TANZIA Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la Dar, Afariki Dunia

Hawa watumishi wa Mungu wamekuwa wazito kutoa waraka ngoja iwatandike akili ziwakae sawa.

Ingekuwa vyema watoe tahadhari kwa waumini ikiwezekana wasisitishe misa zote hadi pale hali itakapotengemaa.
Na mwaka sijakanyaga Kanisani.....Tulijuwa hili VANGAVANGA likianza kujitikisa....sayansi haina UNAFIKI
 
Natamani sana wale wajumbe wa kishindo walipe madhambi yao.
 
Apumzike kwa amani rumi imepoteza makasisi wawili leo hili pengo kuliziba dah.
 
Hawa watumishi wa Mungu wamekuwa wazito kutoa waraka ngoja iwatandike akili ziwakae sawa.

Ingekuwa vyema watoe tahadhari kwa waumini ikiwezekana wasisitishe misa zote hadi pale hali itakapotengemaa.
Waraka wa TEC uliotolewa na Mwenyekiti Mhashamu Baba Askofu Nyaisonga haukuuona mkuu? Kanisa kwa upande wake limeeleza kweli tupu na tahadhari zinafuatwa kwa wale wanaoshiriki misa takatifu.
 
Ha ha ha ha!
Unatisha
 
TANZIA
Wapendwa Mapadri, Mashemasi, Watawa na taifa lote la Mungu, Kristo.

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu juu ya kifo cha Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la DSM, aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Chang'ombe. Padri Boyo amefariki leo tarehe 10 Februari 2021 saa 1:30 usiku katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa akitibiwa. Taarifa zaidi juu ya taratibu za Mazishi zinapangwa na tutawataarifu. Tumuombee Pumziko la Milele Mbinguni. ASANTENI.

+ Jude THADDAEUS Ruwa'ichi
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DSM
APUMZIKE KWA AMANI,AMINA
 
Neno la bwana lihimidiwr
 
Mimi sitashabikia tena mihemko ya Tanzia. Watawala wasiogope aibu wakubali wameshakosea wasaidie Wananch vifo ni vingi tena vinahepukika tu.

Mungu atujalie uzima, maisha marefu na afya tulio hai. Awarehemu waliotangulia mbele za haki. Na awafariji na kuwapa nguvu waliofiwa ambao wanapitia wakati mgumu wa majonzi kwa kupoteza wapendwa wao.

Tuzidi kuombeana.
 
Ila mapadre wanapukutika Sana Aisee.

R.i.p
 
Covid is real killing us very awkwardly, let's us take preventive measures my dear friends!
 
Ee Mwenyenzi Mungu ipomzishe Roho ya Padri mahali Pema Peponi.
Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…