Upande wangu hili la uchaguzi litapita, Nina uhakika 100% watakuwa wajumbe wa CCM. Hofu yangu ni pale watakapoanza kutekeleza majukumu ndipo Viongozi watakapojuta, hapatakuwa na ushiriki wa wananchi na hivyo kukwamishwa kwa Kila kitu na mwishowe ni kukosa maendeleo kwa JUMLA. Kuna waliochaguliwa hawaamini kilichofanyika, wamevunjika MOYO, wana hofu na majirani zao, wanawaonaje, wanawachukukiaje, wanajiona wamebebwa hadi aibu wasiyoitarajia, wabaona heri wasingegombea. Yaani watataabika sana ktk Utawala wao.
Mitaondaoni na kwenye press realise za wakubwa watajisifia wamefanya vizuri huku nafasi zao zikiwa zimekosa Amani. Eti Mgombea wa act kaachwa kwa kuwa Chama chake hakipo kwenye orodha ya msajili. Halafu Ofisi inafungwa siku nzima, sijui hao watendaji warafanyeje kazi zao. Inaumiza sana. Walioshiriki KUFANIKISHA hili naamini watapongezana huku wakijuta nafsini mwao. Ijumaaa , JUMAMOSI na jumapili watajaa kwenye nyumba za ibada wakimsifu na kumtukuza Mungu kwa waliyoshiriki.
Mwishowe turasikia bilioni 900 zimetumika kwenye uchaguzi huu. Km mpango ulikuwa huu ni heri ingetangazwa hakuna UCHAGUZI na hizo fedha zipelekwe kwenye miradi ya maji na Zahanati, mngebarikiwa sana lkn kwa hili naamini laana tunayo