Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Yesu alipanguswa miguu kwa nywele na Kahraba, akashiriki chakula na mtoza ushuru, serikali ya Kirumi ilimind pia sana, kama ambavyo waprotestanti na waisilamu wanavyoshangaa afanyacho Papa
Dini ipo kwaajili ya kuokoa wapotevu
 
Ushoga ndio dhambi pekee?

Je shoga anatakiwa atengwe na jamii?

Hata tusiende mbali kwenye familia kukiwa na shoga anatengwa au kuuwawa?

Dini zote zinatupokea bila kujali udhaifu na dhambi zetu kwa nini ushoga ndio inaonekana haifai?vipi kuhusu wizi,ukahaba,uuaji,ufisadi na kadhalika?hizo sio dhambi

Nafikiri ifike pahala kazi ya kuhukumu aachiwe Mungu kama binadamu tuishi tu kwa kuvumiliana na kuchukuliana.
Wabongo unafikii unawasumbua.
 
Hakuna sehemu Papa alisema sio dhambi soma hii nukuu hapa[emoji116]

Ingawa Francis alikosoa kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja, aliweka wazi kuwa anaamini kuwa vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ni dhambi. "Hebu tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu," Papa alisema.
Asipo kuelewa hapa, haelewi tena.
 
Ukristo ni ushetani, hivi sodoma na gomora ipo wapi na ni mji wa kikristo ama upi maana ushakithiri kwa ushoga karne kadhaa huko nyuma hafi ukachomwa
Sasa huu ushoga mpyaa umekujaje na uliteketezwa kwa motoo hapo zaman
 
Sio wezi tu hata wauwaji wanapata huduma za kiroho ila ndio huwezi kujua kuwa huyu ni muuwaji. Mkuu mie nimetoa ushauri kwamba kama mashoga wanaona jamii inawabagua na wakati wao wanaona suala la dini ni muhimu kwao basi waanzishe dini yao ambayo itahalalisha ushoga na kuwa kitu cha kawaida na hapo watapokea huduma za kiroho kwa raha kabisa kuliko kuangaika kulazimisha jamii ichukulie ushoga ni kitu cha kawaida kama vitu vyengine.
Ndo Papa ameshasema na kila anayetaka kwenda tofauti na yeye ana mfurusha.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwanza kabisa Papa ameweka mbele swala la maslahi katika kanisa hili, lengo la yeye kuchukua uamuzi huu anataka kanisa liwe na idadi kubwa ya waumini pasipokujali tabia na mienendo ya waumini wake akilenga kuwa atakayewahukumu ni Mungu pekee yeye hataki kujihusisha na swala la hukumu hilo ndilo lengo lake.........................................................ameshindwa kuhukumu ila ameweza kuwabariki hongereni wabarikiwa
Kanisa la mashoga ,Roman katholiki na papa shoga
 
Kama hukumu yao ni kuuawa utaua wangapi? Je wale wazazi waliowazaa hao mashoga utawaacha kwenye hali gani baada ya kuwanyonga. Manake wazazi wa hawa mashoga wanamaumivu kama ya kuuguza mgonjwa nafikiri ungewaza namna ya kusaidia na sio kuhukumu
Ua wote hadi papa
 
Mkuu kipaumbele cha kikatoliki ni kanisa kujaa bila kujali tabia za waumini? Mnasali na wezi na mambo mnaona fresh tu?
Kabla papa hajaruhusu tambua kuwa mashoga walikuwa ndani ya kanisa katoliki lakini anachofanya ni kuunga mkono matendo yao, ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
Kwa hiyo kanisa linaacha sheria ya Yesu na kufuata mapendezi ya watu wengi hata kama ni kinyume cha sheria ya Yesu?
Katoliki siyo kanisa ni ushetani
 
Uafanuzi kuhusiana na uamuzi wa Papa Fransis kuwakaribisha wapenzi wa jinsia moja katika kanisa Katoliki.

Watu wengi duniani hasa dini ya Kiislamu, Wahindu na wengineo wamekuwa wakituhumu Imani ya Kikristo pamoja na kiongozi wetu Papa Fransis kana kwamba dini zao zinawaumini Watakatifu pekee jambo ambalo linaweza kuleta picha ya aibu na fedheha katika imani yetu kwa baadhi ya waumini wengine.

Wapo walioenda mbali na kusema Papa Fransis na Imani ya Kikristo inajihusisha na Ushetani.

