Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

Upapa hauwezi kuunga mkono dhambi. Kamwe.
Ni wazi hujui maana ya dhambi. Period!

👉Ibada za sanamu?
👉Ibada kibao za wafu?
👉Kumwabudu ^Bikra^ Maria???
👉Kuungama dhambi kwa mapadre, badala ya kumwomba Mungu moja kwa moja???

👉 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ~ Matendo 4:12

👉14. Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.

👉15. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.

16. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. ~Waebrania 4:14-16
 
Unajua hoja mama ya Padre Martin Luther kuasi RC?.

Ukitambua hilo utaelewa kuna nyakati kanisa lilihalalisha baadhi ya maovu.
Martin aliasi kwa sababu za kisiasa. Thesis zake zote zilikuwa addressed accordingly. Shetani akishakujaa nawe ukakubali kujaa mwisho wako lazima uwe mbaya kama wa Martin Luther.
 
Inahitaji uwe mjinga wa kiwango cha juu sana ndio ushindwe kujua kuwa RC sio dini bali kikundi cha watu walioweka mfumo wa biashara duniani kupitia mgongo wa dini. Dunia yote imekuwa deceived na RC.
 
Ni wazi hujui maana ya dhambi. Period!

👉Ibada za sanamu?
👉Ibada kibao za wafu?
👉Kumwabudu ^Bikra^ Maria???
👉Kuungama dhambi kwa mapadre, badala ya kumwomba Mungu moja kwa moja???

👉 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ~ Matendo 4:12

👉14. Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.

👉15. Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.

16. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. ~Waebrania 4:14-16
▪︎ Hatuabudu sanamu
▪︎ Hatuabudu wafu
▪︎ Hatumwabudu Mama Bikra Maria mama wa Mungu
▪︎ Hatuungami kwa Padre, tunaungama kwa Mungu kupitia kwa Padre kama alivyotuagiza

Shida yenu mkikariri vimistari viwili vitatu kutoka kwenye Biblia iliyofanyiwa compilation na Wakatoliki.

Hamuujui Ukatoliki lakini kutwa kucha kuhangaika kujifanya mnaujua na kujipa umuhimu msiokuwa nayo.

Poleni sana.
 
Kwa kifupi Katoriki siyo Kanisa la Mungu! Asikudanganye mtu kabisa.
Katoriki ni dhehebu la Mpinga Kristo! Ndiyo dhehebu lililoongoza mauaji ya Watakatifu Wakristo kuliko unavyofikiri.
Papa siyo Mtumishi wa Mungu bali ni Kiongozi wa dini ya Kikatoriki duniani.
Sure...wakina kaisari Neto,costantino wote hawa wali husika kiwatesa wakristo wa kwel
 
Martin aliasi kwa sababu za kisiasa. Thesis zake zote zilikuwa addressed accordingly. Shetani akishakujaa nawe ukakubali kujaa mwisho wako lazima uwe mbaya kama wa Martin Luther.
Kwa mfano, kitendo cha kulipa hela ili upewe cheti cha msamaha wa dhambi ambacho kilikuwa kinadumu kwa kipindi flani, ni sahihi kwa mjibu wa imani ya Kikristo?.
 
bibisii ni wazushi.
hakuna chombo chochote cha Vatican kilicho report habari za papa kukubalina na mashoga..

na kwa hulka ya kanisa moja, takatifu, Katoliki na la mitume, siyo kujibizana na vyombo vya habari..
Hawana muda wa kujibu upuuzi na uzushi.
mchakato wa kanisa kubariki ushoga unapikwa na utakapowekwa hadharani ndio utajua haujui kwasababu dalili zinaonekana waziwazi
 
▪︎ Hatuungami kwa Padre, tunaungama kwa Mungu kupitia kwa Padre kama alivyotuagiza
Samahi kiongozi, unaweza nisaidia andiko linalotaka tupitie kwa kiongozi wa kiimani ili kuungama dhambi zetu?.

Ninatanguliza shukrani.
 
mdogo mdogo shetani anapiga hodi kwenye vigango na parokia.

Ukisharuhusu mwanaume aliyeoa mwanaume mwenzie kuwa baba wa ubatizo wa watoto, unategemea hao watoto watauonaje ushoga?, si wataona ni kitu cha kawaida tu, yaani hakuna noma!
 
bibisii ni wazushi.
hakuna chombo chochote cha Vatican kilicho report habari za papa kukubalina na mashoga..

na kwa hulka ya kanisa moja, takatifu, Katoliki na la mitume, siyo kujibizana na vyombo vya habari..
Hawana muda wa kujibu upuuzi na uzushi.
Wewe unawakilisha kundi kubwa la wajinga ambao kutokana na ufinyu mdogo wa akili unaona kumpinga papa ni dhambi kubwa sana kwahiyo hata aongee kitu gani kutokana na ujinga wako utamtetea . Kwakifupi umeshindwa kuisimamia akili yako vyema na una ufinyu wa fikra. Pole sana nyie ndio mitaji yenyewe ya kanisa la roman Catholic.
 
Kwa mfano, kitendo cha kulipa hela ili upewe cheti cha msamaha wa dhambi ambacho kilikuwa kinadumu kwa kipindi flani, ni sahihi kwa mjibu wa imani ya Kikristo?.
Ni sahihi. Kila dhambi uitendayo inapaswa kufanyiwa malipizi.
 
Ikumbukwe huyu Papa wa Vatican anaeongoza Kanisa la RC almaaufu Kanisa Takatifu la Mitume kama wanavyojiita wao ameamua kuwaburuza wenzake wafuate msimamo wake.

