Papa Francis amtimua Askofu anayempinga kuhusu kuruhusu ndoa za jinsia moja, kutoa mimba na waliobadili jinsia

▪︎ Hatuabudu sanamu
Ila? Sanamu zilizojaa makanisani, mnayoibusu na kuisujudia??? Wake up, don't be a religious fool.

Mungu anabudiwa katika Roho na Kweli. Yohana 4:24.

▪︎ Hatuabudu wafu
Siku ya kuwaombea wafu inahusikaje na wokovu?

▪︎ Hatumwabudu Mama Bikra Maria mama wa Mungu
^Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu.^

Sala ya Ukatoliki inaenda namna hiyo. Hiyo ni ibada ya wafu.

👉Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ~ Matendo 4:12

▪︎ Hatuungami kwa Padre, tunaungama kwa Mungu kupitia kwa Padre kama alivyotuagiza

👉Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. ~1 Yohana 1:9

Hakuna padre aliyetajwa hapo wa kuungamiwa dhambi zetu wala kutumika kama kiunganishi kati ya mdhambi na Mungu.

Kwa sababu Kristu ndiye Kuhani Mkuu kwetu, nasi Wakristu woote kwa pamoja ni ^ukuhani wa kifalme^

👉Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake Yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. 1Pet. 2:9

Shida yenu mkikariri vimistari viwili vitatu kutoka kwenye Biblia
Inasikitisha na ni aibu pia kwamba Ukatoliki unafundisha kinyume na hilo Neno.

👉Lakini Yeye [Kristu] alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika. Luka 11:28
 
Samahi kiongozi, unaweza nisaidia andiko linalotaka tupitie kwa kiongozi wa kiimani ili kuungama dhambi zetu?.

Ninatanguliza shukrani.
Hakuna andiko kama hilo, Mwanzo hadi Ufunuo.

Wewe binafsi ukimwomba Mungu kwa imani, kwa unyenyekevu, ukatubu dhambi zako zote, kwa neema ya Yesu Kristo anakusamehe na kukupa nguvu ya Roho Mtakatifu.

👉Mkiomba neno lolote kwa jina Langu, nitafanya. Yohana 14:14.

Mathayo 18:18
Hilo andiko halihusiani na mwanadamu kuomba msamaha kwa Mungu kupitia kuhani.
Majibu yake tu huonesha ni tapeli wa imani ya Ukristu. Hawana majibu, ndiyo maana wanafoka kama Mafarisayo na Masadukayo.

👉Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. ~1Petro 3:15

Andika Biblia yako uweke maana zinazokufurahisha.
Hawa hawaujui Ukristu, hawaijui Biblia na wala hawamtambui Yesu, na wala hayumo mioyoni mwao wala karibu nao.

Wanachojua wao ni kulitumia jina la Kristu ili kujinufaisha na kujitajirisha kidunia.

👉Na siku hiyo wanawake saba watamshika mtu mume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu. ~Isaya 4:1
 
Reactions: K11
kwani mkatoliki anahubiri injili ya nani?
 
Ila? Sanamu zilizojaa makanisani, mnayoibusu na kuisujudia??? Wake up, don't be a religious fool.

Mungu anabudiwa katika Roho na Kweli. Yohana 4:24
Hatuabudu sanamu, hatujawahi kuabudu sanamu na kamwe hatutakuja kuabudu sanamu.

Tunamuabudu Mungu. Tunamuabudu asiyeonekana kupitia vielelezo vinavyoonekana kama wana wa Israel walivyofanya kupitia nyoka wa shaba (Rejea Hesabu 21:8).

Siku ya kuwaombea wafu inahusikaje na wokovu?
Kuombea wafu ni sawa na kuabudu wafu? Kwamba ombi ni sawa na ibada? Umesoma mpaka hatua ipi ya elimu mkuu?

