Padri Dkt. Kitima: Sikujua sababu ya kuitwa Ikulu, msimamo wetu ni ule ule, hatukubaliani na IGA

Padri Dkt. Kitima: Sikujua sababu ya kuitwa Ikulu, msimamo wetu ni ule ule, hatukubaliani na IGA

Katibu Mkuu wa Baraza La Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Dkt.Charles Kitima amesema kuhudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa Host Government Agreement (HGA) iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma siku chache zilizopita haimaanishi kwamba wamekubaliana na mkataba wa Bandari kwani kulikuwa na mazingira ambayo yeye kama yeye asingeweza kujua nini hasa ameitiwa na asingeweza kuweka masharti kwa Rais baada ya kupewa mwaliko ambayo yeye (Kitima) hakuwa anajua lengo lake.

Kitima ameyasema hayo baada JAMBO TV kutaka kupata ufafanuzi wa kile ambacho kilitokea Ikulu Dodoma ambapo kwenye hafla ya kusaini mkataba wa HGA kauli mbalimbali zilisikika zikisema hata wale ambao mwanzoni waliukosoa Mkataba ule (IGA) nao wamehudhuria halfa ya utiaji saini Mkataba wa (HGA) kitendo ambacho kiliashiria kubadili kwao msimamo kuhusu waliyokuwa wanaeleza kama mapungufu ya Mkataba wa makubaliano kati ya serikali ya Tanzania na Dubai wa uendeshaji wa Bandari za Tanzania

" Hatujaona mabadiliko kimaandishi, Tunasimama na Tamko la Maaskofu, tukiona kimaandishi mabadiliko yaliyofanywa kwenye IGA ndipo tutaonana kama mapungufu yamefanyiwa kazi" amesema

Dkt. Kitima amesisitiza kwamba bado msimamo wa Kanisa Katoliki Tanzania ni kwamba IGA inayo mapungufu hivyo hawajabadili msimamo.

Jambo TV
Hakuitwa, Kaalikwa. Asiseme upngo.

TEC na network yao yote ya aakatoliki wasijuwe wanaenda kufanya nini?

Uongo huo.
 
Kwani yeye ni nani kujua siri za nchi kushinda wa Tanzania 60m......hizo phd za theology zina wanadanganya wanata kuji pima umbavu wao na "State"
Kwenye PhD umepuyanga hao jamaa wamejaa watalaamu wa fani tofauti theology ni degree mmoja TU ,mawe Mengine fani tofauti huyo kitime mwenyewe angalia profile yake utachoka ,shule zinagongwa katoliki sio Mzaa padri kuwa na degree sita kawaida sana
 
Kwani yeye ni nani kujua siri za nchi kushinda wa Tanzania 60m......hizo phd za theology zina wanadanganya wanata kuji pima umbavu wao na "State"

Mambo mengi yaliyofanywa kwa siri na wakati mwingine kutumia nguvu sana yaliishia kutia hasara nchi na kunufaisha mafisadi.

Hatusemi kwa nia mbaya ila naomba unikumbushe manufaa ya gesi ya Mtwara, naomba unikumbushe faida za mkongo wa Taifa.

Tuanze na hayo machache
 
Kwani yeye ni nani kujua siri za nchi kushinda wa Tanzania 60m......hizo phd za theology zina wanadanganya wanata kuji pima umbavu wao na "State"
Jibu hoja usipoteze muda na ngonjela za kichawa!
 
Kwani yeye ni nani kujua siri za nchi kushinda wa Tanzania 60m......hizo phd za theology zina wanadanganya wanata kuji pima umbavu wao na "State"
Huna hoja ndugu yangu. Unabwabwaja, hakuna unachokijua. Mtu mwenye uelewa angejibu hoja kuliko kuropoka, kama ulivyofanya.
 
Wakaanzishe serikali Yao huko vatikan. Watuachie nchi yetu ya aman.
Huna hoja ndugu yangu. Unabwabwaja, hakuna unachokijua. Mtu mwenye uelewa angejibu hoja kuliko kuropoka, kama ulivyofanya.
 
