Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Hoja yako haina mashiko hata kidogo, ndoa za jinsia zimepigwa marufuku kwenye maandiko matakatifu BIBLIA hakuna namna ya kuhalalisha huo ushetani,
Hilo suala la ndoa limetoka wapi? Hebu tusiwe na vichwa vizito kusoma, kufikiri na kuelewa. Ushoga unalizimisha uwepo wa ndoa?
 
Wapi imeandikwa ndoa? Kuwa shoga kunahitaji ndoa? Watu wengi humu huwa hawajui mada za nyuzi, nimeona hilo mara nyingi
nadhani ndoa huwa ni baraka na kubarikiwa sasa baraka za jinsia moja ni kitugani na baraka hapo ni ya nini kweli mashetani na wafuasi wao
 
nadhani ndoa huwa ni baraka na kubarikiwa sasa baraka za jinsia moja ni kitugani na baraka hapo ni ya nini kweli mashetani na wafuasi wao
Afadhali sasa umesema 'unadhani'. Basi tulia vizuri ili uelewe badala ya kutumia dhahania. Kuwabatiza, kuwapa sakramenti nyingine mashigo ni kuwabariki na kuwakaribisha katika familia ya Mungu, tatizo watu tumekariri ngono. Halafu mbona inaekeweka, hivi mwizi amewahi kupigwa marufuku kurudi katika njia sahihi kupitia kanisa? Wasema ungo je? Wauaji je? Kwa nini mashoga inachukuliwa kama dhambi maalum?
 
Afadhali sasa umesema 'unadhani'. Basi tulia vizuri ili uelewe badala ya kutumia dhahania. Kuwabatiza, kuwapa sakramenti nyingine mashigo ni kuwabariki na kuwakaribisha katika familia ya Mungu, tatizo watu tumekariri ngono. Halafu mbona inaekeweka, hivi mwizi amewahi kupigwa marufuku kurudi katika njia sahihi kupitia kanisa? Wasema ungo je? Wauaji je? Kwa nini mashoga inachukuliwa kama dhambi maalum?
hapana sio dhambi maana mushabarikiwa hongereni sana
 
Uafanuzi kuhusiana na uamuzi wa Papa Fransis kuwakaribisha wapenzi wa jinsia moja katika kanisa Katoliki

Watu wengi duniani hasa dini ya Kiislamu, Wahindu na wengineo wamekuwa wakituhumu Imani ya Kikristo pamoja na kiongozi wetu Papa Fransis kana kwamba dini zao zinawaumini Watakatifu pekee jambo ambalo linaweza kuleta picha ya aibu na fedheha katika imani yetu kwa baadhi ya waumini wengine

Wapo walioenda mbali na kusema Papa Fransis na Imani ya Kikristo inajihusisha na Ushetani

Kwanza kabisa Papa ameweka mbele swala la maslahi katika kanisa hili, lengo la yeye kuchukua uamuzi huu anataka kanisa liwe na idadi kubwa ya waumini pasipokujali tabia na mienendo ya waumini wake akilenga kuwa atakayewahukumu ni Mungu pekee yeye hataki kujihusisha na swala la hukumu hilo ndilo lengo lake

Kawaida binadamu anapokuwa akihitaji wafuasi wengi hatabagua wezi, wavivu, washirikina na wengineo, dhamira yake italenga kuwa na idadi kubwa ya wafuasi

Kwahiyo Papa Fransis haenezi ushetani kama watu wanavyomtuhumu na wala Wakristo tusionee aibu imani yetu

Papa hataki kujihusisha kwenye hukumu ya wakosefu anataka Mungu awahukumu yeye mwenyewe, dhamira yake ni kuhakikisha kanisa linapata wafuasi wengi pasipokujali mienendo na tabia za waumini wake

Swala la hukumu ni jambo gumu sana duniani ndio maana watu wanamwachia Mungu

Nadhani amefikiri mara kadhaa kuhukumu waumini wa Kanisa Katoliki akashindwa pengine ameona kuwa akianza kutoa hukumu itabidi achanganye wote wakiwemo wezi, walevi, wavivu, washirikina, mafisadi, makahaba, wanyang'anyi, walawiti na wengineo

Katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusiana na ubaguzi alitoa mfano akasema kuwa nchi ya Tanzania imejengwa na makabila tofauti haikujengwa na kabila moja, madhara ya ubaguzi katika nchi ya Tanzania ni kuwa tukianza kuwaondoa Wazanzibari tukamaliza wote, tutajikuta Wazaramo wamebaki tutawaondoa tena wote, tukimaliza Wazaramo tutakuta kuna Wachaga tutaondoa wote tukimaliza tutagundua kuna Wahaya halikadhalika

Kwahiyo Papa ameona kuwa Kanisa Katoliki limejengwa na waumini wema na wabaya halikujengwa na Watakatifu pekee akianza kuondoa walawiti akamaliza atajikuta wezi wapo ataondoa atamaliza, atajikuta washirikina wapo halikadhalika kwahiyo hatabakiwa na waumini Watakatifu pekee

Ndugu zangu tuzungumze kwa uwazi kuhusiana na uamuzi wa Papa Francis kuwapa mashoga uhuru

Wakosoaji wakubwa wa uamuzi huu ni madhehebu mengine yasiyo ya Katholiki huku wakidai kuwa dini ya Katholiki inaruhusu ushoga

Kabla ya kumtuhumu Papa ni kuwa idadi ya mashoga duniani imeongezeka sana kiasi kwamba inatishia idadi ya wale wasio mashoga.

Takwimu alizopokea Papa zimemfikirisha mara kadhaa na kuona kuwa endapo akiwatenga mashoga basi atabaki na idadi ndogo sana ya waumini wa Katholiki, ili kuzuia anguko hilo akaona awaruhusu mashoga kuwa waumini wa kanisa la Katholiki.

Wenzangu wa madhehebu mengine wakiwemo Waislamu, Wahindu na wengineo, mnapomnyooshea kidole Papa mnamaanisha kuwa hakuna muumini wetu hata mmoja duniani ambaye ni shoga.

Swali la kujiuliza, je katika dhehebu lako hakuna muumini wenu hata mmoja duniani ambaye ni shoga?

Turejelee msemo wa kuwa kabla hujatoa boliti katika jicho la mwenzako basi hakikisha katika jicho lako umekwishatoa!
Wakatoliki kumbe ni mashoga.Roma ikisema ,imesema
 
Yaani kuna watu kama sisi hatujawahi hata ona shoga kwa macho
Ila anakuja mtu anasema eti mashoga wamekuwa wengi hadi wanatishia idadi ya wasio mashoga. Hata ikikusanywa mashoga wote wa dunia nzima hawafiki hata idadi ya wakatoliko wa uganda pekee
Wakatoliki ni mashoga.
 
Ukatoliki siyo Mali ya PAPA FRANSIS, UKATOLIKI ulikuwepo tangu mwaka 33 AD.
Hivyo, kama akikosea katika maamuzi marekebisho yatafanywa na watakaofuatia baada yake.
Kwakuwa UKATOLIKI siyo Mali ya PAPA FRANSIS, ni Upumbavu kuikimbia Mali yako Kwasababu ya majungu ya WATU.
Ukatoliki haukuanza mwaka 33AD.Ukatoliki ulianza baada ya upatanisho wa pili wa Niece,kipindi Cha Mfalme Constantine wa Rumi ya kale.Hii ni baada ya kuingiza mambo ya upagani na ushoga na Askofu mkuu wa Roma kujiita Papa.Dioves zilizobaki zikajitenga naye.
 
Nimesoma paragraphs mbili tu nikaacha🚮
Hata ukiacha ndugu bado ushoga utashamiri. Mimi ni msema kweli huwa ninapowaeleza ukweli ninyi mnakasirika, hapa Dar es Salaam ni vijana wangapi mashoga na wametoka dini zote Islamic na Christian?
Kwanini ninapowaeleza mnachukia kana kwamba Tanzania imejaa watakatifu
 
Back
Top Bottom