Kwa taarifa yako tu; hatuna sala ya hivyo. Fanya utafiti kabla ya kuja kutuhumu. JF is becoming a home of stupids.

Mathayo 18:18

Inasikitisha na ni aibu pia kwamba Ukatoliki unafundisha kinyume na hilo Neno.

👉Lakini Yeye [Kristu] alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika. Luka 11:28
Nina uhakika haujui chochote kuhusu Ukatoliki.


NB: Ukatoliki mnaouhangaikia na mnaoufahamu ni tofauti na Ukatoliki wetu... Kanisa pekee lililoanzishwa na Kristu.
 
Haujui chochote kuhusu Ukatoliki.
 
Bora kuhamia RC maana huko hakuna dhambi.
 
Waumini wa kikatoliki wa afrika achaneni na ukatoliki anzisheni makanisa yenu yenye maadili. Mtaaibika na kufedheheshwa na kiongozi wenu huyo mkuu mwenye mamlaka makubwa kanisani. Mtaburuzwa sana na kuonekana nanyi ni wahuni tu na hamna Mungu
shida maokoto...........mapadre wengi wanalishwa na hao wazungu
 
Baadhi ya waumini nao wana mawazo mgando, hawabadiliki.
 
Huyu Papa ni FreeMason Mkubwa duniani anakubali madhambi ambayo Mungu ameyakataza katika vitabu vyake vitakatifu? Huyu Papa ni mpinga amri za Mungu amelaanika kweli.
 
Hatuabudu sanamu, hatujawahi kuabudu sanamu na kamwe hatutakuja kuabudu sanamu.
Kukana tu kwa maneno hakusaidii kuondoa ukweli ulio wazi kwamba Ukatoliki unasujudia na kuabudu sanamu ambazo Biblia imepiga marufuku mara nyingi sana, na kwa maneno makali kadiri iwezekanavyo.

👉 [3] Usiwe na miungu mingine ila Mimi.

👉 [4] Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.

👉 [5] Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa Mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, ~ Kutoka 20

👉Isaya 44:9-20

Tunamuabudu Mungu. Tunamuabudu asiyeonekana kupitia vielelezo vinavyoonekana kama wana wa Israel walivyofanya kupitia nyoka wa shaba (Rejea Hesabu 21:8).
Kama ilivyoelezwa katika Kutoka 20 (hapo juu) Maandiko yamekataza kabisa KUJIFANYIA SANAMU ZA KUCHONGA, KUZISUJUDIA na KUZITUMIKIA.

Ukatoliki utambue kwamba umejifanyia sanamu hizo za kuchonga, na hiyo, kwa mujibu wa Biblia, ni ibada ya sanamu.

Kitendo chao cha kuzisujudia, kuzibusu, kuzikumbatia katika utashi wa kiroho, hiyo ni ibada ya sanamu.

Kitendo chao cha kuzihudumia, kuzipa heshima na umuhimu na umaana wowote wa kiroho, huko ni kuzitumikia. Biblia inataja suala hilo kuwa ni ibada ya sanamu.

Kumhusu nyoka wa shaba, Biblia imefafanua kikamilifu kwenye Injili ya Yohana: 3:

👉[14] Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa;

[15] ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye.

Biblia haijasema sanamu ziinuliwe, bali Mwana wa Adamu (Yesu Kristu), ndiye apewe nafasi ya kuinuliwa na kutukuzwa mioyoni na maishani mwetu.
Kuombea wafu ni sawa na kuabudu wafu? Kwamba ombi ni sawa na ibada?
Ukatoliki unamwomba ^Bikra^ Maria. Hilo liko wazi kwenye ibada zao.

Hiyo siyo tu kwamba ni ibada ya wafu, lakini pia ni ibada ya sanamu.

Ukatoliki unaabudu mizimu, kwa sababu Mariamu, mamaye Yesu alikufa, akazikwa na hakuna kumbukumbu yoyote ya Biblia kwamba alifufuka na kupaa mbinguni.

