Paka kuchukuliwa kama mwanafamilia kwa kutengewa bajeti yake, inakubalika?

Paka yule ana confidence balaa yani unamtofautisha na paka wetu. Jamaa kamtishia kamfukuza ila wapi, mi nimeitwa nikarekebishe kitu narudi nakuta jamaa analazimisha paka atoke. Ni wale watu hawana exposure unamuita aje kukusaidia kazi za kutumwa. Haelewi thamani ya paka kwa boss, walipokuja wenyewe wakaongea Kihindi akawafuata
 
Sawa kabisa kukosa exposure halafu ujuaji mwingi , Mwingine humu anasema ana master degree halafu anachangaika hoja mbaya kuhusu paka, kumbe Hana exposure na hajui lolote
 
Paka mnyama mzuri sana
 
Kiukeli hawa paka kazi pekee wanayojua ni kupumzika na kujizungusha chini ya miguu, Mbaya zaidi wanahisi wanakutawala ukiwaendekeza kuwapa wanachohitaji

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna kipindi niliona rais wa Ireland anahojiwa nje ya nyumba yake uwanjani anakocheza na mbwa. Rais yuko anahutubia mbwa yuko anamvuta anamuonesha mpira ili wacheze, rais hakumfukuza wala kukerwa na raia walipenda.

Raia wanajua yule mbwa wa rais wao ana wivu hata wakija wageni wa kimataifa hapendi wapewe attention zaidi yake. Anataka yeye ndio awe karibu na rais. Wazungu wanaamini ukipendwa na wanyama unakuwa na roho nzuri. Huwezi kuwa unapiga mawe mbwa ukawa na utu. Humanity inaakisiwa kwa unavyowatreat wanyama
 
Kweli kabisa, tabia ya kuonea viumbe wadogo ni matokeo ya kuongezeka ukatili duniani
 
Paka wetu hua anakula pale tunapokula hana bajeti maalum, mda mwingine namnyima chakula akamate panya maana wanasumbua sana, nyumba bado kupiga gypsum,
Kibaya zaidi kajifungua watoto mapacha watatu nimevumilia sana juzi nikaenda kuwatupa mbali nimebaki na mama yao tuu, usawa mgumu huu hakuna bajeti yao
 
Imeniuma kutupa watoto wake
 
Dah usingewatupa jamani
 
Inasikitisha na kuhuzunisha,umefanya kitendo kibaya sana kuwatenganisha watoto wa Paka na Mama yao tena wakiwa wadogo na wanahitaji kunyonya na kua chini ya uangalizi wa Mama yao,ni bora ungesubiri wakakua kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…