Papa amvua Upadri Padri Munyeshyaka kwa kukiri kuzaa mtoto wa Kiume

Papa amvua Upadri Padri Munyeshyaka kwa kukiri kuzaa mtoto wa Kiume

Padre Munyeshyaka pia anahitajika nchi Rwanda kwa makosa ya mauji ya kimbali nchini humu mwaka 1992 wakati akihudumu kama padre wa parokia moja mjini Kigari wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Dah!...poor him..
 
Munyeshyaka-1.jpg

Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, #PapaFrancis amechukua uamuzi huo dhidi ya Wenceslas Munyeshyaka, mzaliwa wa Rwanda ambaye alikuwa akitumikia Kanisa hilo Nchini #Ufaransa kwa karibu miaka 30.

Ofisi ya Dayosisi ya #Évreux imesema Papa alisaini amri ya kuondolewa kazini kwa mtumishi huyo tangu Machi 2023 baada ya kuthibitisha kuwa Mtumishi huyo aliyekimbia mauaji ya #Kimbari mwaka 1994 ana Mtoto wa kiume mwenye miaka 10.

Munyeshyaka aliteuliwa kuwa Kasisi nchini #Rwanda mwaka wa 1992 ambako pia alituhumiwa kuhusika na mauaji ya Mamia ya #Watutsi waliokimbilia Kanisani kwake katika Mji Mkuu wa #Kigali, wakati wa mauaji ya kimbari.

=============

Pope Francis has sacked a Rwandan-born man, who has been serving as a clergyman in northern France for almost three decades, from priesthood.

A communiqué circulating online signed by the bishop of Évreux says that Wenceslas Munyeshyaka, 64, “automatically loses clerical rights” and “is excluded” from serving “anywhere else” as a priest.

The Office of the Diocese of Évreux has confirmed to the BBC the authenticity of the communiqué, which says it is based on a papal decree dated in March.

Mr Munyeshyaka, who fled to France after the Rwandan genocide in 1994, hasn’t commented on the decision.

He was suspended by his diocese in December 2021 after it emerged that he has legally acknowledged being a father of a 10-year-old boy.

Mr Munyeshyaka was ordained a priest in Rwanda in 1992, where he is accused of playing a role in the killing of hundreds of Tutsis who had fled to his church in the capital, Kigali, during the genocide.

Courts in France have cleared him of the genocide charges.
 
Attachments

  • 1683266375396.gif
    1683266375396.gif
    42 bytes · Views: 1
Kwanini asiwe na mtoto? Au kukiri kuwa na mtoto ndo kosa lake?
Au ina maana hatakiwi kuoa au kuwa na mtoto kwa maisha yake yote?
Kama jibu ni ndio basi nadiriki kusema hii sheria ni mbaya na inapelekea hawa watawa kufanya ile dhambi iliyokatazwa ndani ya Torati."USIZINI"

Enyi waumini msiangamie kwa kukosa maarifa,kwa nini Padre asioe au kuwa na mke au mtoto? Je,mnataka tutende dhambi ya kuenenda kinyume na maumbile? Maana imeandikwa, ole wake anaethubutu kubadilisha uumbaji wa Mungu aliye mkuu. Mnataka TUWAHASI hawa viongozi wetu wa kiroho ili wasipate haki ya kujamiiana? Kwa nini mnafanya hii dini iwe ngumu kiasi hiki?
TUTAFAKARI NA TUCHUKUE HATUA. Hakielimuuu ngoo ngooo ngoooo!
 
Usijifanye mjuvi kwa kitu ambacho hukijui, ni ushauri tu
 
Padre Munyeshyaka raia wa Rwanda aliyekuwa akihudumu katika parokia ya Evreux kaskazini kwa Ufaransa amefukuzwa padre na hakubaliwa kuhudumu popote duniani kwa kosa la kukili kuwa na mtoto wa maika kumi.

Padre Munyeshyaka pia anahitajika nchi Rwanda kwa makosa ya mauji ya kimbali nchini humu mwaka 1992 wakati akihudumu kama padre wa parokia moja mjini Kigari wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

====

Papa Francis amemvua upadri mzaliwa wa Rwanda ambaye amekuwa akihudumu kama kasisi kaskazini mwa Ufaransa kwa takriban miongo mitatu.

Taarifa inayosambazwa mtandaoni iliyotiwa saini na askofu wa Évreux inasema kwamba Wenceslas Munyeshyaka, 64, "anapoteza moja kwa moja haki za ukasisi" na "amezuiliwa" kutumikia "mahali popote" kama kasisi.

Ofisi ya Dayosisi ya Evreux imeithibitishia BBC uhalisi wa taarifa hiyo ambayo inasema kuwa inatokana na agizo la Papa la Machi.

Bw Munyeshyaka, ambaye alikimbilia Ufaransa baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, hajazungumzia uamuzi huo.

Alisimamishwa kazi na Dayosisi ya Evreux mnamo Desemba 2021 baada ya kuibuka kuwa amekiri kisheria kuwa baba wa mvulana wa miaka 10.

Bw Munyeshyaka alitawazwa kuwa kasisi nchini Rwanda mwaka wa 1992 ambapo anatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya mamia ya Watutsi waliokuwa wamekimbilia kanisani kwake katika mji mkuu wa Kigali wakati wa mauaji ya kimbari.

Mahakama nchini Ufaransa zimemuondolea mashtaka ya mauaji ya halaiki.

Chanzo: BBC Swahili

USSR
Kosa lake siyo kuzini ila mwanamke kukubali kubeba mimba yake, wenzake wanaendelea kuzini tu na wanawake na wengine hadi mashoga, ili mradi hakuna ujauzito au wamefanya abortion au wameficha watoto wanaendelea kubaki watumishi waaminifu wa kanisa.
 
Dr. Slaa alikua Padre akaruka na sister sister akazaa mapacha, wapo Canada wanakula Maisha
 
Kosa la padre ni kukiri, maana wapo wengi wana watoto na wamewajengea hadi vimada lakini kwakua hawaja kiri basi wameachwa waendelee na huduma
Kweli wapo wengi,kuna mmoja huyo kazaa watoto kama watatu na wote wanafanana nae na kamjengea kinyumba huyo mkewe
 
Mi walim mimbi sista angu kitambo hicho huko nyuma, nkaona dini ya hovyo hii, cha ajabu naksia chini kwa chini bado wako nae now miaka zaidi ya 10, padre alienda Italy ila zawadi ni kama kawa every Christmas, mara sista watoto wanasomeshwa bure kwenye seminary ilimradi mauza uza na sista aliolewa kitambo, hii dini bora waruhusiwe kuoa tu.
Haiwezekani.
 
Nakuungamia MUNGU wangu nawe Padre wangu kwani nimetenda dhambi na dhambi zangu ni hizi.....

Hiki ni Nini ?
Kwa hiyo hapo amesema "Nakuungamia Padre wangu"?? Acha kujitoa fahamu kwa mambo usiyoyafahamu, Haufahamu lolote kuhusu Sakramenti ya upatanisho, haujui lolote kuhusu daraja Takatifu, Wala haujui lolote kuhusu Biblia.
 
Back
Top Bottom