Ukatoliki unaabudu miungu kwa sababu hata kama Mariamu angelikuwa hai mbinguni, bado hana sifa za kuombwa dua na kuabudiwa kama wafanyavyo Wakatoliki.

👉Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. ~Matendo 4:12

Kama hakuna wokovu kwa mwingine awaye yote mbali na Kristu, kwa mujibu wa Biblia, sasa mahangaiko ni ya nini kwa Wakatoliki juu ya Mariamu, tena mtu ambaye ni mfu???

Maana yake, Ukatoliki umemgeuza Mariamu kuwa mungu wao, kwamba hajafa na kwamba anao uwezo wa kuwasaidia na kuwaokoa. Vinginevyo wasingethubutu kabisa kumwomba! Ibada ya sanamu!!!
Kwa taarifa yako tu; hatuna sala ya hivyo. Fanya utafiti kabla ya kuja kutuhumu.
Sala ya ^Bikra^ Maria ni uthibitisho mkubwa mojawapo kwamba Ukatoliki unaabudu mizimu na ibada ya sanamu. Hii ni kinyume kabisa na Maandiko Matakatifu ambayo ndiyo msingi mkuu wa Ukristu.

Mathayo 18:18
Ni wapi ambapo padre ametajwa katika andiko hili la Mathayo 18?

Katika agano jipya, baada ya kifo cha Yesu Msalabani, waumini wote wanahesabika kama makuhani wa Mungu.

👉Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu. ~1 Petro 2:9

Mfumo wa Agano la Kale wa ukuhani ambapo wana wa Israeli walipaswa kwenda kwa kuhani kwenye hema takatifu, maskani au hekaluni, wakiwa na dhabihu zao, ulikuwa kielelezo cha kumwakilisha Masihi Kristu ajaye.

Mfumo huo ulikoma baada ya kifo cha Yesu, ndiyo maana wakati Kristu akikata roho, pazia la hekalu lilipasuka vipande (Mathayo 27:50, 51), ikiashiria kwamb huduma hiyo sasa haina maana, kwa vile imetimia na kutimilika katika Kristu.

Mambo hayo yalikuwa ^kivuli cha mambo yajayo^ -- yaani yalilenga kwa Kristu Yesu (Kolosai 2:17).
Nina uhakika haujui chochote kuhusu Ukatoliki.
???🤔🤔🤔

NB: Ukatoliki mnaouhangaikia na mnaoufahamu ni tofauti na Ukatoliki wetu.
Ukatoliki tunaoupinga kwa nguvu zote ni ule ambao:
👉unafundisha kwamba papa ndiye mwenye mamlaka juu ya Ukristu duniani -- yaani ndiye kaimu wa Mungu.

👉unadai Mtume Petro ndiye papa wa kwanza na kwamba mapapa wote wamerithi na wanarithi mamlaka yao kutoka kwake.

👉unadai kwamba mapokeo ya kanisa na mafundisho ya maaskofu wao na miongozo ya mabaraza iko sambamba na Biblia kimamlaka.

👉unafundisha kwamba ubatizo siyo lazima kuzamisha majini, hata kunyunyiza ni sawa.

👉unadai kwamba katika huduma takatifu ya Meza ya Bwana, vielelezo vya mkate na divai hugeuka kuwa mwili na damu halisi ya Kristu.

👉unafundisha kwamba Maria, mlolongo wa watakatifu, hata waliokwishakufa tayari, wanachangia katika wokovu wetu, kwa kuombwa dua.

👉unafundisha fundisho potofu la toharani ama pagatoria, kwamba ni mahali pa mateso ya utakaso kwa muda kwa ajili ya waumini ambao si waovu sana kiasi cha kwenda jehanum na wala si wema vya kutosha kuingia mbinguni.

👉unafundisha kwamba una mamlaka ya kubadilisha na kubatilisha Maandiko Matakatifu kama upendavyo wenyewe.

