Papa Francis amuunga mkono Mpinga Kristo

Papa Francis amuunga mkono Mpinga Kristo

Mimi namuhitaji roho mtakatifu ndio maana nimeuliza. Nataka namna ya kumpata.
 
Mpumbavuuu anapojaribu kuzungumzia Sayansi na conspiracy za kijima inatia kinyaa! Ni aibu uzi huu umewekwa jukwaa la intelejensia!
hivi ndugu yangu ni lini utaukimbia ukweli? nakushauri usome Biblia Takatifu na umwombe Mungu akufunue akili kabla hujachelewa maana huhitaji kuweka kidole kwenye moto ukibisha kuwa hauunguzi
 
Ukweli upi ndugu..? Porojo za mitandaoni ambao kila mtu anaweza andika...??

Hebu nikuulize ni lini alisema hayo? Alimsapoti mtu gani..? Nani alikwambia micro-chip ni alama ya mpinga Kristo ? Hii umetolea wapi..?

Halafu mbona kitabu cha apocylpse cha Yohana hakiongelei mambo hayo..? Huu upuuzi umeutolea wapi..??

Tatu wewe ni dhehebu gani..?
Ufunuo wa Yohana waelezea kila kitu. Muombe Mwenyezi Mungu kabla hujakisoma ili akufunue akili haya yote yapo humo
 
Hayo ni maelezo ya jumla. Hiyo biblia mnasema huwezi kuielewa bila roho mtakatifu. Na wewe unasema asome biblia bila kusema roho mtakatifu anampataje.
 
Mleta mada ni Msabato. Wao ndiyo hujifanya kuwa wanafahamu mambo ya unabii sana na ni wafafanuzi wakubwa wa vitabu vya Ufunuo na Daniel. Kanisa zima lilianzishwa kutokana na vuguvugu la kutabiri kurejea kwa Yesu kule Marekani. Baada ya utabiri huo kushindikana na Yesu kutorejea hasa mwaka 1844, walikokotoa mahesabu ya kitabu cha Daniel upya wakatabiri tena wakashindwa. Tangu hapo Kanisa hili halijaachana na mambo ya unabii, kutabiri tabiri na conspiracy theories. Kila tukio jipya liwe natural au la hupitishwa katika chekecho la unabii; na unabii wa vitabu vya Daniel na Ufunuo ndiyo central theme.

Papa ni mtu wa muhimu sana kwa Waadventista Wasabato. Wanaamini kuwa Pope ndiye mpinga Kristo na mmiliki wa ile namba tata 666 na kwamba siku za mwisho kanisa katoliki litarudia hadhi yake liliyokuwa nayo hapo zamani wakati ule likitawala dunia na kuwapitishia hukumu za kifo akina Galileo Galilei. Wanaamini kuwa wao pekee ndiyo washika amri sahihi za Mungu na ndiyo pekee watakaokwenda mbinguni. Na wale wahafidhina hawali nyama, kunywa kahawa au chai, samaki wasio na magamba, wanyama wasio na kwato na sheria nyingine za Kumbukumbu la Torati hasa zinazohusu siku ya Sabato. Siku ya Sabato hawaruhusiwi hata kupika! Kwa hiyo wokovu unafungamanishwa na sheria hizi za Musa jambo ambalo linapingwa na Wakristo wengi (Damu ya Yesu ndiyo ilimaliza kila kitu msalabani na mtu hataikosa mbingu eti tu kwa vila alikula samaki asiye na magamba!)

Wanatheolojia wengi na wachambuzi wa Biblia huwachukulia Wasabato kama aina mojawapo ya cult za Kikristo zilizofanikiwa sana. Badala ya kuamini Biblia pekee, wanaamini pia maandishi mengi (karibia vitabu 600) vya mama mmoja Mmarekani aitwaye Ellen G. White. Huyu wanamtambua kama nabii wao na baadhi ya vitabu vyake kama Pambano Kuu (The Great Controversy) vina hadhi kubwa sana kanisani. Pia wanaamini kuwa Yesu hakumaliza kazi ya kutukomboa msalabani bali kuanzia mwaka 1884 aliingia Patakatifu pa Patakatifu (Holly of Hollies) huko mbinguni ili kuendelea kututetea mbele ya Mungu Baba kuhusu dhambi zetu tunazoendelea kuzitenda hapa duniani.

