TANZIA Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88

TANZIA Papa Francis amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88

Waafrika wengi huwa wanajiona ni wafia dini na wanaijua dini zaidi kuliko hata hao waliozileta dini zenyewe.
Uyu Papa alisema kabisa,

mashoga wasinyanyapaliwe, wale ni walemavu Kama walemavu wengine.

Walemavu Wote wameumbwa na Mungu

Kama wapo walemavu WA miguu,mikono,ngozi.n.k, Basi waroma wasishangae uwepo wa walemavu WA vinyeo😂

Waroma WA tandika mishipa ikawatoka balaa😂
 
Nataka nigombee hiyo nafasi ndugu zangu Watanzania naombeni sapoti yenu basi..
Kama wewe ni Kardinali, kila la kheri muadhama katika harakati zako, ila sisi wa humu ndani hatuingii kwenye conclave. Kwanini uombe support humu
 
Upo sahihi kabisa,ok ndiyo mimi sasa nimekengeuka kama wengine wanavyokengeuka wakawa wezi,wazinzi (kuziniana mwanaume kwa mwanamke) mfitini,mnafiq,yote mabaya wanafanya then nipo mimi shoga!

Mkuu unataka kuniambia ni haki wewe kuruhusu hao wenzangu hapo juu waliotoka nje ya mstari wa Mungu kama mimi kujumuika na wewe kwenye mambo ya Kimungu bila kuzingatia udhaifu wao wa dhambi huku mimi ukiniacha?obviously utakapotaka kukaa nao hao ni ili waache dhambi so unaona kabisa ilikuwa haki mimi nife na dhambi yangu wakati ulikuwa na uwezo wa kuniita kama wadhambi wengine na mimi niokoke?

Check your facts,imani siyo hasira wote sisi tuna dhambi qualities tunaziweka sisi ila Mungu ikiwa tu alishawahi kuonya kitu basi hicho moja kwa moja akitendaye hana tofauti na aliyetenda kingine alichokataza
Haiwezekani ukaenda kituo cha polisi ukaombe kibiriti ili uvute bangi. Hakuna binadamu anaweza kuwatumikia mabwana wawili wenye kukinzana, ukiwa kwenye njia ya kumtumikia Mungu basi jitahidi kwa kadri uwezavyo umtumikie Yeye, kwani kinyume chake utajikuta unamtumikia shetani.
Njia za kuokoka zipo wazi na njia za upetevu zipo wazi na ni jukumu la watumishi wa Mungu kuwaonyesha binadamu njia zilizonyooka ili mtu akizifuata atapata uzima wa milele.
 
Papa ajaye huenda akawa mliberali, papa mkonsevativu ni kama hatakiwi kutokana na misimamo yake ya kihafidhina
 
Mm sijaelewa hata kidogo, pamoja na kuwa nimeangalia video na kusoma subtitles zote lkn sijaipata mantiki ya kile ulichoandika.
Tunaomba uzi ufungwe kwa comment hii.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Kwamba papa badala afurahie kifo, akakae na kina yesu na MUSSA meza Moja, eti naye anapambania maisha yake ili asife
Vitu vya kushangaza sana mkuu. Ukiachilia kukataa kwenda kula raha na starehe huko Mbinguni, bado ni mtu mzima wa miaka 88 bado alikua anaogopa kufa. Anaogopa kwenda kuonana na Yesu, kuonana na Musa,Elia, Daudi, Yusuph, Ibrahim baba wa imani.

Hizi dini ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Kadinali Protade Rugambwa askofu wa Tabora kuwa Pope.


Toka Maktaba 2023

1745237756338.jpeg

Historia ya makadinali kutoka Tanzania :

19 2024
Vatican City
KANISA la SANTA MARIA IN MONTESANTO JIJINI ROME KARDINALI RUGAMBWA

Sherehe iliyoambatana na sala wakati wa kukabidhishwa Rasmi KANISA la SANTA MARIA IN MONTESANTO JIJINI ROME KARDINALI RUGAMBWA ni Arcivescovo wa Jimbo la Tabora.

View: https://m.youtube.com/watch?v=PfOyI0V2PQo
sherehe zilihudhuriwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA nchini Italy Mh. Mahmoud Thabit Kombo, Wanafunzi wa Vatican na Diaspora.

Toka maktaba 2023:






Baba Mtakatifu Fransisco amemteua Askofu mkuu Mwandamizi Protase Rugambwa kuwa Kadinali. Mhashamu Protase Rugambwa ni mwandamizi wa kiti cha uaskofu Jimbo kuu Katoliki la Tabora.



Mhadhama Rugambwa anakua Kadinali wa tatu katika historia ya Kanisa Katoliki Tanzania. Kadinali wa kwanza alikua Mhadhama Kadinali Laurian Rugambwa kuanzia mwaka hadi alipofariki dunia mnano Desemba 8, 1997 akiwa na umri wa miaka 85 alihudumu akiwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuula Dar es salaam Kuanzia mwaka 1968 hadi



Baba Mtakatifu Paulo XXIII Alimteua Hayati Laurian Kardinali Rugambwa Kwa Kumpa Adhama ya Ukardinali na Kumsimika Rasmi 28/03/1960 hadi alipofariki Dunia mwaka 08/12/1997



Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa Askofu Mwandamizi Polycarp Pengo, kuwa Kardinali na kumsimika rasmi tarehe 21 Februari 1999.

Tanzania ikaweka historia ya kupata Kardinali mpya miezi michache tu baada ya kufariki dunia, Kardinali Laurian Rugambwa. Tarehe 2 Septemba 1990 wakati Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea Tanzania, Kardinali Polycarp Pengo, aliyekuwa Askofu mkuu mwandamizi,



Hongera sana Mhashamu Rugambwa.



Taarifa toka Vatican

Sister Angela Rwekiza
 
Nilimpenda kwa alivyowatetea wapalestina. Aliniudhi aliposema mashoga wapewe nafasi
Apumzike anapostahili
 
Back
Top Bottom