Hatuabudu sanamu, hatujawahi kuabudu sanamu na kamwe hatutakuja kuabudu sanamu.
Kukana tu kwa maneno hakusaidii kuondoa ukweli ulio wazi kwamba Ukatoliki
unasujudia na
kuabudu sanamu ambazo Biblia imepiga marufuku mara nyingi sana, na kwa maneno makali kadiri iwezekanavyo.
👉 [3] Usiwe na miungu mingine ila Mimi.
👉 [4]
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
👉 [5]
Usivisujudie wala
kuvitumikia; kwa kuwa Mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, ~ Kutoka 20
👉Isaya 44:9-20
Tunamuabudu Mungu. Tunamuabudu asiyeonekana kupitia vielelezo vinavyoonekana kama wana wa Israel walivyofanya kupitia nyoka wa shaba (Rejea Hesabu 21:8).
Kama ilivyoelezwa katika Kutoka 20 (hapo juu) Maandiko yamekataza kabisa
KUJIFANYIA SANAMU ZA KUCHONGA,
KUZISUJUDIA na
KUZITUMIKIA.
Ukatoliki utambue kwamba umejifanyia sanamu hizo za kuchonga, na hiyo, kwa mujibu wa Biblia, ni ibada ya sanamu.
Kitendo chao cha kuzisujudia, kuzibusu, kuzikumbatia katika utashi wa kiroho, hiyo ni ibada ya sanamu.
Kitendo chao cha kuzihudumia, kuzipa heshima na umuhimu na umaana wowote wa kiroho, huko ni kuzitumikia. Biblia inataja suala hilo kuwa ni ibada ya sanamu.
Kumhusu nyoka wa shaba, Biblia imefafanua kikamilifu kwenye Injili ya Yohana: 3:
👉[14] Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo
Mwana wa Adamu hana budi
kuinuliwa;
[15] ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye.
Biblia haijasema sanamu ziinuliwe, bali
Mwana wa Adamu (Yesu Kristu), ndiye apewe nafasi ya kuinuliwa na kutukuzwa mioyoni na maishani mwetu.
Kuombea wafu ni sawa na kuabudu wafu? Kwamba ombi ni sawa na ibada?
Ukatoliki unamwomba ^Bikra^ Maria. Hilo liko wazi kwenye ibada zao.
Hiyo siyo tu kwamba ni
ibada ya wafu, lakini pia ni
ibada ya sanamu.
Ukatoliki unaabudu mizimu, kwa sababu Mariamu, mamaye Yesu alikufa, akazikwa na hakuna kumbukumbu yoyote ya Biblia kwamba alifufuka na kupaa mbinguni.
Ukatoliki unaabudu miungu kwa sababu hata kama Mariamu angelikuwa hai mbinguni, bado hana sifa za kuombwa dua na kuabudiwa kama wafanyavyo Wakatoliki.
👉Wala hakuna wokovu
katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ~Matendo 4:12
Kama hakuna wokovu kwa mwingine awaye yote mbali na Kristu, kwa mujibu wa Biblia, sasa mahangaiko ni ya nini kwa Wakatoliki juu ya Mariamu, tena mtu ambaye ni mfu???
Maana yake, Ukatoliki umemgeuza Mariamu kuwa mungu wao, kwamba hajafa na kwamba anao uwezo wa kuwasaidia na kuwaokoa. Vinginevyo wasingethubutu kabisa kumwomba! Ibada ya sanamu!!!
Kwa taarifa yako tu; hatuna sala ya hivyo. Fanya utafiti kabla ya kuja kutuhumu.
Sala ya ^Bikra^ Maria ni uthibitisho mkubwa mojawapo kwamba Ukatoliki unaabudu mizimu na ibada ya sanamu. Hii ni kinyume kabisa na Maandiko Matakatifu ambayo ndiyo msingi mkuu wa Ukristu.
Ni wapi ambapo padre ametajwa katika andiko hili la Mathayo 18?
Katika agano jipya, baada ya kifo cha Yesu Msalabani, waumini wote wanahesabika kama makuhani wa Mungu.
