TANZIA Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88

TANZIA Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88

Mara eeh kardinali Protase Rugambwa kachaguliwa kuwa Papa
 
Haiwezekani ukaenda kituo cha polisi ukaombe kibiriti ili uvute bangi. Hakuna binadamu anaweza kuwatumikia mabwana wawili wenye kukinzana, ukiwa kwenye njia ya kumtumikia Mungu basi jitahidi kwa kadri uwezavyo umtumikie Yeye, kwani kinyume chake utajikuta unamtumikia shetani.
Njia za kuokoka zipo wazi na njia za upetevu zipo wazi na ni jukumu la watumishi wa Mungu kuwaonyesha binadamu njia zilizonyooka ili mtu akizifuata atapata uzima wa milele.
Kiongozi unajua shida inaanzia hapo unapochukua wewe jukumu la kufunga hesabu,nilipo-bold...

Unataka Watumishi wa Mungu wawaonyeshe wapotevu gani njia kama siyo wezi wazinzi makahaba mashoga etc?na kuna namna nyengine ya kuwaonyesha njia tofauti na kuwasubiri maeneo husika (Makanisani au Misikitini) ili kuwahubiria waachane na hizo dhambi?sasa mbona utake waitwe tu wezi wazinzi wasengenyaji lakini siyo mashoga?tatizo huwezi ukalitatua kama hujalikubali,kosa (kwa mujibu wenu) alilolifanya Papa,yaani mlitaka na yeye awalaani wakati hiyo siyo kazi yake yeye alitakiwa awashawishi kwa maneno matamu ili waingie Kanisani awahubirie hiyo dhambi waiache.
 
Mara eeh kardinali Protase Rugambwa kachaguliwa kuwa Papa
Papa anachaguliwaje?

Ni hivi makardinali wote duniani walio chini ya umri wa miaka themanini wataenda Roma(au vatikani sijui niseme) ambapo watakuwa na mkutano unaitwa konklave. Kwenye huo mkutano watapiga kura kumchagua baba mtakatifu ajaye. Baba mtakatifu akipatikana utaona moshi mweupe kutoka kwenye chimney(sijui neno la kiswahili).

Kwa Tanzania kardinali Protase Rugambwa ataenda kujiunga na makadinali wenzake. Kadinali Polycarp Pengo hataenda kwa kuwa mwaka jana nafikiri alitimiza miaka themanini. Hata hivyo kadinali Polycarp Pengo alishiriki konklave ya mwaka 2005 iliyomchagua Papa Benedikto XVI na konklave ya mwaka 2013 iliyomchagua Papa Fransisko.

Mbali na Polycarp Pengo kadinali Laurean Rugambwa alishiriki kwenye konklave iliyomchagua Papa Yohane Paulo II.
 
Vitu vya kushangaza sana mkuu. Ukiachilia kukataa kwenda kula raha na starehe huko Mbinguni, bado ni mtu mzima wa miaka 88 bado alikua anaogopa kufa. Anaogopa kwenda kuonana na Yesu, kuonana na Musa,Elia, Daudi, Yusuph, Ibrahim baba wa imani.

Hizi dini ni utapeli kama utapeli mwingine.
Imani ya kweli ipo na imani za kitapeli zipo.
Ukiona mtu anahubiri imani na ajenda yake kuu ni mambo ya kidunia basi itafakari mara mbili.
Tatizo kuna watu wanatumia mwamvuli wa dini kwa kujinufaisha wao na kuwanyonya wenzi wao.
 
Papa anachaguliwaje?

Ni hivi makardinali wote duniani walio chini ya umri wa miaka themanini wataenda Roma(au vatikani sijui niseme) ambapo watakuwa na mkutano unaitwa konklave. Kwenye huo mkutano watapiga kura kumchagua baba mtakatifu ajaye. Baba mtakatifu akipatikana utaona moshi mweupe kutoka kwenye chimney(sijui neno la kiswahili).

Kwa Tanzania kardinali Protase Rugambwa ataenda kujiunga na makadinali wenzake. Kadinali Polycarp Pengo hataenda kwa kuwa mwaka jana nafikiri alitimiza miaka themanini. Hata hivyo kadinali Polycarp Pengo alishiriki konklave ya mwaka 2005 iliyomchagua Papa Benedikto XVI na konklave ya mwaka 2013 iliyomchagua Papa Fransisko.

Mbali na Polycarp Pengo kadinali Laurean Rugambwa alishiriki kwenye konklave iliyomchagua Papa Yohane Paulo II.
Kadinali Laurean Rugambwa ndio alikuwa kadinali wa kwanza muafrika. Usishangae papa wa kwanza muafrika akatoka Tanzania wale wanaoamini mambo ya nyota.
 
Pia kadinali Laurean Rugambwa (marehemu au sijui hayati kwa sasa) alishiriki konklave ya mwaka 1963 iliyomchagua papa Paulo VI sambamba na za mwaka 1978 ya kwanza ilimchagua papa Yohane Paulo I na ya pili ilimchagua papa Yohane Paulo II.

