Pamoja na kushusha bei wananipita wanaenda kwingine, najiuliza nakosea wapi?

Nipo rangi 3 nauza viatu unakuta kwa siku nauza 3 au 2 dah halafu bado kodi nawaza
Pole sana mkuu jaribu kutengeneza mob

Yaani uwe kama kichaa piga makofi na nyimbo ita wateja ikiwezekana weka na spika ya matangazo

Usisubiri waje kwa hiari yao wakati mwingine mteja anaenda sehemu walipojazana watu akiamini ndio kuna huduma nzuri kuliko pale ambapo hamna hata mtu japo bidhaa ni ile ile

Lenga kujaza wateja hata kama hawanunui wanunuzi watakuja
 
Kuna mwamba kitaani akifungua kibanda cha chips. Jamaa mwanzoni alikua akiuza kile kindoo cha rangi cha litre 4 tu.

Jamaa hakugiveup, alikaza zaidi ya miezi kadhaa sahivi anajitajidi kwa siku mbili au tatu anamaliza gunia.

So me naamini biashara ni kutetegemea mabadiriko au faida ndani ya usiku mmoja, maintain quality tu.
 
Wapo mkuu wenye maspika inakuwa kelele yaani unakuta mtu anajaribisha tu anasema ahsante anakula kona
 
Powa bro wacha nikaze
 
Wapo mkuu wenye maspika inakuwa kelele yaani unakuta mtu anajaribisha tu anasema ahsante anakula kona
Usikate tamaa kuna siku watanunua

Lakini pia matangazo sio kelele, ni kelele kwa yule ambae halimuhusu ila kwa linaemhusu sio kelele

Mimi kwenye ofisi yangu naweka tangazo muda wote kuna wanaosema nawapigia kelele ila nikilitoa wateja wanauliza tangazo likowapi kidogo nisije nikajua haupo

Kwa hiyo tumia kila mbinu mkuu asaivi ushindani sokoni ni mkubwa sana
 
Hakika mkuu sema baadhi ya viatu vinakaa mpka matoleo yanapitia hasara sana nafikiria nihamie eneo
 
Watu wa uswahilini purchasing power yao IPO chini Sana .


Mimi niliwahi kuuza nguo za mtumba grade one nilikuwa nanunua karume nakuja kuuza uswahilini nilikuwa sipati returning yoyote


Lakini nilianza kwenda sinza aisee nilikuwa napata pesa nzuri kabisa.


So Biashara inahitaji uangalie purchasing power

MTU wa uswahilini ukiuza dagaa Michele unauza unamaliza Ila nyama Kama nyama sio Sana .

Pia chumvi ya mawe inasaidia kiasi fulani kurahisisha mambo yaende vzr.

Lugha nzuri


Ila kikubwa angalia purchasing power ipoje katika eneo ulilopo kwanza.

Usiwe unawauzia kuku watu wenye uwezo wa kula mchicha .
 
Kweli I see mfano huku rangi 3 kila mtu anataka viatu vya 3500
 
Hii imezidi bro
Hapana, usijali hii ni kawaida
Bado hawajazoea na pia hawakujui
Inabidi uwe na subra sana
Wengine moja kwa moja wanaanza kuwaza Ushirikina na kuanza kuulizia
Ujue biashara nyingi hufa miaka miwili ya kwanza
Ukitoboa hapo basi unaanza kujenga ukaribu na wateja
 
Duu hasa hapo kuna akiba si tutatumia kabisa
 
Biashara inahatua za ukuaji...ndo upo kwenye hatua ya kwanza be patient...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…