Panya Road wapuuza karipio la Rais Samia, waendeleza uhalifu kama kawaida

Panya Road wapuuza karipio la Rais Samia, waendeleza uhalifu kama kawaida

Inashangaza sana Panya road vijana zaid ya 20 wanapanga na kujeruhi raia bila polisi kua na taarifa ila vikao vyote vya CHADEMA polisi wana intelejensia ya kuvijua na kuzuia visitokee.

Jeshi lishakua la kisiasa, limepuuza jukumu lake la msingi la kulinda raia na mali zao.
kama ktk taasisi kuna waajiriwa wanao report ktk mamlaka, wakiongozwa na mwenyekiti hapa una zani kuna nini?
 
Raisi aliongea kiwepesi sana na kwa sauti ya kike nzuri ila watakaoshughulika nao ni wengine si yeye.

Jamani, Tuwaonye hawa watoto, Pay back itakapoanza katoto kako kakawa mbele ya chatu mwenye njaa huku kapakawa unga na mafuta ya kuteleza hatakuwepo wa kumsaidia.
ATAOGOPA SANA LAKINI HATOPONA.

Wazazi na jamii mnaowafahamu hawa vijana nafasi ni hii ya kumsikiliza raisi na kuwaonya. Hii nchi ina raisi mwenye sauti nzuri ila ina watu katili wanaoilinda.
Hao kuna maeneo wanaenda kuvamia
Wanajua huko wanyonge

Ova
 
Inashangaza sana Panya road vijana zaid ya 20 wanapanga na kujeruhi raia bila polisi kua na taarifa ila vikao vyote vya CHADEMA polisi wana intelejensia ya kuvijua na kuzuia visitokee.

Jeshi lishakua la kisiasa, limepuuza jukumu lake la msingi la kulinda raia na mali zao.
Unajua kule tuna mapandikizi huwa yanatoa taarifa mapema ila kwa PR hamna untarajia mnara ya intelijensia usome japo E?
 
Magufuli aliwakuta wanatamba akawafuta kabisa.

Enzi za JK awa watoto walikuwa wanafunga mtaa na ikasemekana walishindikana.
Magufuli alitumia maguvu ya DOLA akaonekana kama vile kafanikiwa kupambana na hao Panya road na vikundi vingine.
Lakini alicho kifanya ni kulifukia (suppress) tu hilo tatizo, tena kwa muda. Tatizo lililopo hapa linaloongezeka kwa kasi ni ukosefu wa ajira hasa kwa vijana. Vijana wanazidi kuandamwa na umasikini wa kipato.
 
Pamoja na Rais wa nchi kusimama na kutoa kalipio kali kwa vijana wahalifu wa Panya Road.

Wameendeleza harakati zao za kujeruhi watu na kuiba mali.

Inabidi Rais sasa aonyeshe uongozi hii ni dalili mpaka watoto kama hawa ambao hata Makonda aliweza kuwafuta kwenye mitaa hawamuogopi na wanampuuza.

Kipindi hiki ndio uwa wananchi wanalia machozi kumisss uongozi strong wa Magufuli.

Soma: Panya Road wajeruhi 19, Mtongani
WAKULA KWA UREFU WA KAMBA ZAO

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Wameambiwa JK amerudi nao sasa wamerudi!
Ukweli ni kwamba hawa mnaowaita Panya Road are sending a signal showing the shortcomings in our society!! Kwani kuwa funga ndio suluhisho la njaa yao na familia zao? Kufanya hizo doria za Polisi is just postponing the problem!

Hivi nyie watawala hamuoni kuwa kuna uhusiano kati ya mfumuko wa bei( inflation) na ongezeko la uhalifu wakiwemo hawa mnaowaita panyaroad katika jamii?
 
Ufanisi katika utendaji kazi wa Jeshi la Polisi ukianza kutiliwa mashaka, kulegalega, ama kushindwa kutimiza kikamilifu majukumu yake, kinachopaswa kufanyika ni kubadilisha uongozi wote wa juu.

Ni aibu, kwa kuwa jeshi likiwa chini ya you wa Siro huyu huyu liliweza kuthibiti vyema vitendo vya uhalifu pale alipokuwa chini ya JPM, lakini leo amegeuka kuwa mlalamikaji na mpigaji mikwara mbuzi. Vibaka na majambazi hawapaswi kuchekewa ama kufanyiwa masikhara hata kidogo.
 
Kwa hiyo wewe kwa akili zako unafikiri panya road unaweza mpa ajira gani?
Ndugu,
Panya road ni mwanadamu kama wengine, anaweza kupewa ajira itakazomwezesha kupata kipato kilicho halali na kwa usalama HATA wa kwake kibaka mwenyewe, akatulia.
Hata Magufuli angekuwa MKWELI, kwenye takwimu za fursa na ajira alizokuwa anadai kutoa/kutengeza, tatizo hilo lingeweza kuendelea kupungua.
 
Suala la panya road liliwahi kuibuka ndani ya tawala zilizopita ikiwemo serikali ya Kikwete, Magufuli na sasa ya SAMIA.
Naomba msilichukulie hili jambo kama failure ya uongozi wa Samia.
Hebu nendeni Zingiziwa- Chanika muulizie habari za wale vijana panya road mtaambiwa wanaendeleaje , au nenda Tabata ule mtaa waliotia fujo muulizie habari za wale vijana.
Kama haitoshi nendeni central mtapata majibu.
Polisi wapo tu, na ndio walewale waliokuwepo kipindi cha Magufuli.
Kijana ukirogwa kujiingiza kwenye upanya road nakuhakikishia mtaani kwako hawatakuona na watakusahau.
Wanayofanyiwa hawa panya road na vyombo vya Dola mngeona mngeanza kuvilaani vyombo vya Dola.
Muviache vifanye kazi yake
 
Bila shaka na wewe ni mkabili panya road na panya buku
 
Pamoja na Rais wa nchi kusimama na kutoa kalipio kali kwa vijana wahalifu wa Panya Road.

Wameendeleza harakati zao za kujeruhi watu na kuiba mali.

Inabidi Rais sasa aonyeshe uongozi hii ni dalili mpaka watoto kama hawa ambao hata Makonda aliweza kuwafuta kwenye mitaa hawamuogopi na wanampuuza.

Kipindi hiki ndio uwa wananchi wanalia machozi kumisss uongozi strong wa Magufuli.

Soma: Panya Road wajeruhi 19, Mtongani
Panya road JPM zinalink vp ss hapo
 
Kwani kwa akili yako unadhani aliyetia fujo Tabata ndiye huyohuyo aliyetia fujo Zingiziwa au Kunduchi?
Hawa vijana wakisikia huko wenzao wanefanya hivi nao huhamasika kufanya bila kujua nini wenzao kimewakuta.
Mpuuzi wewe ingekuwa mumeo amekatwa panga usingeleta hizi blabla zako
 
Back
Top Bottom