Kwanza kabisa Papa ameweka mbele swala la maslahi katika kanisa hili, lengo la yeye kuchukua uamuzi huu anataka kanisa liwe na idadi kubwa ya waumini pasipokujali tabia na mienendo ya waumini wake akilenga kuwa atakayewahukumu ni Mungu pekee yeye hataki kujihusisha na swala la hukumu hilo ndilo lengo lake.

Kawaida binadamu anapokuwa akihitaji wafuasi wengi hatabagua wezi, wavivu, washirikina na wengineo, dhamira yake italenga kuwa na idadi kubwa ya wafuasi.

Kwahiyo Papa Fransis haenezi ushetani kama watu wanavyomtuhumu na wala Wakristo tusionee aibu imani yetu.

Papa hataki kujihusisha kwenye hukumu ya wakosefu anataka Mungu awahukumu yeye mwenyewe, dhamira yake ni kuhakikisha kanisa linapata wafuasi wengi pasipokujali mienendo na tabia za waumini wake.

Swala la hukumu ni jambo gumu sana duniani ndio maana watu wanamwachia Mungu.

Nadhani amefikiri mara kadhaa kuhukumu waumini wa Kanisa Katoliki akashindwa pengine ameona kuwa akianza kutoa hukumu itabidi achanganye wote wakiwemo wezi, walevi, wavivu, washirikina, mafisadi, makahaba, wanyang'anyi, walawiti na wengineo.

Katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusiana na ubaguzi alitoa mfano akasema kuwa nchi ya Tanzania imejengwa na makabila tofauti haikujengwa na kabila moja, madhara ya ubaguzi katika nchi ya Tanzania ni kuwa tukianza kuwaondoa Wazanzibari tukamaliza wote, tutajikuta Wazaramo wamebaki tutawaondoa tena wote, tukimaliza Wazaramo tutakuta kuna Wachaga tutaondoa wote tukimaliza tutagundua kuna Wahaya halikadhalika.

Kwahiyo Papa ameona kuwa Kanisa Katoliki limejengwa na waumini wema na wabaya halikujengwa na Watakatifu pekee akianza kuondoa walawiti akamaliza atajikuta wezi wapo ataondoa atamaliza, atajikuta washirikina wapo halikadhalika kwahiyo hatabakiwa na waumini Watakatifu pekee.

Ndugu zangu tuzungumze kwa uwazi kuhusiana na uamuzi wa Papa Francis kuwapa mashoga uhuru.

Wakosoaji wakubwa wa uamuzi huu ni madhehebu mengine yasiyo ya Katholiki huku wakidai kuwa dini ya Katholiki inaruhusu ushoga.

Kabla ya kumtuhumu Papa ni kuwa idadi ya mashoga duniani imeongezeka sana kiasi kwamba inatishia idadi ya wale wasio mashoga.

Takwimu alizopokea Papa zimemfikirisha mara kadhaa na kuona kuwa endapo akiwatenga mashoga basi atabaki na idadi ndogo sana ya waumini wa Katholiki, ili kuzuia anguko hilo akaona awaruhusu mashoga kuwa waumini wa kanisa la Katholiki.

Wenzangu wa madhehebu mengine wakiwemo Waislamu, Wahindu na wengineo, mnapomnyooshea kidole Papa mnamaanisha kuwa hakuna muumini wetu hata mmoja duniani ambaye ni shoga.

Swali la kujiuliza, je katika dhehebu lako hakuna muumini wenu hata mmoja duniani ambaye ni shoga?

Turejelee msemo wa kuwa kabla hujatoa boliti katika jicho la mwenzako basi hakikisha katika jicho lako umekwishatoa!
Kwenye mada yako tenganisha ukristo na ukatoliki, kama wakatoliki mmeamua kuvutia mashoga ili muwe wengi duniani basi rekebisha contents za andiko lako.
Wakatoliki na kiongozi wenu papa ndo mmeruhusu ushoga kwenye madhehehu yenu siyo Wakristo.
 
Kama mtoto wa jirani yako ni mwizi basi kabla hujamnyooshea kidole hakikisha wako sio mwizi
Wahalifu wapo kila sehemu, ila hawaruhusiwi. Ndo maana wanapingwa na wakijulikana wana adhibiwa. Na mashoga ni wahalifu Sasa kama wakatoliki mmeruhusu kufirn haina maana huko kwingine hawapo, wapo ila hawajaruhusiwa na wanahama na kuja huko mnako ruhusu.
 
Back
Top Bottom