Panya Road wamerudi, tuchukue tahadhari, Polisi Dar wafanya msako wawanasa waliowapiga watu mapanga

👍Ngoja nifanyie kazi huu ushauri mtu anaweza kuona ni kama upuuzi ila ni silaha kubwa mno tena vipanya road vilivyokuwa havina nguvu unavichakaza vyote.
Silaha yao ni wingi wao.wakimbize hata na chainsaw.
 
Kama unaishi na mwanamke ambaye haumuamini au una watoto watundu tafadhali sana achana na hizi chemical
Ukiwa na mke mshali au mke moto usiweke bastola nyumbani badala iiue jambazi itakuua wewe
 
Huo mda wa kuandaa hilo pilau utalipata wapi panya road uzuka tu kama magaidi hawana siku wala saa mida yao huwa ni kuanzia saa 12 hadi saa 2 usiku makutanio yao huwa kwenye viwanja vya mpira ujifanya wanamechi au wanafanya mazoezi.
Wazo la ndoo la msosi wenye sumu linafaa maskani ya vibaka wanapovutia bhangi ni rahisi sana kuiteka saikolojia ya vibaka sababu ni viumbe visivyo na akili.Unakuwa na vihela vidogo na simu mbovu ya torch umebeba ndoo ya wali wa sherehe unakatiza mitaa yao wanakuweka mtu kati unakua mpole unawaambia sina kitu huu uwali nimechukua kwenye harusi niwaachieni mle.Unaenda zako kesho unapita kuchukua mrejesho.
Ukiwapa ushirikiano
 
Hii ya kutikishwa niliisikia inatumika kanda ya ziwa kuwapa adhabu wahalifu,sijajua effect zake zikoje kwa anayetikiswa,tupe no mkuu
Ubongo unavurugika na damu then unawahi kuzimu haraka.Sawa na adhabu ya kupewa umle nyoka mbichi
 
Vibaka wezi majambazi hawana huruma hawa linapokuja suala la kutaka pesa usiombe uuingie anga zao.Kama ujajipanga wape tu ushirikiano wape wakitakacho ukiingia anga zao
 
Mtaa mkiwa na ushirikiano vibaka awaji,pia vibaka uogopa mitaa iliyonyooka means Hakuna chocho,
 
Huyo aliyeuawa, alithibitika kweli au ndio mob justice?
 
Huyu alipigwa na Bodaboda na kuchomwa moto,na mkusanyiko wa wananchi mbalimbali ,sijapata exactly walimpataje huyo mMoja..
Tusijichukulie sheria mkononi, hiyo ni principle yangu, maana itauma sana kama mtu asie na hatia akafanyiwa unyama
 
Watoto wanaadabisha wazazi wao kwa kushindwa kuwalea ipasavyo.

Vitoto 26 vinasimamisha mtaa daah kweli Dar nyoso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…