Padri Kitima: Bado hatujamsikia Rais akisema neno 'Samahani' kwa yaliyotokea

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Padri Kitima leo kwenye mahojiano maalum amesema japo Rais alikiri kutokea kwa changamoto na kusema matukio hayo hayakuwa ya kawaida na hayatapaswa kujirudia, bado hajatamka neno "samahani" kwa niaba ya watendaji wa serikali yake.

"Ni kweli Mheshimiwa Rais alisema yaliyotokea hayakupaswa kutokea na hayatatokea tena. Lakini bado hatujamsikia akisema 'samahani' kwa niaba ya watendaji wake waliokusababishia wananchi maumivu hayo," alisema kiongozi huyo wakati wa mahojiano hayo.

View attachment 3649900
Naona Serikali iliamua kuficha kile hasa kilichozungumzwa
 
Neno samahani litasaidia nini? Je, uhai wa watu waliopotea nani ataulipia.

Uwajibikaji pekee ndio kitu kinatakiwa.
Kukiri makosa na kuomba msamaha "publicly" au kusema "Sorry" (publicly) kwa yalotokea ni jambo la uungwana na huonyesha umestaarabika.

Raisi Samia kwa niaba ya serikali apaswa kuomba radhi kwa watanzania kukiri kwamba makosa yalotokea, kuwajibishwa kwa wote walotenda maovu yale ya October 2025 na mwisho kulipa fidia kwa familia ziloathirika na majanga yake na wahanga wote wa matukio yale.

Akifanya hivyo, atatoboa kwa kiasi kikubwa.

Pia akifanya hivyo ataponya vidonda na majeraha yote na hata kama kidonda kilitaka kuwa kidonda ndugu basi dawa itaingia na kitapona.
 
Wakuu,

Padri Kitima leo kwenye mahojiano maalum amesema japo Rais alikiri kutokea kwa changamoto na kusema matukio hayo hayakuwa ya kawaida na hayatapaswa kujirudia, bado hajatamka neno "samahani" kwa niaba ya watendaji wa serikali yake.

"Ni kweli Mheshimiwa Rais alisema yaliyotokea hayakupaswa kutokea na hayatatokea tena. Lakini bado hatujamsikia akisema 'samahani' kwa niaba ya watendaji wake waliokusababishia wananchi maumivu hayo," alisema kiongozi huyo wakati wa mahojiano hayo.

Rais kusema samahani" kwa niaba ya watendaji wa serikali yake ni sawa na kukiri moja kwa moja kwamba watendaji wake ndiwo walioua watu kitu ambacho tangu mwanzo amekuwa akikikanusha kwa namna anayojua yeye na wanaomshauri.
 
Haya mambo yalianza mbali sana na TEC hawakujiongeza!

Mauaji ya Zanzibar 2001 kipindi cha mkapa,mkapa aliomba radhi!!?haki ilitendeka!!?mlidai katiba na tume huru ya uchaguzi!!?wazanzibari sio watu!!?

TEC hawakudai katiba Wala tume huru ya uchaguzi kipindi kile cha mkapa!!

Damu Ile Ile imemwagika huku ndio TEC wanajitokeza na kukomaa!

Sasa najiuliza mlikua wapi!!?au wazanzibari hawakua watu ni wanyama!!?

Au kwasababu mkapa alikua Tanganyika mwenzetu!!?

TRUST ME NAWAAMBIENI UKWELI AMBAO WENGI HAMUUJUI

MAUAJI YA OCTOBER WAZANZIBARI WALIKUA WANALIPA KISASI NA WAMEFURAHI SANA COZ WAMEPIGWA NA KUUMIZWA KWA MIAKA MINGI SASA ILIKUA ZAMU YETU!!!

HUO NDIO UKWELI ULIOJIFICHA KABISA NA MAMA AMEWAKOSHA KWA KUTUMIA KATIBA ILE ILE NDIO MAANA ANATOA MANENO YA SHOMBO "HAKUNA CHA NYWII NYWII"

HULKA ZA WANAWAKE WENGI NI KULIPA KISASI

Hata thabit kombo juzi alilopoka bungeni kwamba askari walifuata amri halisi ndani ya utaratibu wa kawaida ya ku shoot!

Wazanzibari wametumia ubovu wa katiba kulipa kisasi!!
 
Tuna kiongozi mnafiki anayetaka maridhiano kwasababu za kisiasa na kujirudisha kwa international community, sio kiongozi anayejutia kwa dhati kwa yale yaliyotokea.

Kichwa kinachowaza mikopo na misaada kila siku hakiwezi kutukumbuka wala kukumbuka madhila ya makusudi kilichotufanyia, ndio maana hata juzi akiwa Zanzibar akaendelea kutusimanga kwa aliyotufanyia.
 
Haya mambo yalianza mbali sana na TEC hawakujiongeza!

Mauaji ya Zanzibar 2001 kipindi cha mkapa,mkapa aliomba radhi!!?haki ilitendeka!!?mlidai katiba na tume huru ya uchaguzi!!?wazanzibari sio watu!!?

TEC hawakudai katiba Wala tume huru ya uchaguzi kipindi kile cha mkapa!!

Damu Ile Ile imemwagika huku ndio TEC wanajitokeza na kukomaa!

Sasa najiuliza mlikua wapi!!?au wazanzibari hawakua watu ni wanyama!!?

Au kwasababu mkapa alikua Tanganyika mwenzetu!!?

TRUST ME NAWAAMBIENI UKWELI AMBAO WENGI HAMUUJUI

MAUAJI YA OCTOBER WAZANZIBARI WALIKUA WANALIPA KISASI NA WAMEFURAHI SANA COZ WAMEPIGWA NA KUUMIZWA KWA MIAKA MINGI SASA ILIKUA ZAMU YETU!!!

HUO NDIO UKWELI ULIOJIFICHA KABISA NA MAMA AMEWAKOSHA KWA KUTUMIA KATIBA ILE ILE NDIO MAANA ANATOA MANENO YA SHOMBO "HAKUNA CHA NYWII NYWII"

HULKA ZA WANAWAKE WENGI NI KULIPA KISASI

Hata thabit kombo juzi alilopoka bungeni kwamba askari walifuata amri halisi ndani ya utaratibu wa kawaida ya ku shoot!

Wazanzibari wametumia ubovu wa katiba kulipa kisasi!!
Acha wazanzibar wapambane na zanzibar yao na tanganyika wapambane na tanganyika yao after all sio competition nan alipigwq sana na nan kalia sana
 
"Kusameheana"
Kama neno lilivyo lipo katika tendo- uwili, namaanisha linahusisha pande mbili kutendeana. Tunategeme pia kulisikia Kanisa likitamka neno "samahani" Ili kukamilisha uwili kamilishani wa tendo.

Narejea " Baba uwasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo" hapa aliyeomba msamaha alijenga msingi imara sana na kuonesha kuwa hata katika haki kuna msamaha.
 
Back
Top Bottom