Padri Henry Rimisho wa Kanisa Katoliki atunukiwaa PhD ya Architecture

Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.

Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.

Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.

Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).

Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!

Malisa GJ
FB_IMG_1638646856214.jpg
 
Mimi Padre Dr. Henry Rimisho (AJ) Natimiza miaka 20 ya Ukuhani wangu Karibu utabasamu nami kumshukuru Mungu

Naomba uniombee niendelee kuwa Padre wa mfano katika maisha yangu.

Naomba niseme machache kuhusu Mimi.

Mimi pia Mhadhiri wa chuo kikuu Cha Ardhi Der es salaam( Architect Dr. Henry Rimisho (AJ)

Majina yangu pamoja na vyeo vyangu ni Rev. Fr. Capt. DR. Architect Henry Rimisho (AJ)

Nilipewa Daraja takatifu la Upadre Tarehe 14/7/2001 katika Kanisa la kiaskofu la Kristo Mfalme Jimbo Katoliki la Moshi na Hayati Askofu Amedeusi Msarikie aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Moshi.

Mimi ni Padre wa Shirika la Mitume wa Yesu.
Tangu nipewe Daraja takatifu la Upadre nimekuwa nikifurahia Upadre wangu, na ninafurahia kuwatumikia watu wa Mungu.

Mwenyezi Mungu ameniteua Kati ya wengi nimtumikie, Asante Mungu wangu.

Maombi yangu kwako.

Nawaombea wote!
Mnaotamani KUPATA watoto mjaliwe.neema hiyo

Mnaotamani KUPATA waume na wake wa maisha yenu, mjaliwe hayo

Mnaotamani kuona watoto wenu wanabadilika wanakuwa wa mfano, mjaliwe hivyo

Mnaotamani kupokea Uponyaji kwa njia mbalimbali hasa kwa MAOMBEZI ya na nguvu ya Ekaristi, Yesu mwema awaguse maumivu yenu.

Mnaotamani kupiga HATUA za kimaisha kwa namna yeyote, Mungu awafanyie wepesi

Enyi mnaolia machozi yenu yakawe Kicheko kwa neema ya Mungu.

Nawabariki
MBARIKIWE mnapotoka na mnapoingia, MBARIKIWE mjini na mashambani, MBARIKIWE KILA mnachokifanya.

Baraka za Mungu Baba, za Mwana na Roho Mtakatifu zishuke na kukaa nanyi daima

Amina.
 
Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.

Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.

Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.

Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).

Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!

Malisa GJ
View attachment 2033162
 
Hizo sio karama si degree.Karama anatoa Mungu (Roho Mtakatifu) na uwa hatoi ukomando au PHD .Mfano wa karama ni kukirimu,unabii,uponyaji,kupambanua roho n.k
 
Uzi uunganishwe, Halafu ni Architect, sio Architecture, na ni chuo kikuu Ardhi, sio chuo kikuu cha Ardhi
Inasikitisha sana Mtu anakuja na Uzi wa 'Kumshadadia' Mtu wa Mahaba yake nae halafu katika Maelezo yake marefu kuna Makosa lukuki ya 'Kiuwasilishaji' kama ambavyo umeyaainisha hapa Mkuu.

Umejua Kumuumbua kweli kweli na nadhani aliko sasa anajiona mdogo kama Kidonge cha 'Piriton' tu Kudadadeki zake.

Cc: DIDAS TUMAINI
 
Wana Jamii From!

Bila yakupoteza muda naomba kufahamu jambo moja zito ambalo kwa uelewa wangu nimeshindwa lipatia majibu!

Hivi inawezekana vipi Mtumishi wa Mungu Padre awe mwanajeshi tena komandoo??

Picha hapo chini ni Padre Henry,ambaye ni mwanajeshi komandoo,ambaye katunukiwa PhD yake ya Architecture!

Ongeza bidii kwenye kufanya mambo ya msingi na uache wivu.
 
Back
Top Bottom