👉Bali ninyi ni mzao mteule,
ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. ~1 Petro 2:9
Mfumo wa Agano la Kale wa ukuhani ambapo wana wa Israeli walipaswa kwenda kwa kuhani kwenye hema takatifu, maskani au hekaluni, wakiwa na dhabihu zao, ulikuwa kielelezo cha kumwakilisha Masihi Kristu ajaye.
Mfumo huo ulikoma baada ya kifo cha Yesu, ndiyo maana wakati Kristu akikata roho, pazia la hekalu lilipasuka vipande (Mathayo 27:50, 51), ikiashiria kwamb huduma hiyo sasa haina maana, kwa vile imetimia na kutimilika katika Kristu.
Mambo hayo yalikuwa
^kivuli cha mambo yajayo^ -- yaani yalilenga kwa Kristu Yesu (Kolosai 2:17).
Nina uhakika haujui chochote kuhusu Ukatoliki.
???🤔🤔🤔
NB: Ukatoliki mnaouhangaikia na mnaoufahamu ni tofauti na Ukatoliki wetu.
Ukatoliki tunaoupinga kwa nguvu zote ni ule ambao:
👉unafundisha kwamba papa ndiye mwenye mamlaka juu ya Ukristu duniani -- yaani ndiye kaimu wa Mungu.
👉unadai Mtume Petro ndiye papa wa kwanza na kwamba mapapa wote wamerithi na wanarithi mamlaka yao kutoka kwake.
👉unadai kwamba mapokeo ya kanisa na mafundisho ya maaskofu wao na miongozo ya mabaraza iko sambamba na Biblia kimamlaka.
👉unafundisha kwamba ubatizo siyo lazima kuzamisha majini, hata kunyunyiza ni sawa.
👉unadai kwamba katika huduma takatifu ya Meza ya Bwana, vielelezo vya mkate na divai hugeuka kuwa mwili na damu
halisi ya Kristu.
👉unafundisha kwamba Maria, mlolongo wa watakatifu, hata waliokwishakufa tayari, wanachangia katika wokovu wetu, kwa kuombwa dua.
👉unafundisha fundisho potofu la toharani ama pagatoria, kwamba ni mahali pa mateso ya utakaso kwa muda kwa ajili ya waumini ambao si waovu sana kiasi cha kwenda jehanum na wala si wema vya kutosha kuingia mbinguni.
👉unafundisha kwamba una mamlaka ya kubadilisha na kubatilisha Maandiko Matakatifu kama upendavyo wenyewe.
👉unafundisha kwamba wokovu haupatikani kwa neema bali kwa matendo; kwamba kipimo cha wokovu ni kwamba tu matendo ya wema yazidi yale maovu; kwamba kadiri muumini anavyojitesa, anavyotoa pesa, juhudi na mali kumtumikia Mungu na kanisa, kadiri anavyofanya huduma na ibada, nk ndivyo anavyo anahesabiwa haki machoni pa Mungu. Ndiyo maana Ukatoliki na Uislamu ni mapacha na mapapa wawili wanaofanana.
👉unafundisha kuchonga, kusujudia, na kutumikia sanamu kwa kisingizio kwamba unatumia kama vielelezo tu vya ibada.
👉Kama mambo haya na mengine mengi yanayofanana nayo ni tofauti na Ukatoliki wenu, basi una haki ya kukaa pembeni, maana wewe hauhusiki hapo.
Kanisa pekee lililoanzishwa na Kristu.
👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu Kristu kwao hatoshelezi kwa wokovu, lazima asaidiwe na akina Maria na watakatifu wengine.
👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu unapingana waziwazi na Maandiko Matakatifu.
👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu umepoka mamlaka ya Kristu, na papa kujiweka kama mungu duniani.
👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu historia ya matendo yake, mauaji ya Wakritu uliyoyafanya, ukatili wake katika nyakati zote vinapingana kabisa na Ukristu.
👉Ni sahihi 100% kusema kwamba Ukatoliki ni wakala wa Shetani duniani, ambaye hujificha kwenye vazi la Ukristu na utu wema.
👉Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo,
walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. ~ Mathayo 7:15
👉Wito wa Mungu kwa waumini na Wakristu wote, hata wale waliomo kwenye jumuia ya imani potofu ya Ukatoliki:👇
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema,
Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana
dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. ~Ufunuo wa Yohana 18:4, 5