HOJA Pale Kariakoo tuvunje shule ya Benjamin Mkapa na Uhuru mchanganyiko ili tupate eneo la Parking

HOJA Pale Kariakoo tuvunje shule ya Benjamin Mkapa na Uhuru mchanganyiko ili tupate eneo la Parking

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Nadhani mipango miji haikuzingatiwa huwezi weka jengo lenye ghorofa kadhaa tena kwa ajili ya biashara ikimaanisha mikusanyiko ya watu bila kuangalia miundombinu ya parking lilikuwa ni kosa. Hata ukivunja shule zote bila kuweka mpango bora wa parking kwa mwendelezo wa kuvunja majengo ya chini na kugeuza viwanja kuwa maghorofa bado ni kutwanga maji kwa kinu.

Tujikite kwanza kwenye kufuata taratibu za utoaji vibali bila kutanguliza matumbo yetu mbele kwa usitawi wa ukuaji wa miji yetu
 
Maendeleo ni bora kuliko kuwa na magofu yasiyokuwa na faida . Ile mijengo haina cha maana chochote kuna watalii wanaoenda pale ?

kwa hiyo dunia nzima wanaotunza majengo ya kale ni wajinga na wewe tu ndio muelewa pekee yako, taasisi yote ya un unesco inayoheshimika duniani wote ni wajinga kwa sababu tu wewe unataka kupaki gari lako? btw hebu jaribu kwenda zanzibar ukawaambie wabomoe mji mkongwe (stone town) na kujenga "maghorofa kisasa na parking" ...
 
Tunasubiri Wazungu waje watupe mawazo, waafrika sisi ni bure kabisa.Hivi ina maana wanaohusika hawaoni jinsi kwenda kariakoo kunavyokatisha tamaa...??Kama tunashindwa kuiweka sawa kariakoo, tutaweza kutuma sattelite kweli??
 
Nadhani mipango miji haikuzingatiwa huwezi weka jengo lenye ghorofa kadhaa tena kwa ajili ya biashara ikimaanisha mikusanyiko ya watu bila kuangalia miundombinu ya parking lilikuwa ni kosa. Hata ukivunja shule zote bila kuweka mpango bora wa parking kwa mwendelezo wa kuvunja majengo ya chini na kugeuza viwanja kuwa maghorofa bado ni kutwanga maji kwa kinu.

Tujikite kwanza kwenye kufuata taratibu za utoaji vibali bila kutanguliza matumbo yetu mbele kwa usitawi wa ukuaji wa miji yetu
Kariakoo haikuwa hivyo. Kariakoo ilikuwa eneo la makazi ya kawaida mengi na maduka machache mitaa kama Msimbazi na Tandamti. Hio Kariakoo unayoiona leo ni imejaa mafremu ni ujenzi holela tu kama maeneo mengi ya Dar.
 
Kwa miaka ile jiji lilikuwa bado halija changanya ila kwa sasa population imekuwa kubwa sana kiasi kwamba majengo kama ya shule hayana maana kuwa katikati ya jiji
hivi ile al halamain secondary bado iko ? wazo lako hata mimi nalikaubali wajenge parking ya kulipia ,jiji waone hilo
 
Watu hawaoni madhara ya hizo shule KUWEPO pale amini nakwambia hata hizo foleni tunazo lalamika kila siku, chanzo chake ni kuto kuwa na parking kubwa na ya kisasa yenye walau floor tatu au nne kwisha kabisa tatizo la foleni
 
Tunakoelekea ni kubaya zaidi nafikiri mipango miji imezidiwa na maamuzi ya kisiasa na ubepari usiojali kanuni na misingi husika ya kibiashara leo tunaongelea kuvunja mali na maeneo ya umma kwa usitawi binafsi inanikumbusha ule mradi wa bandari kavu kupelekwa nje ya mji lakini leo mji haufai kwa foleni za malori kisa bandari kavu za watu binafsi na wakiendelea kununua makazi ya watu na kuyageuza bandari kavu. Kikubwa michezo ya kuigiza kama si kujitekenya kisa kucheka kama zuzu, haiwezekani mpango ulikuwa kontena zitolewe pale bandalini kwa treni mpaka nje ya mji hivyo malori yote kuishia kule leo barabara zimefungwa hadi mtu anaiona nyumba yake mtaa wa pili mita zisizozidi 10 ila kupafikia mzunguko wake anatumia dakika kumi mpaka thelathini kupafikia kisa foleni ya kupakia makontena kweli sie bado sana
 
Naunga mkono bandari kavu iheshimiwe kwa eneo lake nje ya mji,na zilizopo mijini ziondoshwe!
 
Nitajie gorofa gani k/koo lina underground parking? Kwanini tusiwalaumu waliojenga magorofa bila kuweka underground parking. Kila gorofa k/koo, Basement wameweka ma frame. Ilitakiwa itungwe sheria Nchini kote kila gorofa likijengwa kuwe na underground parking.
 
Back
Top Bottom