Kuna brother wa kitaa Sengerema anaitwa Bosco Mosha (Maneno anaifahamu hii familia), kwasasa yupo Glasgow kule group la home huyu Padre ni classmate wake alisoma naye Uru Seminary, na akiwa Padre kabatiza watoto wa Bosco. Kweli ni Padre wa hilo shirika linalotajwa, sio Padre wa jimbo (kwa wakatoliki wanajua tofauti). Shirika lake lilimtuma South Sudan kutoa huduma ya kiroho na kule aliingizwa SPLA (Jeshi la Ukombozi la Sudani Kusini) na Garang. Then alipata basic training na kuwa Chaplain (mhudumu kiroho) kwenye Jeshi la South Sudan, vyeo hivyo alipandishwa hukohuko South Sudan, hopefully tunafahamu upandishwaji wa vyeo kwa SPLA ulikuwa wa mtindo gani, very politically kwa interest tofauti. Kwa taarifa za brother Bosco hata hizo uniform ni za South Sudan (SPLA). Ila hana uhakika wa cheo cha Meja, sio Komando ila anapenda kucheza Karate na Kung-fu kama part ya mchezo na kujiweka fit, kilichozua mjadala ni andishi la kipotoshaji la Malisa...😄😄