👉unafundisha kwamba wokovu haupatikani kwa neema bali kwa matendo; kwamba kipimo cha wokovu ni kwamba tu matendo ya wema yazidi yale maovu; kwamba kadiri muumini anavyojitesa, anavyotoa pesa, juhudi na mali kumtumikia Mungu na kanisa, kadiri anavyofanya huduma na ibada, nk ndivyo anavyo anahesabiwa haki machoni pa Mungu. Ndiyo maana Ukatoliki na Uislamu ni mapacha na mapapa wawili wanaofanana.

👉unafundisha kuchonga, kusujudia, na kutumikia sanamu kwa kisingizio kwamba unatumia kama vielelezo tu vya ibada.

👉Kama mambo haya na mengine mengi yanayofanana nayo ni tofauti na Ukatoliki wenu, basi una haki ya kukaa pembeni, maana wewe hauhusiki hapo.

Kanisa pekee lililoanzishwa na Kristu.
👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu Kristu kwao hatoshelezi kwa wokovu, lazima asaidiwe na akina Maria na watakatifu wengine.

👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu unapingana waziwazi na Maandiko Matakatifu.

👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu umepoka mamlaka ya Kristu, na papa kujiweka kama mungu duniani.

👉Kamwe Ukatoliki hauwezi kuwa Kanisa la Mungu kwa sababu historia ya matendo yake, mauaji ya Wakritu uliyoyafanya, ukatili wake katika nyakati zote vinapingana kabisa na Ukristu.

👉Ni sahihi 100% kusema kwamba Ukatoliki ni wakala wa Shetani duniani, ambaye hujificha kwenye vazi la Ukristu na utu wema.

👉Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. ~ Mathayo 7:15

👉Wito wa Mungu kwa waumini na Wakristu wote, hata wale waliomo kwenye jumuia ya imani potofu ya Ukatoliki:👇

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake. ~Ufunuo wa Yohana 18:4, 5
 
 

Attachments

  • IMG_20231109_231209.jpg
    124.7 KB · Views: 6
Msimamo wa Papa Francis nauelewa vizuri sana, hayupo mwenye dhambi anayetakiwa kutengwa, hata Yesu Kristu hakuja duniani kwa ajili ya wenye haki, alikuja kwa wenye dhambi ili wapate kuokoka.

Huyo bishop aliyesimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi angetakiwa kutuambia, mtu mwenye dhambi ukishamtenga utakuwa umemsaidiaje kuachana na hiyo dhambi yake? atuambie ni biblia ipi iliyomfundisha hivyo?

Kuliko kujitetea kwa kusema tu hayo mambo ya ushoga yanaharibu nature, nature haiwezi kuharibiwa kwa sababu ya mambo yanayofanywa na wawili waliopotoka, nature inaharibiwa kama hiyo tabia ndio itageuka mfumo rasmi wa kukutana na mwenza duniani kote, jambo ambalo kiuhalisia haliko hivyo.

Siku zote mwenye dhambi sio wa kumnyooshea kidole na kumhukumu, ni wa kumuombea abadilike, ndio maana maandiko yanasema usihukumu ili nawe usije hukumiwa, huyo bishop anaonekana kabisa amepanic.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
miaka 12 ndani ya JF ila bado uandishi wako unakuwa na walakini mkubwa sana..

Hebu jitafakari mkuu unaweza kuwa na taarifa nzuri ila uwasilishaji ukawa mbovu mbovu tu.
Sina hakika humu ndani tunafundishwa kuandika
 
Msimamo wa Papa Francis nauelewa vizuri sana, hayupo mwenye dhambi anayetakiwa kutengwa, hata Yesu Kristu hakuja duniani kwa ajili ya wenye haki, alikuja kwa wenye dhambi ili wapate kuokoka...
Ndiyo maana wezi hawaishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…