Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Paji la uso na siri ya jicho la tatu

Nazungumzia hizo mkuu
Ni ngumu sana kumwambia mtu nini maana ya wokovu na faida zake kama hajaokoka
Dunia inazunguka na maisha yanakuwa live kwasababu ya nafsi hai....ni kupitia hiyo nafsi hai ndio mambo yote huanzia hapo na ufunguo wake ni hiki tunachokiita jicho la tatu....huyu ndie mtawala wa dunia
 
Nakushukuru sana Mshana jf! pia nimushukuru ndugu Raphew peter kwa mchango mzuri! nimesoma uzi wote na michango yote! nimejifunza kitu! sasa zamani nilikuwa nikiota ndo %78 ilikuwa kweli! hivi karibuni tuliachana na mchumba wangu. tena ameniacha kwa dharau sana! niliumia nikaona niingie kwenye maombi! nilingia na neno toka Yer 31:13 b. baada ya kumaliza kuomba nilijilaza chali kitandani. nilifumba macho, na usingizi ulikuwa unanichukua kwa mbali! ilikuwa mchana. nikaona 11:11 nikajiuliza nn hii? basi kwakuwa nilikuwa nasoma biblia niliamua kufungua Yer 11:11. usiku nikaota kuwa kwa mchumba wangu kuna mtu amevunjika miguu, halafu alinilaumu mimi kuwa nimesababisha! sasa ajabu jana nilimwita huyo binti kumwambia kuwa sio vizuri kununiana! kuachana sio uadui! wakati tunaongea akasema nawahi nyumbani mama amepata ajali amevunjika mguu. nikashangaa sana! sasa hli ndilo jicho la tatu? nifanyeje iliniweze kulitumia vizuri?
 
f6e63668ac1c4a88887ca94b0bd11c01.jpg

Hutaamini utakachogundua hapa kuhusu paji lako la uso...hapa ndio asili ya neno kipaji ilipatikana..hapa napo ni lango hapa ndio penye njia ya kuingilia mlango wa sita baada ya ile mitano. Hili ni jicho la ndani jicho lisioonekana.lango kuu la kiroho.

Anzisha shule au chuo unaweza kukipa jina lolote, nakuhakikishia nacte wanaweza kukosa wanafunzi wakupeleka vyuo vingine na bodi ya mikopo watataharuki

Tutaenda kwa mitazamo yote ya kidini na kiimani, kisayansi, kihisia na hata kwenye nguvu za giza.

1. Third Eye - Thalamus - Eye of Horus
c028b8f6365bdd2fb44aaf6796fdf17f.jpg

Hapa ni kwa mtazamo wa kisayansi nafikiri ni kwenye somo la anatomy kuhusu ubongo, jicho la tatu linaonekana katikati ya ubongo (zingatia katikati) vertebrate brain hapo ndio zinapozalishwa homoni za kulaza au kuamsha hisia maono usingizi nk.

2. Mathematics
22f4856d4325c03356542c3c19a96824.jpg

Katika ulimwengu wa mahesabu na hesabu, wanamahesabu kwenye ishu za ratio cos na tan watatusaidia hapa.

3. Tahjud (Meditation)
1a3f1076a0eecca2d21fb8771039a216.gif

Kwenye tahajudi wale waliosoma chakra na habari za milango nane, ukiangalia vizuri huo mchoro chakra ya sita ndio ya kuingilia mlango wa sita wa fahamu.

4. Baptism & Sijda
b23bbe047b4fed53bc8acd968bfbde9f.jpg
7581aaa5dd84dc3d74104360bf95c259.jpg

Kiimani katika ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndio hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili sasa.. Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi..

Kwenye Uislam tunajua nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wako katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.

5. A kiss on the Forehead
95e4888b95b1f04ef937618e752fd13d.jpg

Kwenye mahusiano busu kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.

6. FREEMASONRY
2eaa591e515e975051f9640238953750.jpg

Kwenye imani za mpinga Kristo freemason satanism nk alama yao kubwa ni jicho la tatu

7. SEVERE PUNISHMENTS (WATERBOARD)
8654ca9f3d106b3012aa7228ab664632.jpg

Kwenye adhabu na mateso mbalimbali paji la uso hutumika kuleta adha ya ajabu mwilini... Mateso ya water board ni mfano mmojawapo. Unalazwa chini unafunikwa kitambaa usoni kisha unamwagiwa maji.. Ni aina ya adhabu isiyoumiza mwili bali inayoumiza hisia.