Kumbuka papa Yohane Paulo I alihudumu kwa siku 33 tu kwenye kiti cha askofu wa Roma
 
Nani anaweza kuchaguliwa kuwa papa?

Mwanaume yeyote mkatoliki aliyebatizwa anaweza kuchaguliwa kuwa papa maana ake ata mimi naweza chaguliwa, hata hivyo makdinali huwa wanajipendelea kwahiyo tegemea miongoni mwa makadinali watakaosafiri kwenda roma kumchagua papa mpya mmoja wao atakuwa papa.
 
Kiongozi unajua shida inaanzia hapo unapochukua wewe jukumu la kufunga hesabu,nilipo-bold...

Unataka Watumishi wa Mungu wawaonyeshe wapotevu gani njia kama siyo wezi wazinzi makahaba mashoga etc?na kuna namna nyengine ya kuwaonyesha njia tofauti na kuwasubiri maeneo husika (Makanisani au Misikitini) ili kuwahubiria waachane na hizo dhambi?sasa mbona utake waitwe tu wezi wazinzi wasengenyaji lakini siyo mashoga?tatizo huwezi ukalitatua kama hujalikubali,kosa (kwa mujibu wenu) alilolifanya Papa,yaani mlitaka na yeye awalaani wakati hiyo siyo kazi yake yeye alitakiwa awashawishi kwa maneno matamu ili waingie Kanisani awahubirie hiyo dhambi waiache.
Sisi sote ni watendao dhambi hayupo kati yetu asiyetenda dhambi, lakini viongozi wa dini khususan wale wenye mamlaka katika jamii zao wawe mstari wa mbele katika kukemea maovu. Ikiwa mtu amekwiba basi aende kwa kiongozi wa dini atafute ushauri wa yeye kupata riziki yake kihalali na si kufanya dhuluma ya kumuibia mwenzake, ikiwa mtu mzinifu pia aende kwa kiongozi wa kiimani ili ampe nasaha za kuweza kuacha uzinifu, kwa mtu shoga hali kadhalika anatakiwa aende kwa kiongozi wa kiimani ili amuombee na kumnasihi ili aacha tabia hiyo yenye kumchukiza Mungu, ikiwa kiongozi wa kiimani utabariki hicho kitendo ili mtendaji awe karibu na wewe hivyo ni kuonyesha kwamba jambo hilo halina madhara na huenda watu wengine wakashawishika na kulitenda kwani litapata baraka na kiongozi mkubwa wa imani yao na machukivu ya Mungu yatakuwa kwa mtendaji na mwenye kulibariki pia.
 
Tunamshukuru Mungu kwa kifo chake maana aliku ni fitina hapa duniani, Adhabu kali ya moto iwe juu yake mzee wa kubariki ushoga
Hivi kuubariki ushoga, ndo waja mna nongwa kiasi hiki? Sasa anae kuja ndo ana halalisha kabisaa.
Sijui itakuajee, lol
 
Hivi kuubariki ushoga, ndo waja mna nongwa kiasi hiki? Sasa anae kuja ndo ana halalisha kabisaa.
Sijui itakuajee, lol
Rugambwa haweza halalisha amelelewa na mama mswahili ambye alikuwa mzuri kama wewe. Wewe unaweza fundisha mtoto wako ahalalishe vitu kama hivyo?
 
Kwakweli papa alikua anazingua anajifanya yupo kati, habariki wala hapingi alikua analeta ukakasi sana...... Alale salama
Subiri anae kuja, ndo atawafurahisha zaidi, yaan mtawehuka hatariii.
😂😂😂😂😂
 
Rugambwa haweza halalisha amelelewa na mama mswahili ambye alikuwa mzuri kama wewe. Wewe unaweza fundisha mtoto wako ahalalishe vitu kama hivyo?
Nasemaje, yajayo yanafurahishaaa.
 
Papa anachaguliwaje?

Ni hivi makardinali wote duniani walio chini ya umri wa miaka themanini wataenda Roma(au vatikani sijui niseme) ambapo watakuwa na mkutano unaitwa konklave. Kwenye huo mkutano watapiga kura kumchagua baba mtakatifu ajaye. Baba mtakatifu akipatikana utaona moshi mweupe kutoka kwenye chimney(sijui neno la kiswahili).

Kwa Tanzania kardinali Protase Rugambwa ataenda kujiunga na makadinali wenzake. Kadinali Polycarp Pengo hataenda kwa kuwa mwaka jana nafikiri alitimiza miaka themanini. Hata hivyo kadinali Polycarp Pengo alishiriki konklave ya mwaka 2005 iliyomchagua Papa Benedikto XVI na konklave ya mwaka 2013 iliyomchagua Papa Fransisko.

Mbali na Polycarp Pengo kadinali Laurean Rugambwa alishiriki kwenye konklave iliyomchagua Papa Yohane Paulo II.