Ova!

hakuna ajuaye siku ya kurudi kwa YESU KRISTO ila Mwenyezi Mungu mwenyewe. Binadamu ni nani hata aweze kuijua?

pili, njia pekee ya kukamilika kiimani Kikristo ni kupitia BIBLIA TAKATIFU pekee na ndio chanzo cha waprotestant kujitenga na Kanisa la Roma ambalo linafundisha kuwa Pope ndie aliye "infallible"

tatu, unachokisema kimepotoka ndugu. nakushauri ukisome kitabu cha Ellen White "Tumaini Kuu" ili uone essence ya kitabu chake ni nini maana umekitaja as if ni biblia.

nne, fatilia kisa cha Luther mpaka kuja kuuwawa kwake halafu uje uniambie nani alikuwa mpinga kristo kama sio Pope Gregory VII na wenzake. walikuwa wanatoa "vyeti vya msamaha wa dhambi" as if wao ndo wenye authority ya kusamehe dhambi

tano, Fatilia chanzo cha French revolution 1789 na "Guillotine." na kisa cha watu kuchomwa moto hai katika kipindi hiko

na leo Pope anaidhinisha "microchip" mwenye kuelewa na aelewe ila nashauri watu walinganishe statement ya Pope na maandiko ya Biblia kwenye Ufunuo wa Yohana kabla ya kuja kumbishia mleta uzi.
 
Daah....Umemaliza hata Darasa la saba ndugu..?

Fanya hima umalize hata shule ya msingi bana...Usipende kushinda kwenye lessoni na kula kande siku ya Sabato..Kande hudumaza ubongo ujue!
USIBISHE USILOKUWA NA UHAKIKA NALO.. KISA CHA POPE GROGORY VII NA WALIOMFUATIA KUAGIZA LUTHER NA WAFUASI WAKE WACHOMWE MOTO WANGALI HAI NI NINI?
 
mmmh mi najua kila mtu na imani yake. Mkiaza kugusa masuala ya kiimani hapa mtaishia kugombana bure.
 
Hakuna Mpinga kristo mwenye namba 666. Kristo kama Mungu alishapingwa zamani sana. Kristo kama Yesu na binadamu yupo lakini kama Mungu alipingwa zamani sana. Dunia imegawanyika nusu kwa hali
 
Inamaana hujui kuwa papa ni agent wa anti-Christ?@Chemtrail
Sijui umeishia darasa la ngapi bt huwa naamini kuwa mtu yeyote member wa jf 99% atlest amemaliza kidato cha nne, pia naamini kwa elimu hiyo unaweza kufanya reasoning , hata kama ukishindwa basi google ipo.

Hivi kanisa lililohusika kukusanya vitabu , kujadiliana kitabu gani kiingie na kipi kibaki, leo unadai ni Ant- crist !!!

Unajua kuhusu Injili ya Maria Magdalena?
Unajua kuhusu injili ya Juda.
Unajua hata mgogoro wa deutrocanon books!?

How pathec are YOU!!!!!!!!
 
Bila shaka wewe ni msabato, maana mna shida sana, mnaishi kwa ndoto za kipumbafu muda wote.
 
Hon

Hongera sana, inabidi tuwasaidie walioko huko wa-come back to their senses, they have a very limited time left.
amini amini nawaambia your sailing in the same sinking boat.
 
Ukweli upi ndugu..? Porojo za mitandaoni ambao kila mtu anaweza andika...??

Hebu nikuulize ni lini alisema hayo? Alimsapoti mtu gani..? Nani alikwambia micro-chip ni alama ya mpinga Kristo ? Hii umetolea wapi..?

Halafu mbona kitabu cha apocylpse cha Yohana hakiongelei mambo hayo..? Huu upuuzi umeutolea wapi..??

Tatu wewe ni dhehebu gani..?
Mkuu, hawa watu wanapaswa kuonewa huruma. Wana ujinga mkubwa juu ya uelewa wa maandiko matakatifu hasa hiyo namba 666
 
Katika hali ya kushangaza, Papa Francis amejitokeza hadharani kuunga mkono matumizi ya vichipu vya RFID, yaani Radio Frequency Identification kwa wanadamu. Amesema tekinolojia hii inaleta matumaini makubwa katika kutatua matatizo mengi ya wanadamu na hivyo kuboresha ustawi wao.

Matamshi haya yanakuja huku akijua msimamo wa kiimani wa makanisa mengi ya Kikristo na hata kanisa Katoliki lenyewe. Makanisa mengi ya kikristo yanaamini kwamba RFID chipping ni alama ya mnyama au Shetani kama ilivyoelezwa katika kitabu cha Ufunuo. Tukio hili kufuatana na imani ya makanisa haya, linaashiria mwisho wa dunia.

Katika kitabu cha Ufunuo13 msitari wa 16-18 tunasoma maneno haya, 16Naye alimlazimisha kila mtu, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea chapa katika mkono wake wa kulia au paji la uso, 17 ili kila mtu asiweze kununua au kuuza mpaka awe na hiyo chapa, ambalo ndilo jina la huyo mnyama au namba ya jina lake. 18 Hii inahitaji hekima, kama mtu ana ufahamu aitafute namba ya huyo mnyama, kwa sababu ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.

