Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Pamoja na kuvurugika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kwanini Waziri Jafo hajiuzulu?

Najua kuwa Jiwe ndiye aliyetoa maagizo yote hayo, lakini kwa muumini wa dini kama Jafo, ni kwanini akubali hili jumba bovu limwangukie??
Nafikiri wapinzani waungane waache CCM kuèndelea na uchaguzi wao
 
Nafikiri wapinzani waungane waache CCM kuèndelea na uchaguzi wao
Absolutely true

Haiingii akikini kwa hao maccm kupanga mipango miovu ya kiasi hicho, halafu bado wapinzani waendelee kushiriki uchaguzi huo
 
Hivi Jafo anajua kuwa ni yeye ndiye anataka kuivuruga amani na anataka kuleta umwagaji damu nchini??

Hivi kukitokea machafuko hapa nchini kutokana na huu "uchafuzi" wanaoufanya, ni nani atalaumiwa??
Mawazo gani haya?
 
Ushindi wa kishindo wa mapema wa sisiem....
Hongera serikali ya awamu ya tano hii inadhirisha wananchi walivyo na amani nao....
 
Hivi Jafo anajua kuwa ni yeye ndiye anataka kuivuruga amani na anataka kuleta umwagaji damu nchini??

Hivi kukitokea machafuko hapa nchini kutokana na huu "uchafuzi" wanaoufanya, ni nani atalaumiwa??
Nani wa kuleta machafuko nchi hii?

Wote tunaishia nyuma ya keyboard tu hao viongozi wa upinzani wanaishia Twitter tu huko kulalama.

Wote wanaogopa kipigo cha mbwa koko hivyo hakuna machafuko yatakayotokea kwenye nchi hii labda machafuko ya kwenye mitandao.
 
Ukiwa CCM akili na ufahamu wako wote unausalimisha mfukoni mwa jiwe. Ukiwa na akili za Mussa Assad lazima utimuliwe na uchafuliwe.
Kiufupi, Jah Hana la kufanya zaidi ya kuitikia ndio mzee JIWE.
Bado wanadhani habari za machafuko Ni za Africa Kaskazini na Mashariki ya Kati
kwel mkuu!! jiwe ni hatari
 
Kuna watu wana mambo eti kuna machafuko kwenye mitandaoni nasio uraiani unajua maana ya demokrasia kweli wewe
 
Absolutely true

Haiingii akikini kwa hao maccm kupanga mipango miovu ya kiasi hicho, halafu bado wapinzani waendelee kushiriki uchaguzi huo
Hapo watawapa CCM sifa za kihuni kuwa wameshinda kwa kishindo kumbe uhuni mtupu. Kwa hyo wajiondoe mapema
 
Hivi Jafo anajua kuwa ni yeye ndiye anataka kuivuruga amani na anataka kuleta umwagaji damu nchini??

Hivi kukitokea machafuko hapa nchini kutokana na huu "uchafuzi" wanaoufanya, ni nani atalaumiwa??
Kwa kumbukumbu zangu mtu ambaye alishajiuzuru ni mmoja tu Mzee Mwinyi alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Haitatokea labda watumbuliwe.
 
Jafo ajiuzulu kwa kufanya alichotumwa kukifanya na amekifanya "vizuri" kupitiliza?
Acha vituko na wewe!
 
Kwa kumbukumbu zangu mtu ambaye alishajiuzuru ni mmoja tu Mzee Mwinyi alipokuwa waziri wa mambo ya ndani. Haitatokea labda watumbuliwe.
Na mwingine ni yule Mzee wa mamvi, mwaka 2008
 
Na mwingine ni yule Mzee wa mamvi, mwaka 2008
Huyo simkumbuki. Wangejiufunza toka wenzetu ambao hata kufanya mapenzi na subordinate wako ni kosa kama yule wa MacDonald aliyejiuzuru. Au akina Cameroon aliposhindwa kura ya maoni ya Brexit alivyoachia ngazi. Sisi hatoki mtu maana hawa ni wafalme, malkia na maprinces.
 
Act hakijasajiliwa na msajili
IMG-20191107-WA0000.jpeg
 
Jafo hawezi kujiuzulu, ajiuzulu kwasababu gani wakati ametimiza wajibu aliotumwa na boss wake?

Ministerial responsibility is associated with Parliamentary systems of government. Ministerial responsibility is the convention that a minister is answerable to Parliament for the conduct and actions of his or her ministry's personnel. Originally, the ministerial responsibility was quite strictly imposed on a minister and resignation might be demanded even where the minister did not have, and could not reasonably have been expected to have, knowledge of improper or negligent acts or omissions by officials. In recent times, this idea has been abandoned and it is rare for a minister to accept ministerial responsibility and resign. Individual ministerial responsibility is a constitutional convention in governments using the Westminster System that a cabinet minister bears the ultimate responsibility.
 
Jafo hawezi kujiuzulu, ajiuzulu kwasababu gani wakati ametimiza wajibu aliotumwa na boss wake?
Kinachompa kiburi Jiwe, ni hili Jeshi letu la Polisi, ambalo mishahara yao tunailipa walipa kodi wote wa nchi hii, bila kujali itikadi zetu za kisiasa

Namuomba Jiwe akasome maandiko matakatifu, katika kitabu cha Biblia, ili asome kilichompata yule mbabe Goliath, pamoja na kuwa na mavazi na silaha za kivita, lakini aliuawa na kijana mdogo tu Zaidi, ambaye yeye alitumia manati tu kama silaha yake!

Jiwe anapaswa atambue kuwa kwa Mungu hakuna kinachoshindikana, badala yake husimamia wale binadamu walioipitia mateso makubwa sana katika maisha yao
 
Upande wangu hili la uchaguzi litapita, Nina uhakika 100% watakuwa wajumbe wa CCM. Hofu yangu ni pale watakapoanza kutekeleza majukumu ndipo Viongozi watakapojuta, hapatakuwa na ushiriki wa wananchi na hivyo kukwamishwa kwa Kila kitu na mwishowe ni kukosa maendeleo kwa JUMLA. Kuna waliochaguliwa hawaamini kilichofanyika, wamevunjika MOYO, wana hofu na majirani zao, wanawaonaje, wanawachukukiaje, wanajiona wamebebwa hadi aibu wasiyoitarajia, wabaona heri wasingegombea. Yaani watataabika sana ktk Utawala wao.

Mitaondaoni na kwenye press realise za wakubwa watajisifia wamefanya vizuri huku nafasi zao zikiwa zimekosa Amani. Eti Mgombea wa act kaachwa kwa kuwa Chama chake hakipo kwenye orodha ya msajili. Halafu Ofisi inafungwa siku nzima, sijui hao watendaji warafanyeje kazi zao. Inaumiza sana. Walioshiriki KUFANIKISHA hili naamini watapongezana huku wakijuta nafsini mwao. Ijumaaa , JUMAMOSI na jumapili watajaa kwenye nyumba za ibada wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa waliyoshiriki.

Mwishowe turasikia bilioni 900 zimetumika kwenye uchaguzi huu. Km mpango ulikuwa huu ni heri ingetangazwa hakuna UCHAGUZI na hizo fedha zipelekwe kwenye miradi ya maji na Zahanati, mngebarikiwa sana lkn kwa hili naamini laana tunayo
 
Back
Top Bottom