Orodha ya Makardinali Wanaotajwa Zaidi​


1. Kardinali Pietro Parolin (Italia, miaka 70)​


  • Katibu wa Jimbo la Vatican na mwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa.
  • Anaonekana kama mgombea wa maelewano kati ya makundi ya kihafidhina na ya mageuzi ndani ya Kanisa.

2. Kardinali Luis Antonio Tagle (Ufilipino, miaka 67)​


  • Anajulikana kama "Francisko wa Asia" kwa mtazamo wake wa kichungaji na wa kimataifa.
  • Amehudumu kama mkuu wa Caritas Internationalis, ingawa alikumbwa na changamoto za kiutawala.

3. Kardinali Matteo Zuppi (Italia, miaka 69)​


  • Askofu Mkuu wa Bologna, anayejulikana kwa juhudi zake za amani na haki za kijamii.
  • Amehusika katika mazungumzo ya amani na anaungwa mkono na wafuasi wa mageuzi.

4. Kardinali Peter Turkson (Ghana, miaka 76)​


  • Amewahi kuwa Rais wa Baraza la Kipapa la Haki na Amani.
  • Angeweza kuwa Papa wa kwanza kutoka Afrika katika historia ya kisasa.

5. Kardinali Péter ErdÅ‘ (Hungaria, miaka 72)​


  • Askofu Mkuu wa Esztergom-Budapest na mwanasheria wa Kanisa mwenye msimamo wa kihafidhina.
  • Anajulikana kwa ujuzi wake wa lugha na uongozi wa kisheria.

6. Kardinali Jean-Marc Aveline (Ufaransa, miaka 66)​


  • Askofu Mkuu wa Marseille, anayejulikana kwa maoni yake ya maendeleo na juhudi za mazungumzo ya kidini.
  • Analinganishwa na Papa Yohane XXIII kwa mtazamo wake wa mageuzi.

7. Kardinali Joseph Tobin (Marekani, miaka 72)​


  • Askofu Mkuu wa Newark, anayejulikana kwa msimamo wake wa ujumuishaji, hasa kwa jamii ya LGBTQ+.
  • Amesifiwa kwa uongozi wake wakati wa migogoro.

8. Kardinali Juan José Omella (Hispania, miaka 79)​


  • Askofu Mkuu wa Barcelona, mwenye msisitizo kwenye haki za kijamii.
  • Amehusishwa na masuala ya uchunguzi wa unyanyasaji wa kingono, jambo linaloweza kuathiri nafasi yake.

Mchakato wa Uchaguzi wa Papa Mpya​


  • Makardinali wote walio chini ya umri wa miaka 80 wanaruhusiwa kushiriki katika konklave.
  • Kwa sasa, kuna makardinali wapiga kura 138 kati ya 253.
  • Mchakato huu hufanyika kwa siri katika Kanisa la Sistine, ambapo kura hupigwa hadi kufikia theluthi mbili ya kura kwa mgombea mmoja.
  • Moshi mweupe huashiria uchaguzi wa Papa mpya, wakati moshi mweusi huashiria kutokuwepo kwa mshindi.
 
Kama wewe ni Kardinali, kila la kheri muadhama katika harakati zako, ila sisi wa humu ndani hatuingii kwenye conclave. Kwanini uombe support humu
Ah mi sio Kadinali wala nini ila naamini kwa koneksheni zilizopo humu mkinipigia promo mbona nafasi naichukua ile asubuhi na mapema..?
 
Hivi kuubariki ushoga, ndo waja mna nongwa kiasi hiki? Sasa anae kuja ndo ana halalisha kabisaa.
Sijui itakuajee, lol
Hapana usiseme hivyo, kitu ambacho mtu kuona mtoto wako wa kiume wa kumzaa umemlea na kumsomesha halafu anajimithili jinsia ya kike, kwa kweli inatia uchungu sana. Sidhani kama kuna mzazi analifurahia hili.
 
Nasemaje, yajayo yanafurahishaaa.
Si tutaona

Papa ajaye atahubiri ukweli kwa uthabiti wala hakuna atakayechanganyikiwa tena kwa maana atautenga ukweli na uongo kama mchungaji anavyotenga mbuzi na kondoo. Hakuna tena mtu atamwita mbuzi we kondoo au kumuita kondoo wewe mbuzi.

Atahubiri ukweli wa Kristo kama alivyofanya mtangulizi wake Petro mtume, na watu wote waliopotea watatubu kwa vilio wakijipaka majivu na kinyesi kichwani wakifunga na kujifunika na gunia na kumrudia Mungu aliye hai, baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Waumini wa dini nyingine kutoka uarabuni, mashariki ya mbali na India watabatizwa, wakristo walokole, walutheri , waanglikana waorthodox wote watarudi ndani ya kanisa katoliki, Itakuwa dunia ya amani ambayo mfalme wake ni Yesu Kristo.
 
Back
Top Bottom