Kwa wale wachunguzi watakubaliana na mimi kwamba namba hii inatumika sana siku hizi.Wapo ambao wanaitumia kwa uwazi kwenye bidhaa. Wanamuziki wa Rock hasa nchi za Ulaya na Marekani nao wanaitumia sana, lakini wengi wanatumia kwa siri, kwa hiyo inahitaji umakini mkubwa kuweza kujua kwamba ni 666. Hata logo ya Olympic ina namba 666. Matumizi ya namba hii kwenye barcodes ni wazi kidogo!

Katika hotuba yake ya kila wiki Vatican, Papa alizungumzia juu ya imani aliyonayo kwenye tekinolojia ya RFID. Aliwahakikishia waumini wake kwamba hakuna athari zozote za kiroho au kiafya zinazoweza kutokana na matumizi ya vichipu vya RFID. Hata hivyo inafahamika kwamba yapo matatizo makubwa ya kiafya yanayoweza kutokana na matumizi ya vichipu vya RFID vinapochoka, ikiwa ni pamoja na maumivu makali mwilini na majipu mwili mzima.

Aliendelea kwa kusema wamechunguza maandiko vizuri na hivyo wanaweza kusema kwamba hakuna ushahidi wowote unao-onyesha kwamba vichipu vya RFID ambacho kinawekwa mwilini kina muwakilisha Shetani. Nadhani alisahau Ufunuo 13:16-18! Aliongeza kusema RFID ni baraka kutoka kwa Mungu mwenyewe ambayo ameileta kwa wanadamu.

Aliwaomba wauminu wa Kanisa Katoliki waipokee baraka hii kwa moyo mmoja. Alimalizia kwa kusema kuanzia sasa itakuwa lazima kwa kila mfanyikazi wa Vatican kuwekewa kichipu cha RFID.

Kusoma zaidi:Google "Pope Francis goes public in support of RFID implantation. "

Kama jina la chip lilivyo' Radio Frequency Identification device' ni kifaa cha utambulisho tu na hakina uhusiano na Biblia. wanaoamini mambo kama hayo ni washirikina kama wale wananchi wa Dodoma waliowaua watafiti wa kilimo na kuwachoma moto. Kanisa Katoliki pia lina wasomi waliobobea na wanasayansi, kwa hiyo haliwezi kushiriki katika kuwapotosha waumini wake. Hayo mambo yako kwenye makanisa ya MIUJIZA ambayo yamepotosha watu wengi kwa kuchezea hisia na matatizo yao ya maisha.
Maagizo yote ya Kanisa Katoliki ama yako kwenye Cannon Law au kwa Waraka wa Papa kwa Maaskofu wote.
 
Imeandikwa, "..watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.."
The issue watu wenye kuamini Dini kwa uoga always huchanganya madesa... The issue Mpinga kristo haihusiani na kukosa maarifa ili kutoangamia na solution za bible za kuepukana na majanga ni kujenga juu ya mwamba imara ukiumwa na nyoka uitizame sanamu ya nyoka same kama ile nembo Muhimbili hospital... Kula vyakula vilivyokatazwa kwenye agano la kale zaidi angalizo lipo kwenye ufunuo.. Sasa ikija volcano mnakufa kimbunga mnakufa mvua mnakufa,jua mnakufa,baharini mnakufa angani mnakufa... Maalifa labda kwenda Mars au Jupiter....

Historia inaonesha Mpinga kristo ilikuwa ni serikali ya Roma miaka ya Yesu kwani alitabiliwa ndie atakuwa mfalme Wa wayahudi so walihakikisha anaishi bila Amani na ndio ilivyokuwa siku ya uchungu ilibidi azaliwe zizini asiuliwe akiwa kichanga,and then akatoroshwa Egypt hadi Roman walipojiridhisha watoto wote wameuawa akarejeshwa baada ya miaka kadhaa... And then alipotimiza miaka 12 akasepa ughaibuni nchi za Iraq Uturuki hadi uchina masomoni akarejea alipofikisha miaka 30 akaishi kidogo Wa Roma wakamtight akamalizwa ila yasemekana Wanafunzi wake wakamuiba akiwa amezirai wakamtibu na dawa kali sana ya manemane akazinduka na aliwaaga akapanda mlima akateremkia upande Wa pili akasafiri huko uturuki hadi India mji uitwao Kashmir na ndipo kaburi lake lipo hadi leo hii fika huko utapata historia yake na huko uchina Tibet chuo kikuu Kuna signature zake na alikuwa msomi haswa...
 
Back
Top Bottom