Pafyumu gani ni nzuri kwa wanawake na wanaume?

Pafyumu gani ni nzuri kwa wanawake na wanaume?

Usipate shida best, nilihangaika sana ila nikapata solution. tafuta FOR MEN, 3,000/= tu! tena mbili ni 5,000/=
 
Kiufupi perfume kwanza sio swala la bei tu ingawa budget yako kwa kununua inahusika kwanza. Muhimu ufahamu wataka perfume ya kuvaa muda gani usiku/mchana mana ake kazi au casual outings, pia taste yako wapenda harufu gani michanganyiko ipi. Lakini kama huna uzoefu huo au ni zawadi andaa kwanzia 100,000 minimum nenda madukani wambie wakishauri utapata. Personal recommendations Men try Kenneth Cole Reaction, Cartier, Aqua Di Gio Men, Hugo Boss Sports or Bvlgari Aqua Marine zote za Mchana
hizo, Kenneth Cole Black/ Vintage, Gucci Guilty sio mbaya. Za kike jaribu Dior, Jean-Paul Gautier au Auqa Di Gio na Versace.
 
daa ugonjwa wangu huu.inategemea unapenda harufu ya namna gani.wengine wanapenda perfume kali,wengine wanapenda iliyopoa.mimi kwa upande wangu napenda iliyopoa,ukimpitia mtu lazima atageuka{natania}nina amini harufu iliyopoa haimkeri mtu yoyoyte unaekaa nae karibu.list ya baadhi ya perfume nilizotumia ni chloe original{nzuri sana}opium{imetulia sana kwa kweli na harufu yake inakaa muda mrefu}burberry{imeshatoka na nyengine}channel{hii kwa upande wangu niliiona kidogo ipo strong}1 million{hii ki ukweli nilitumia ya kiume,niliipenda harufu ya kiume kuliko ya kike}Givenchy{hii niliitumia muda}gaultier by jean paul{this is one of the best} kuna nyengine flower bomb{nzuri sana} na nyengine miss dior{zipo kama 3,ila chaguo langu ni ya rangi ya peach]kwa kuchagua top 3 ni gaulter,opium, na burberry
 
me kuna moja hivi nina wiki naitumia inaitwa OBAMA

wameshaichakachua jiou, nilituma mtu kaniletea mimaji ntu, lakn mm niliipenda kwa kuisikia kwa mtu ambaye alinunua mwanzoni kabisa
 
halafu lazima tujue kuna tofauti kati ya Perfume na Cologne, Perfume ni zile za kike ilihali Cologne ndio za kiume, so wote mnaoita perfume hata za kiume mnaingia chaka (talk of common mistakes)

kiasili zinaitwa hivyo sbb wanaume wanategemewa kutumia harufu strong kutokana na nature ya shughuli zao na cologne simply are strong odor

Cologne is for men.Perfume is for women.-http://answers.yahoo.com/question/index?qid=

Cologne is for men and usually has a stronger smell. Perfume is for women and usually has a lighter smell

wadau naomba tujuzane pafyumu nzuri za wanawake na wanaume ukiweka na bei itakuwa poa sana.
Mimi ni mmasai. Kikwetu perfume nzuri ni samuli iliyochanganywa na kinyesi na mkojo wa ng'ombe kigogo, kisha vundika kwa miezi miwili. Ukijipulizia hiyo hata simba, chui, nyati waweza kupiga kiss.
 
Perfume ya nini wakati kuna Marashi ya kwenye vichupa kama za kuwekea mikojo.
 
kwa mwanamme inategemea mtu anapenda mpenzi wake atumie ipi lakini kwangu mimi napenda wangu atumie Polo Red,
Mont blanc black, Creed au ralph lauren No1..
na kwa wanawake M.mikalif, Allure sensuelle na Coco zote za chanel, Amor Amor Cacharel ya Red, CH red by CH
na kama ya Udi ziko mpya za Christian Dior Ambre Nuit,Oud Ispahan hizo ndio choice yangu..
 
Jipatie perfume inaitwa run,ina harufu descent,made in Tanzania price elfu kumi tuu
 
mimi najua kuanzia 100,000 hadi 1,000,000 za 10,000 sizijui....ninazopenda ni hizo HUGO BOSS,TOMMY HILFIGER,YSL KOUROS,GUCCI ONE,ISSEY MIYAKE,212 MEN,CK[EUPHORIA,OBSESSION,ONE] hizi ndio ninazozipenda bei 100,000-200,000

212 Men nzuri Tsh 5,000/=

Aiseee.....!!! Uzuri wa JF huwezi kudanganya hapa usishtukiwe.....!!!!!:confused2::confused2::nono::nono:
 
daa ugonjwa wangu huu.inategemea unapenda harufu ya namna gani.wengine wanapenda perfume kali,wengine wanapenda iliyopoa.mimi kwa upande wangu napenda iliyopoa,ukimpitia mtu lazima atageuka{natania}nina amini harufu iliyopoa haimkeri mtu yoyoyte unaekaa nae karibu.list ya baadhi ya perfume nilizotumia ni chloe original{nzuri sana}opium{imetulia sana kwa kweli na harufu yake inakaa muda mrefu}burberry{imeshatoka na nyengine}channel{hii kwa upande wangu niliiona kidogo ipo strong}1 million{hii ki ukweli nilitumia ya kiume,niliipenda harufu ya kiume kuliko ya kike}Givenchy{hii niliitumia muda}gaultier by jean paul{this is one of the best} kuna nyengine flower bomb{nzuri sana} na nyengine miss dior{zipo kama 3,ila chaguo langu ni ya rangi ya peach]kwa kuchagua top 3 ni gaulter,opium, na burberry

Safi sana dada, ndiyo vitu tulivyotegemea kuvikuta humu!! Siyo watu wamejaza mizaha kupitiliza mpaka maana nzima ya uzi wenyewe imepotea kabisa!! Wengine wake zetu ni watumiaji wakubwa wa hivi vitu na ukisafiri ukamletea zawadi ya unyunyu unaona kabisa anavyo appreciate kwa furaha ingawa ugumu ni kwa sisi wanaume kuujua unyunyu mzuri wa kike!! Ni shughuli, asante na nimeichukua hii na inafanyiwa kazi soon.
 
Aiseee.....!!! Uzuri wa JF huwezi kudanganya hapa usishtukiwe.....!!!!!:confused2::confused2::nono::nono:

Hakuna aliyedanganya hapo! Bei ya original perfume iko juu sana kama alivyo eleza jamaa juu.
Huyo mwenye the same perfume kwa bei ya andazi naye hajadanganya ila ya kwake ni immitation tu!
Zipo aina hiyo hiyo (212) products za San Siro zinauzwa buku! Zipo kwenye vichupa vidogo vinafanana na pen!
 
Back
Top Bottom