Padre wa Kanisa Katoliki Italia afukuzwa baada ya kuhubiri kwamba Papa Francis ni 'Masonic' na 'Anti-pope'

Padre wa Kanisa Katoliki Italia afukuzwa baada ya kuhubiri kwamba Papa Francis ni 'Masonic' na 'Anti-pope'

Fr. Ramon Guidetti wa Italy amefukuzwa tar 3 January 2024 baada ya kuhubiri kwamba papa francis anakinajisi kiti cha Mtume Petro (anti-pope) na anatimiza matakwa ya wapinga Kristo.

Hio ilitokea alipokua anahubiria tarehe 31 December 2023 siku iliokua ni kumbukizi ya kifo cha Papa Benedicto wa 16. Alienda mbali zaidi na kusema kwamba Papa Benedicto ndie alikua papa wa kweli lkn huyu wa sasa ni 'Antipope and masonic jesuit'

Ikumbukwe pia wakuu kadhaa ndani ya roman catholic walitumia siku ya trh 31 ambayo ni kumbukumbu ya kifo cha papa benedicto wa 16 kutoa yao ya moyoni dhidi ya uendeshaji potofu wa papa francis wakiwemo makardinali wawili waliokua karibu sana na papa benedicto wa 16

Soma zaidi hapa Italian priest excommunicated for slandering Pope Francis during Mass

Maoni yangu, mapadri, maaskofu wote wanaofukuzwa wafungue kanisa jipya ambalo litafuata kanuni za conservative catholics lkn tu lisimtambue papa kama walivyofanya orthodox, wakifungua hilo kanisa mimi nitakua muumini wa kwanza hapa Tanzania, huyu papa wa sasa 'Tumepigwa'
Hivi ni nchi gani iliyopo hapa duniani kwa sasa ambayo imenusurika na janga la Mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja ??? Ipo nchi kama hiyo??

Kwa sasa, ni vigumu sana watu kumuelewa huyu Papa, lakini kwa kadiri muda unavyoenda pole pole watu wataanza kumuelewa. Itachukua muda mrefu sana watu kuja kumuelewa fully kabisa juu ya nini hasa huyu Papa anamaamisha kuhusu huu Waraka wake. Ni suala la muda tu. Dunia kwa sasa, hasa watu wengi wa bara la Afrika bado wapo katika denianism stage.
 
Lakini ndiyo watu wema wengi wetu wa 60,70&80s tumezaliwa kwenye hospital zao kuwaje wasitufanyie hayo mambo ya kishetani?

Mkristo yeyote hupaswi kumuona binadamu mwenzako kama kichaka cha shetani cha kufanya muombee arudi kwa Mungu unaemuamini wewe hao unaowaona hapa shetani wao wanakuombea wewe heri usiwe mwepesi kuhukumu.
je ukiambiwa katoliki ni babeli mkuu mama wa makahaba anayelevya wakuu wa nchi kwa mvinyo wa divai yake utaelewaje hapo?
 
Wasabato humuhusisha papa na alama ya kishetani ya 666. Wanadai iwe isiwe papa ndiye ataamuru namba hii kutumika na kila mwanadamu ktk dunia hii.

Sasa naanza kuwaamini wasabato.
achana na wasabato hawajui maana ya mnyama na namba 666 wanakanganya sana
 
Ungekuwa upo deep kiasi cha kuyajua mengi kunishinda ungeshanielewa pale juu nilipokwambia uombe hekima kwanza ndiyo ujadili haya mambo ya imani.

Imagine huijui hata sekunde moja ya pumzi yako lakini unathubutu kusema hapa kwamba watu fulani ni wa shetani,who are you bro?mimi nitaenda motoni unajuaje kama nitaenda motoni mzee?just kwa sababu ni Mkatoliki?umeujuaje utendaji wa Mungu?umeijuaje hekima ya Mungu ktk kuwahukumu wale waliojitahidi au kujaribu kumtafuta lakini wakawa hawapo sehemu sahihi?

Usijimilikishe wewe ukuu,Mungu ana taratibu zake siyo mimi wala wewe anayezijua itoshe kusema tusali kwa imani zetu tukingoja yajayo hakuna mwenye mamlaka ya kumuhukumu mwenzake.
1 yhn 3,8 atendae dhambi ni wa ibilisi;
 
je ukiambiwa katoliki ni babeli mkuu mama wa makahaba anayelevya wakuu wa nchi kwa mvinyo wa divai yake utaelewaje hapo?
Nitamuuliza anayeniambia yeye maneno hayo aliambiwa na nani hata mimi nisiyajue au kuyasikia?
 
Mimi Mkatoliki nina dhambi sawa sikatai!

Sasa wewe msafi sana nenda kamsome Yohane huyo huyo ktk Sura ya 8 mstari wa 7 halafu rudi hapa uniambie aliyemkariri alikuwa anakukataza nini na hapa unafanya nini?
Tatizo wakatoliki hata maandiko hamyajui hakuna walaka wa kwanza wa yohana 8,7
 
vipi kwa waislam huendi huko?
Yaani siku mimi nikiwa siyo Mkatoliki nitakuwa either atheist au marehemu hii ipo clearly kabisa Mungu aonae sirini anajua,nilipofikia sina muda wa kwenda kufundishwa jinsi ya kuwa hater na mbinafsi.

Imani nyingi nje ya Kanisa Katoliki zinashambulia wale wasiokuwa wenzao hazipo kwa ajili ya kujengana kiimani,mtu kumuita mwenzake shetani,kum-provoke anachokiamini au kumnanga siyo mwenzao ni kitu cha kawaida lakini ndani ya Kanisa Katoliki hakuna siku Padre,Askofu au Shemasi atasimama madhabahuni na kusema wale ni wa shetani sisi ni wa Mungu lakini hao wengine tangu mwanzo wa ibada mpaka mwisho wa ibada ni majungu tu.
 
Tatizo wakatoliki hata maandiko hamyajui hakuna walaka wa kwanza wa yohana 8,7
Sawa wewe msafi sana usiyekuwa na dhambi na unayejua sana maandiko Matakatifu rudi ktk post yangu nionyeshe wapi nimeandika neno “WARAKA WA KWANZA WA YOHANE”

Upo huru usije kusema nimerudi ku-edit soma uliponi-quote original post yangu umeishikilia wewe siwezi kui-edit,kama Mungu unayemuamini ndiye amekupa utashi huu ndugu unastahili kujiuliza mara mbili mbili ni Mungu kweli au kitu gani?

Brother hekima,nasisitiza hekima binadamu unayepumua ukikosa kitu kinaitwa hekima wewe ni bure siyo kwa jamii tu hata kwa Mungu wako.
 
Back
Top Bottom