8. Michezoni:
Kwenye mchezo wa ngumi alama za juu ni zile ambazo zinaangukia kwenye paji la uso.

Nimejaribu kwenda na picha kuokoa ufafanuzi wa maneno mengi... Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu mno.. Tunashiriki kitu hicho hicho lakini kwa maana matumizi na mitizamo tofauti. Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.

Manabii na watenda miujiza hupenda kuwapuliza ama kuwashika watu penye paji la uso na kifuatacho hapo ni mzinga kama si kupiga kelele... Baadhi ya tiba mbadala hutumia paji la uso kama lango la uponyaji.

Wahindi na wahindu kwenye imani zao hujipaka rangi katikati ya macho kama sehemu ya ibada nk.

Jaribu kutafakari kwa hatua hiki kinachoitwa jicho la tatu, paji la uso, imani yako na maisha yako ya kila siku... Mwishowe tunaweza kujikuta tunaabudu paji la uso kwa muktadha tusiojua.
 
Nakushukuru sana Mshana jf! pia nimushukuru ndugu Raphew peter kwa mchango mzuri! nimesoma uzi wote na michango yote! nimejifunza kitu! sasa zamani nilikuwa nikiota ndo %78 ilikuwa kweli! hivi karibuni tuliachana na mchumba wangu. tena ameniacha kwa dharau sana! niliumia nikaona niingie kwenye maombi! nilingia na neno toka Yer 31:13 b. baada ya kumaliza kuomba nilijilaza chali kitandani. nilifumba macho, na usingizi ulikuwa unanichukua kwa mbali! ilikuwa mchana. nikaona 11:11 nikajiuliza nn hii? basi kwakuwa nilikuwa nasoma biblia niliamua kufungua Yer 11:11. usiku nikaota kuwa kwa mchumba wangu kuna mtu amevunjika miguu, halafu alinilaumu mimi kuwa nimesababisha! sasa ajabu jana nilimwita huyo binti kumwambia kuwa sio vizuri kununiana! kuachana sio uadui! wakati tunaongea akasema nawahi nyumbani mama amepata ajali amevunjika mguu. nikashangaa sana! sasa hli ndilo jicho la tatu? nifanyeje iliniweze kulitumia vizuri?
Duu kwanza pole sana
Kuna link kaweka Raphew peter ipitie imeshiba hayo maarifa na inajibu maswali mengi kwa undani
 
Naamini tuna wanafunzi wengi wa Buddhism humu ndani hasa kwenye kipengele cha spiritual awakening.

dc556203657c470dbe63ccbc7d5602a4.jpg

Unaposoma hiyo topic na ukaja kulinganisha na huu mchoro unapata mtiririko wenye kuleta uhalisia wa ajabu kabisa.

c19a91f68d318dd66366655ef11060a7.jpg

Lakini pia kuna baadhi ya mimea hutumika kiimani kama stimuli/stimulas ya jicho la kiroho... Ni kama shortcut ya meditation au ya kuingia mlango wa sita kupitia moshi.

f0ae1602a46f2fb9ece65cbd9be7812f.jpg

Ndio maana mijadala haiishi kuhusiana na mmea... Shida moja ya mmea ni kwamba huamsha pande mojawapo kati ya zile mbili za mawasiliano ya kiroho ndani ya nafsi upande wa hasi na upande wa chanya... Inategemea kichocheo kipi kitawahi.

Kuna hii kitu mtu akifanya mambo yasiyoeleweka anaambiwa ni madhara ya bhangi za kuvutia chooni, ni kama mzaha vile lakini chooni panajulika kama mlango wa kuzimu na makazi ya roho wachafu...

Sasa bhangi inaamsha mlango wa sita kupitia jicho la tatu halafu unalivutia chooni, hapa unachanganya hasi na chanya. Matokeo yake lazima kichwa kipate moto.
I love this point of your argument
 
Ni ngumu sana kumwambia mtu nini maana ya wokovu na faida zake kama hajaokoka
Dunia inazunguka na maisha yanakuwa live kwasababu ya nafsi hai....ni kupitia hiyo nafsi hai ndio mambo yote huanzia hapo na ufunguo wake ni hiki tunachokiita jicho la tatu....huyu ndie mtawala wa dunia
Me sielewi hapa! Mtawala wa Dunia unamaanisha Lucufer? Huyu si ndio Ametabiriwa atakuja kutawala Dunia! Na si ndio anajicho moja ambalo liko kwenye paji LA uso! Na sasa nyinyi si ndio mnamuandalia mazingira ili akija watu wasitaharuki!
 
Hatumuandalii ameshatake cover, jiulize barcode ni kitu gani. . . na kwanini siku hizi mambo mengi ni password...! Jiulize kuhusu biometric nk
 
Back
Top Bottom