Wapuuzi wakubwa nyie, ubovu wa IGA ni upi haswa?. Mliweza kuiona IGA baada ya kuvuja msitegemee kuja kuuona mkataba wa biashara kati ya Dubai na Tanzania. Kwanza ni kosa kisheria kuonyesha vipengele vya mkataba wa kibiashara, kinachoandikwa mle ni siri ya pande mbili. Pili serikali haiwezi kuingia gharama kubwa ya utetezi dhidi ya wote watakaoishambulia mitandaoni wakiongelea mikataba tena ambayo uelewa mpana wa watakaohoji ni mdogo sana.
Umeandika ujinga mtupu, mjinga unayeamini kuna siri kati ya serikali isiyoaminika na wawekezaji, na unairuhusu hiyo siri iwepo! huna tofauti na n'gombe anayeswagwa kupelekwa malishoni.

Hapa ndipo umepigilia msumari wa ujinga kwenye jeneza lenu na Samia, mkataba wa biashara uwe siri wakati unahusu rasilimali ya taifa ambayo ni mali ya umma wote?

Huna akili kabisa.
 
Wagalatia hasa kutoka katoliki huwa wanajiaminisha kuwa kanisa ndio lina run hii nchi, sasa wanaumbuliwa waziwazi
Hao ni Wagalatia wasiojua. Mimi pia ni Mgalatia lakini naamini katika misingi ya mgawanyo wa mamlaka.
 
Kwani yeye ni nani kujua siri za nchi kushinda wa Tanzania 60m......hizo phd za theology zina wanadanganya wanata kuji pima umbavu wao na "St
Ungefahamu nguvu ya TEC wala huu utumbo wako usingeuongea! State is nothing to TEC!
 
Wala usimtilie maanani huyo Fr. Kitima. Hata Vatican yenyewe inamchukulia poa tu ndio maana ma junior wake wamepata u-Askofu kama vile Baba Askofu Msonganzila, Baba Mfumbusa kutaja wachache.
Nani alikwambia Uaskofu ni Dili?
 
Ungefahamu nguvu ya TEC wala huu utumbo wako usingeuongea! State is nothing to TEC!
Natamani kutumia neno "stupid" lakini ebu nijitahidi kujizuia.....hujui unacho ongea hujui state ni nini, TEC is nothing to the state haitambuliki na katiba ya Jamhuri wala mihimili ya nchi na sio NGO.....nyie wanavo wapigisha magoti na kuwapora pesa kwa jina la sadaka unafikiri ni kubwa kwa kila mtu loh, ficha ijinga wako mkuu.
 
Umeandika ujinga mtupu, mjinga unayeamini kuna siri kati ya serikali isiyoaminika na wawekezaji, na unairuhusu hiyo siri iwepo! huna tofauti na n'gombe anayeswagwa kupelekwa malishoni.

Hapa ndipo umepigilia msumari wa ujinga kwenye jeneza lenu na Samia, mkataba wa biashara uwe siri wakati unahusu rasilimali ya taifa ambayo ni mali ya umma wote?

Huna akili kabisa.
Kuhusu rasilimali za taifa hakuondoi mkataba kuwa ni siri ya pande mbili. Mjinga ni wewe uliyedhani kuvuja kwa mkataba wa IGA ni haki yako ya kuujadili, lile lilikuwa ni kosa la kimfumo ambalo limesharekebishwa tayari, hutakuja tena kuona mkataba wa aina ile.

Mjinga ni wewe unayedhani kuwa mmiliki wa mali za taifa ndio kuwa na kibali cha kujadili kila kinachojadiliwa na kufanyika, kama ni hivyo hakuna sababu ya kuwepo kwa nyaraka za serikali.

Hili la DP World mmepigwa na kitu chenye ncha kali utosini, tafuteni mada nyingine ya kujadili.
 
Usinifokee, nani alikuambia Kuna mihuri ya challenging mnayo wachache… peleka kichefuchefu chako kule

Nimeweka very simple understanding hapo

Naona unawashwa
Umetumia lugha usiyo ielewa vizuri, na ulipojibiwa katika lugha ile ile akili zote zikakuruka kichwani.
Watu wa aina yako ndio waliojazana huko ndani ya serikali hii ya kitapeli sasa hivi. Hakuna lolote la maana mnalolijua; kazi ni kutumia ulaghai na ujanja ujanja tu; toka juu kwa mkuu wenu, hadi ngazi za chini kabisa.
 
Back
Top Bottom