Swali nje ya topic
Mshana Jr. ... unawezaje kujua kama umefanyiwa chuma ulete kwenye chakula au hela?
Unajinasuaje kwenye chuma ulete?
Back to the topic: hii jicho la tatu linahusiana na maono? Hisia kuwa huyu mtu si mzuri au huyu mtu ni mwema? Au zinahusiana na utambuzi wa mambo?
Kuna kipindi huwa inanitokea niko ndotoni napambana na nguvu ambayo nimeitambua kuwa ni nguvu mbaya au za giza. Jinsi ninvyopambana ile nguvu ya upande wa pili inakuwa inanizidi nguvu kwa kupigana inakuwa ni vuta nikuvute kama mieleka au kukabana.
Mara inanijia sauti anza kusali anza kusali na ukemee usipigane hizo nguvu zitakimbia.....
Naanza kusali na kusali nakemea na kukemea zile nguvu zinakuwa kama zinaishiwa nguvu na zinaanza kujiondoa kwangu na kuweka gap kati yetu. Ila mara zinarudi na kunionesha kuwa haziogopi maombi na kama inakuwa inanishiria niachane na hayo maombi maana hayatasaidia mimi kutoka kwenye zile nguvu za giza.
Ila sauti nyingine hainiombei bali inaniambia sali kwanguvu usimsikilize wala usimuangalie wee sali tuu. Nikiendelea kusali woga unaniisha na najiwa na nguvu zaidi na naendelea kusali.
Sasa ishanitokea mara kwa mara nakuwa nasali kwenye ndoto hadi nastuka nakuwa macho na najikuta niko katikati ya sala na nakuwa sina mamlaka au utashi wa kunyamaza. Naendelea kusali hadi ile nguvu iniishe kisha aidha usingizi utakata kabisa au utanipitia baadae.
Waweza nisaidia hapo kuna lolote ambalo nafunuliwa ila sijalitambua. ..... jicho la rohoni linahusika hapo?