Panama yaruhusu jeshi la Marekani kulinda na kuendesha mfereji wa Panama, Wachina watimuliwa

Panama yaruhusu jeshi la Marekani kulinda na kuendesha mfereji wa Panama, Wachina watimuliwa

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
933
Reaction score
3,051
Yani mngejua tu namna China anavyoichukia Marekani ya awamu hii na jinsi walivyo na hasira acheni tu, Soko kubwa la dunia nzima lipo Marekani wao wamepigwa pin kwa ushuru mrefu halafu nchi zingine wamepunguziwa 10 % tu, Hawajakaa sawa Marekani imewashinikiza Panama kuwafukuza wachina kwenye mfereji wa Panama.

Kwa muda mrefu, Mfereji wa Panama umekuwa kitovu cha biashara ya kimataifa, lakini pia uwanja wa vita vya kiushawishi kati ya mataifa makubwa. Sasa mambo yamechukua mkondo mpya – Panama imekubali rasmi kushirikiana kijeshi na Marekani kulinda na kuendesha mfereji huo muhimu, na kudhibiti ushawishi wa China .

Hii ni video ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth akiwa anatoa ripoti baada ya kurudi kutoka Panama

"Tumerudi tu kutoka Panama usiku wa kuamkia leo. Tulikuwa kwenye Mfereji wa Panama... na tumesaini mikataba kadhaa ya kihistoria... tunauchukua tena mfereji huo. China imekuwa na ushawishi mkubwa kupita kiasi. Obama na wengine waliwaruhusu kujiingiza polepole. Sasa, sisi pamoja na Panama, tunawapush waondoke, mheshimiwa."

We just got back from Panama last night. We were at the Panama Canal... and signed a couple of historic deals... we're taking back the canal. China's had too much influence. Obama and others let them creep in. We, along with Panama, are pushing them out, sir.

Katika hatua nyingine Panama imeridhia kuzipa meli za Marekani kipaumbele na pupunguza au kufuta ushuru kwa meli za Marekani zilizokuwa zikitozwa ada kubwa hapo kabla, pia Panama imeridhia kuingiza jeshi la Marekani kwajili ya ulinzi na kushirikiana kuendesha mfereji wa Panama Canal, Rais wa Marekani, Donald Trump amekubali ombi hilo kwa kutuma wanajeshi na vifaa vya kijeshi kuimarisha ulinzi
 
Kwa muda mrefu, Mfereji wa Panama umekuwa kitovu cha biashara ya kimataifa, lakini pia uwanja wa vita vya kiushawishi kati ya mataifa makubwa. Sasa mambo yamechukua mkondo mpya – Panama imekubali rasmi kushirikiana kijeshi na Marekani kulinda na kuendesha mfereji huo muhimu, na kudhibiti ushawishi wa China .

Katika hatua hii ya kihistoria, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth akiwa Panama mbele ya rais wa Panama, alitia msisitizo akisema “China did not build this canal. China does not operate this canal, and China will NOT weaponize this canal.” Na akafuatilia kwa kauli yenye ujumbe mzito: “We built it for Panama, not China. US and auxiliary ships will now be able to sail free.”
Ipo siku Mgermany naye atasema anakuja kuchukua vitu vyake alivyovijenga hapa TZ.
Panama hawakuwa na option maana ni kama hata kuvamiwa wangevamiwa. Ngoja nione Greenland kama itasalimika.
 
ngoja tuone ,ukiona nchi kubwa inaraia wana Anza kuwa na frame kariakoo

Juaga ,nchi hiyo sio tajiri bali serikali ndo tajiri
Marekani imedhamiria kuwaumiza China, hebu fikiria soko kubwa dunia nzima lipo Marekani lakini China wanafungiwa kwa kupigwa ushuru mrefu halafu nchi nyingine zimepewa ruhusa ya kulipa 10% tu, hawajakaa sawa wanatimuliwa Panama Canal
 
Panama Canal imejengwa kwa akili, jasho, na damu na wamerekani enzi hizo halafu eti mchina kiulaghai anataka aumiliki yehe! Hakuna kitu kama hicho.
Tatizo mchina hajui diplomasia, alipopata controll akaanza kuonyesha ubabe wa "nafanya chochote na hamtanifanya chochote" kile kiburi cha kutaka kuonekana unaweza kuionea Marekani dunia ikusifie, akaanza kwa maksudi kuzichelewesha meli za Marekani hadi za kijeshi ila anazipa kipaumbele meli za China, kuzitoza ushuru mkubwa meli za Marekani, n.k.

Hayo mambo yalivumiliwa na kina Biden, hii njemba iliyoingia white house haina mzaha ni vitendo tu
 
Congo nayo tayari wameshakabidhi nchi Yao Kwa trump, kubishana na mmarekani nahitaji Akili kubwa Sana
Marekani ikiongozwa na Rais anaeweza kuitumia Nguvu yake kikamilikfu sioni China wala Russia wala India zikipandisha mabega, Ni kimya !

Mchina kajijaza kwenye mfumo yupo bize kujibizana na Marekani kwenye kupandishiana tozo, Marekani wamefungua soko kwa nchi nyingine kulipia ushuru wa 10 % tu, kuna nchi nyingi sana zinatamani soko la Marekani ila wanazibwa na China na huu ndio wakati wa kutumia nguvu zote kuteka masoko ya Marekani, Yani mngejua tu namna China alivyopatwa na hasira acheni tu, wenzake wamepewa visu vya kula nyama choma yeye kapewa kijiko
 
Hawa clowns🤡 kwa nini matatizo yote ya America wanawatishwa Obama na Biden?!
 
Hizi propaganda huwa mnazitoa wapi?