Baadhi ya mambo ambayo anataka Kanisa lake lifuate ni

-Kuwatambua Mashoga bila kukemea akisema wenye dhambi ndio wanatakiwa kwenda kanisani

-Kubariki Ndoa za mashoga

-Kufuhusu utoaji Mimba

-Kutambua watu Waliobadili Jinsia kinyume na maumbile Yao ya Asili

-Kuwa na msimamo legelege na kuficha taarifa za watawa wanaokumbwa na kashfa za kulawiti Watoto wadogo.

-Kufuhusu Baadhi ya Maaskofu wa RC huko Amerika ya Kusini kuoa kinyume na msimamo wa Kanisa lao Hilo la Mitume.

Haya wenye Kanisa lenu johnthebaptist mnaitwa huku 😁😁

==========≈=

Papa Francis amemfuta kazi askofu Joseph Strickland, ambaye ni mkosoaji mkubwa aliyeibua maswali juu ya uongozi wa Papa katika Kanisa Katoliki.

Kwa mujibu wa taarifa ya Vatican, askofu huyo ameondolewa madarakani kufuatia uchunguzi katika Jimbo Katoliki la Tyler, huko Texas, Marekani alilokuwa akiliongoza .

Askofu Strickland ni mmoja kati ya sauti kinara katika tawi la uongozi wa Kanisa Katoliki nchini Marekani ambalo linapinga vikali mabadiliko yanayopigiwa chapuo na Papa.

Kuondolewa kwake kunakuja baada ya Papa kuzungumzia juu ya hali “ya kuwa nyuma” kifikra ya baadhi ya viongozi wa Kikatoliki nchini Marekani.

Askofu Strickland mara kadhaa ameshambulia hatua za Papa kutaka kubadili msimamo wa Ukatoliki katika masuala kadhaa ya kijamii ikiwemo kutoa mimba, haki za waliobadili jinsia na ndoa za jinsi moja.

Mwezi Julai mwaka huu, alionya kuwa mafunzo mengi ya Ukatoliki ambayo ni ya “ukweli wa msingi” yalikuwa yanapingwa, ikiwemo kile alichokiita majaribio ya “kudunisha” ndoa “kama ilivyoundwa na Mungu” baina ya mwanamume na mwanamke tu.

Askofu huyo pia amekosoa majaribio hayo aliyoyaita ya “kuvunja miiko” na kusema wanaoyapigia chapuo “wanapinga utambulisho wao wa kibailojia waliopewa na Mungu”.

Katika barua yake ya mwezi Julai, askofu Strickland amedai kuwa majaribio “kubadilisha visivyobadilika” yatasababisha mfarakano mkubwa ndani ya Kanisa. Na wale wanaotaka mabadiliko, ameonya kuwa “ndio hasa wanaofarakanisha [Kanisa]".

Askofu Strickland alikuwa chini ya uchunguzi wa Vatican na hapo awali alitupilia mbali uwezekano wa kujiuzulu, na katika barua ya wazi mwezi Septemba alimtaka Papa amfute kazi.

"Siwezi kujiuzulu kama Askofu wa Tyler kwa sababu kufanya hivyo itakuwa ninawatelekeza wana kondoo,” alisema.

Kwa mujibu wa Vatican, uamuzi wa kumfukuza umefikiwa baada ya “ziara ya kitume katika Jimbo la Tyler iliyoagizwa na Papa mwezi Juni".

Vyombo vya habari vya Kikatoliki vinaeleza kuwa uchunguzi huo pia uliangazia masuala ya kifedha katika jimbo hilo.

Askofu Strickland, 65, aliteuliwa kuwa askofu mwaka 2012, wakati wa Papa Benedikto XVI.

Vatican imesema kuwa Jimbo la Tyler kwa sasa litaongozwa kwa mpito na Askofu Joe Vasquez wa Jimbo la Austin.

Hatua hii inafuatia hatua mahususi zinazochukuliwa na Papa ili kulifanya Kanisa Katoliki kuendana na wakati kwenye utawala wake.

Siku ya Alhamisi, Vatican ilitangaza kuwa watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa katika Kanisa Katoliki ilimradi kwa kwa kufanya hivyo hakutazua kashfa ama “mchafuko”.

Mwezi Oktoba Papa alisema kuwa Kanisa linaweza kukubali kubariki wanandoa wa jinsi moja, huku akiwaeleza makardinali kuwa "hatuwezi kuwa majaji ambao tunachofanya ni kukana, kukataa na kutenga tu".

Akizungunza katika mkutano wa Siku ya Vijana Duniani jijini Lisbon Papa alisema kuwa mgando wa fikra wa baadhi ya watu “hauna manufaa”.

"Kwa kufanya hivyo unapoteza utamaduni halisi na utategemea itikadi ili kuungwa mkono. Kwa maana nyingine, itikadi inachukua nafasi ya imani,” aliongeza kusema.

Mabadiliko ya tabianchi pia imekuwa ni moja ya ajenda kuu ya utawala wa Papa Francis - ambapo mwaka 2015 alitoa chapisho muhimu kuhusu mazingira ambalo lilionya kuwa dunia ilikuwa inaelekea hatua mbaya zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Papa pia amewashutumu vikali wale wote wanaokanusha mabadiliko ya tabianchi na anatazamiwa kuwa katika mkutano wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP28 baadae mwezi huu huko Dubai.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Papa kuhudhuria toka mikutano hiyo ianzishwe mwaka 1995.

Chanzo: BBC
Kitabu cha haki kimebakia kuwa quran tu ikizingatia kwa makini hakijawahi kubadilika na hakitobadilika, huku kwingine ni maono ya wazungu tu
 
Back
Top Bottom