kuna sehemu tunachanganya mambo, nafkiri tuuelewe umma unachokitaka kwa sasa kwamba baada ya makosa kutendeka basi wahusika wawajibike, kweli tunapojaribu kupingana na huu ukweli ndio tunapozidi kufanya mambo yawe magumu zaidi.
Nafkiri tunafahama.
Padre alieua albino tunafahamu hatua zote alizochukuliwa, kubwa zaidi ikiwa ni kanisa kujitenga nae ili kuviachia uhuru vyombo vinavyohusika kuendelea na taratibu zake... sasa wenzangu tunaopenda kuitumia hii kama silaha ya kuwadhohofisha hawa nafkiri tuangalie kitu kingine.
Wapo tunaopenda pia kukumbushia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia, yes, vilikuwepo na yawezekana labda vipo.. lkn ukitaka kujua msimamo wa kanisa juu ya jambo hili kwa watoto, hudhuria misa zao za kupewa upadre, kuna viapo kwa sasa wanaapa mbele ya watu, na huko mbele wanaahidi kwamba ikitokea jambo amelifanya ni lake wala kanisa lisihusishwe, kumbe jamaa wameona ni vizuri jambo kuliweka sawa mbele ya watu na Mungu ili kuendelea kulinda kanisa na utakatifu wake. Hata serikali inaweza kujitenga na wale wanaofanya mabaya katika jamii ili kuendelea kujijengea imani katika umma wake na hiki ndio kitu watu wanataka kuskia na kuona, lkn sasa hawakiskii wala kuyaona yakitendeka.
Mimi binafsi siamini kama Serikali inateka na kupoteza watu ila swali ninalojiuliza kila siku ni kwamba...
"Ni kweli Serikali yetu na vyombo vyake vyote vya ulinzi na usalama vimeshindwa kubaini watekaji ni akina nani, na watu wote waliotekwa mpaka leo kwamba wako wapi?" Hii habari ya kwamba tunaendelea na uchunguzi kwa miaka yote kwa (mfano Ben Saanane) unaweza kusema kuna umakini kweli kwenye vyombo vyetu?
Asante...
#mamaanatosha