Paka kuchukuliwa kama mwanafamilia kwa kutengewa bajeti yake, inakubalika?

Mtafuga na majini bure
Mimi kwangu sifugi mnyama tofauti na mbuzi,ng'ombe na kuku.
 
Chuna ngozi huyo paka kawauzie Wachina, kama nyumba haina panya hakuna sababu ya kukaa na paka.....hana faida hata kidogo.
 
Safi kabisa, baba anafikiri anachokipenda yeye na familia itakipenda, kutunza familia siyo chakula na mavazi tu. Hata kuheshimu na kujali hobbies za wanafamilia ni sehemu ya majukumu ya baba, utakuta wengine wanachinja wanyama nyumbani huku watoto wanaona na wanaanza kulia sana, sababu wanawapenda wanyama. Watanzania wengi hawana elimu kuhusu tabia za viumbe na ndiyo maana bundi na paka wanahusishwa na Imani potofu za kishirikina.
 
Nimesoma Uzi nzima watu wamekalili kuwa kazi ya paka ni kuua panya tu,ok fine,sipendi paka lakini paka ni kiumbe mzuri Sana ,mwaka elfu 2000 nilikuwa kwa Bibi yangu tumelala chini ,na Bibi alipenda Sana kufuga paka,Ile naamuka asubuhi pale chini usawa wa godoro nilishangaa kuona nyoka amekufa,isingekuwa paka nyoka yule angetuuma.


Tena nakumbuka mwaka 2018 nikiwa Lindi ,ghafula paka wa jirani yangu alianza kutoa sauti ya kuashiria hatari,nilipo toka nje sikuamini macho yangu,nilimkuta paka anapambana na nyoka mkubwa Sana aliyekuwa akihangaika kuingia ndani ya nyumba,paka alikuwa akimzui,nilipambana naye na kumuua yule nyoka.

Paka Ni wazuri Sana,tuache kukalili kuwa kazi yao Ni kupambana na panya tu!
 
Ongea na wife na watoto mpate suluhisho. Mwambie ukweli wako unavyofikiri.
 
Zamani nilikuwa nafunga mbwa kwa ajili ya kuwinda na ulinzi ,paka naye alikwepo ila anajitafutia chakula kivyake maana siyo panya tu anakamata njiwa ,hadi kware .Ila jioni na asubuhi mnapokamua ng'ombe anakuja pale kulia anataka maziwa tunampa hata nusu lita anajipigia zake anaondoka but maisha ya Sasa yamebadilika ,paka na mbwa wamekuwa kama mapambo tu,unakuta paka hali nyama mbichi anataka vilivyokaangwa
 
Hakika mkuu kwa waswahili paka mweusi na bundi anaonekana ni msala lkn kiuhalisia hawa viumbe ni wazuri kudhibiti wadudu hatari ndani ya nyumba tunahitaji elimu kuhusu hawa wanyama
 
Hausumbuliwi na panya kwa sababu paka yupo,waenga sio wajinga walisema "paka akitoka(kuondolewa au kufa)panya utawala "
 
Mnyama yeyote afugwae ni mmoja ya familia, kinachofanyika hapo kwako ni jambo jema sana na lakiimani sana kuhudumia mfugo ni wajibu na ni sehemu ya jukumu letu wanadamu, nikuombe tu usivunjike moyo wasapoti wanafamilia kwa hilo la kupenda wanyama na uwekeze ktk kuwajali na kuwatizama vyema.
WATAZAMENI NDEGE WA PORINI HAWAVUNI WALA HAWASOKOTI LAKINI BABA WA MBINGUNI ANAWAPA KULA KULALA KUNYWA NA UHAI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…