Yani mngejua tu namna China anavyoichukia Marekani ya awamu hii na jinsi walivyo na hasira acheni tu, Soko kubwa la dunia nzima lipo Marekani wao wamepigwa pin kwa ushuru mrefu halafu nchi zingine wamepunguziwa 10 % tu, Hawajakaa sawa Marekani imewashinikiza Panama kuwafukuza wachina kwenye mfereji wa Panama.
Kwa muda mrefu, Mfereji wa Panama umekuwa kitovu cha biashara ya kimataifa, lakini pia uwanja wa vita vya kiushawishi kati ya mataifa makubwa. Sasa mambo yamechukua mkondo mpya – Panama imekubali rasmi kushirikiana kijeshi na Marekani kulinda na kuendesha mfereji huo muhimu, na kudhibiti ushawishi wa China .
Hii ni video ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth akiwa anatoa ripoti baada ya kurudi kutoka Panama
"Tumerudi tu kutoka Panama usiku wa kuamkia leo. Tulikuwa kwenye Mfereji wa Panama... na tumesaini mikataba kadhaa ya kihistoria... tunauchukua tena mfereji huo. China imekuwa na ushawishi mkubwa kupita kiasi. Obama na wengine waliwaruhusu kujiingiza polepole. Sasa, sisi pamoja na Panama, tunawapush waondoke, mheshimiwa."
We just got back from Panama last night. We were at the Panama Canal... and signed a couple of historic deals... we're taking back the canal. China's had too much influence. Obama and others let them creep in. We, along with Panama, are pushing them out, sir.
View attachment 3300490
Katika hatua nyingine Panama imeridhia kuzipa meli za Marekani kipaumbele na pupunguza au kufuta ushuru kwa meli za Marekani zilizokuwa zikitozwa ada kubwa hapo kabla, pia Panama imeridhia kuingiza jeshi la Marekani kwajili ya ulinzi na kushirikiana kuendesha mfereji wa Panama Canal, Rais wa Marekani, Donald Trump amekubali ombi hilo kwa kutuma wanajeshi na vifaa vya kijeshi kuimarisha ulinzi