China haijawahi kumiliki Panama Canal ila Panama ni member wa BRI, project ya China ya kufadhili ujenzi wa infrastructure

Iko hivi; kampuni binafsi ya Hong Kong inayoitwa CK Hutchnisons inamiliki bandari 2 eneo la Panama canal
​

  • Bandari hizi zimekaa eneo zuri sana kimkakati (strategic infrastructure) kibiashara na kiusalama kwa sababu ni kama gateway kati ya bahari ya Atlantic na Pacific​
​
  • Na ziko "one at each end of canal" unapoingia na kutoka. Ni moja ya checkpoint muhimu sana kwenye global maritime trade (5% of global container trade volume hupita hapo)​
Uongozi wa Trump ulichofanya ni kuishinikiza kampuni ya Hong Kong CK Hutchinson inayomiliki Container Terminal hizo 2 karibu na Panama Canal iziuze kwa kampuni ya Marekani ya BlackRock kwa USD 23 Billion.

Ilikuwa Hutchnisons na BlackRock wasaini mkataba wa mauziano April 02, 2025.

Serikali ya China iliingilia kati na kuizuia CK Hutchinson kuuza bandari hizo, biashara haijafanyika tena mpaka leo ni wiki 2 zimepita.

Mpaka sasa BlackRock na Washington wako kimya na CK Hutchinson haitasaini tena mkataba huo.

Kati ya Marekani na China nani mshindi hapo?

Marekani ingekuwa ni mshindi kama ingeweza kununua hizo bandari au kuishinikiza Panama ijitoe BRI lakini imeshindwa.

Muwe mnajitahidi kufuatilia mambo sio mnaokoteza vihabari uchwara mnavileta jukwaa la kimataifa kuwadanganya watu

​
 
Hizi propaganda huwa mnazitoa wapi?

China haijawahi kumiliki Panama Canal ila Panama ni member wa BRI, project ya China ya kufadhili ujenzi wa infrastructure

Iko hivi; kampuni binafsi ya Hong Kong inayoitwa CK Hutchnisons inamiliki bandari 2 eneo la Panama canal
​

  • Bandari hizi zimekaa eneo zuri sana kimkakati (strategic infrastructure) kwa sababu ni kama gateway kati ya bahari ya Atlantic na Pacific kibiashara na kiusalama. ​
​
  • Na ziko "one at each end of canal" unapoingia na kutoka. Ni moja ya checkpoint muhimu sana kwenye global maritime trade (5% of global container trade volume hupita hapo)​
Uongozi wa Trump ulichofanya ni kuishinikiza kampuni ya Hong Kong CK Hutchinson inayomiliki Container Terminal hizo 2 karibu na Panama Canal iziuze kwa kampuni ya Marekani ya BlackRock kwa USD 23 Billion.

Ilikuwa Hutchnisons na BlackRock wasaini mkataba wa mauziano April 02, 2025.

Serikali ya China iliingilia kati na kuizuia CK Hutchinson kuuza bandari hizo, biashara haijafanyika tena mpaka leo ni wiki 2 zimepita.

Mpaka sasa BlackRock na Washington wako kimya na CK Hutchinson haitasaini tena mkataba huo.

Kati ya Marekani na China nani mshindi hapo?

Marekani ingekuwa ni mshindi kama ingeweza kununua bandari hizo au kuishinikiza Panama iachane na BRI lakini imeshindwa.

Muwe mnajitahidi kufuatilia mambo sio mnaokoteza vihabari uchwara mnavileta jukwaa la kimataifa kuwadanganya watu

​
Wape madini mzee baba
 
Marekani ikiongozwa na Rais anaeweza kuitumia Nguvu yake kikamilikfu sioni China wala Russia wala India zikipandisha mabega, Ni kimya !

Mchina kajijaza kwenye mfumo yupo bize kujibizana na Marekani kwenye kupandishiana tozo, Marekani wamefungua soko kwa nchi nyingine kulipia ushuru wa 10 % tu, kuna nchi nyingi sana zinatamani soko la Marekani ila wanazibwa na China na huu ndio wakati wa kutumia nguvu zote kuteka masoko ya Marekani, Yani mngejua tu namna China alivyopatwa na hasira acheni tu, wenzake wamepewa visu vya kula nyama choma yeye kapewa kijiko
Ndio mlipobakia kujiona nyie mnakili sana kumbe unalala na kuku chumba kimoja sasa ww mandate ya kuisema China unaitoa wapi wakati mlo mmoja tu unakushinda
 
ngoja tuone ,ukiona nchi kubwa inaraia wana Anza kuwa na frame kariakoo

Juaga ,nchi hiyo sio tajiri bali serikali ndo tajiri
Tanzania inawanyima Raia wake Uraia pacha inafungulia mataifa mengine kama China kuja kufanya umachinga Nchini.

Ile Nchi ina watu Bilioni 1.5 almost, hawawezi wote kufanikiwa mule ndani lazima watoke kupumue, watafute masoko ya bidhaa zao nje na waziuze wao huko waendako.

Sisi tunafungia raia wetu, halafu hatuna technologia hata ya kutengeneza kijiko, tutajifunza wapi ikiwa wote ndani tunataka siasa?
 
Uraia pacha unazuiliwa kwa ajili ya kuilinda ardhi ya Wa tanzania.

Leo hii ukiwa na milioni 5 unapata kiwanja Dar. Kama u raia pacha ungeruhusiwa ingekuwa haiwezekani kupata kiwanja dar kwa milioni 5 leo hii
 
Hahaha Mbona Wachina wanainunua Majumba Mikocheni na Kariakoo, au ndio wao hawanunui ardhi wananunua Majumba tu?
Kiwanja cha Milioni Tano kiko wapi? Hata Buza Hakipo.
 
Back
Top Bottom