Kama hii habari ni ya kweli, naunga mkono alichosema huyo papa.
Labda tu niweke sawa, namuunga mkono si kwa sababu ya kuhusianisha swala hili na dini, lakini kwa sababu amezungumza swala ambalo ni dhahiri kwa macho ya kawaida bila hata kutumia biblia kuhalalisha.
Watu wazima walioridhia kufirana wenyewe vyumbani mwao, kwanini wawe ni swala linalohitaji kuwa tatizo la jamii nzima?
Watu wasifanywe ama wasifanyike kuwa wahanga (victimized) kwa sababu tu ya nani wanampenda au nani wanalala naye kitandani. Sio swala la jamii, ni swala binafsi.
Hayo mengine ya biblia mimi sijui. Hayanihusu sana.