Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Papa Francis hapaswi kukosolewa dhidi ya uamuzi wake juu ya LGBTQ

Ukatoliki siyo Mali ya PAPA FRANSIS, UKATOLIKI ulikuwepo tangu mwaka 33 AD.
Hivyo, kama akikosea katika maamuzi marekebisho yatafanywa na watakaofuatia baada yake.
Kwakuwa UKATOLIKI siyo Mali ya PAPA FRANSIS, ni Upumbavu kuikimbia Mali yako Kwasababu ya majungu ya WATU.
Unachoshindwa kujua ni kuwa upapa ni taasisi.
Mapapa ni watekelezaji tu.
Na hili lilikuwepo kwenye mpango tokea kuanzishwa kwa RC
 
Kama waliweza kumkana YESU Tena kwa kuuliza huyu ni nani watashindwa kukumbushia ya sodoma. Napita tu.
 
Uafanuzi kuhusiana na uamuzi wa Papa Fransis kuwakaribisha wapenzi wa jinsia moja katika kanisa Katoliki

Watu wengi duniani hasa dini ya Kiislamu, Wahindu na wengineo wamekuwa wakituhumu Imani ya Kikristo pamoja na kiongozi wetu Papa Fransis kana kwamba dini zao zinawaumini Watakatifu pekee jambo ambalo linaweza kuleta picha ya aibu na fedheha katika imani yetu kwa baadhi ya waumini wengine

Wapo walioenda mbali na kusema Papa Fransis na Imani ya Kikristo inajihusisha na Ushetani

Kwanza kabisa Papa ameweka mbele swala la maslahi katika kanisa hili, lengo la yeye kuchukua uamuzi huu anataka kanisa liwe na idadi kubwa ya waumini pasipokujali tabia na mienendo ya waumini wake akilenga kuwa atakayewahukumu ni Mungu pekee yeye hataki kujihusisha na swala la hukumu hilo ndilo lengo lake

Kawaida binadamu anapokuwa akihitaji wafuasi wengi hatabagua wezi, wavivu, washirikina na wengineo, dhamira yake italenga kuwa na idadi kubwa ya wafuasi

Kwahiyo Papa Fransis haenezi ushetani kama watu wanavyomtuhumu na wala Wakristo tusionee aibu imani yetu

Papa hataki kujihusisha kwenye hukumu ya wakosefu anataka Mungu awahukumu yeye mwenyewe, dhamira yake ni kuhakikisha kanisa linapata wafuasi wengi pasipokujali mienendo na tabia za waumini wake

Swala la hukumu ni jambo gumu sana duniani ndio maana watu wanamwachia Mungu

Nadhani amefikiri mara kadhaa kuhukumu waumini wa Kanisa Katoliki akashindwa pengine ameona kuwa akianza kutoa hukumu itabidi achanganye wote wakiwemo wezi, walevi, wavivu, washirikina, mafisadi, makahaba, wanyang'anyi, walawiti na wengineo

Katika hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusiana na ubaguzi alitoa mfano akasema kuwa nchi ya Tanzania imejengwa na makabila tofauti haikujengwa na kabila moja, madhara ya ubaguzi katika nchi ya Tanzania ni kuwa tukianza kuwaondoa Wazanzibari tukamaliza wote, tutajikuta Wazaramo wamebaki tutawaondoa tena wote, tukimaliza Wazaramo tutakuta kuna Wachaga tutaondoa wote tukimaliza tutagundua kuna Wahaya halikadhalika

Kwahiyo Papa ameona kuwa Kanisa Katoliki limejengwa na waumini wema na wabaya halikujengwa na Watakatifu pekee akianza kuondoa walawiti akamaliza atajikuta wezi wapo ataondoa atamaliza, atajikuta washirikina wapo halikadhalika kwahiyo hatabakiwa na waumini Watakatifu pekee

Ndugu zangu tuzungumze kwa uwazi kuhusiana na uamuzi wa Papa Francis kuwapa mashoga uhuru

Wakosoaji wakubwa wa uamuzi huu ni madhehebu mengine yasiyo ya Katholiki huku wakidai kuwa dini ya Katholiki inaruhusu ushoga

Kabla ya kumtuhumu Papa ni kuwa idadi ya mashoga duniani imeongezeka sana kiasi kwamba inatishia idadi ya wale wasio mashoga.

Takwimu alizopokea Papa zimemfikirisha mara kadhaa na kuona kuwa endapo akiwatenga mashoga basi atabaki na idadi ndogo sana ya waumini wa Katholiki, ili kuzuia anguko hilo akaona awaruhusu mashoga kuwa waumini wa kanisa la Katholiki.

Wenzangu wa madhehebu mengine wakiwemo Waislamu, Wahindu na wengineo, mnapomnyooshea kidole Papa mnamaanisha kuwa hakuna muumini wetu hata mmoja duniani ambaye ni shoga.

Swali la kujiuliza, je katika dhehebu lako hakuna muumini wenu hata mmoja duniani ambaye ni shoga?

Turejelee msemo wa kuwa kabla hujatoa boliti katika jicho la mwenzako basi hakikisha katika jicho lako umekwishatoa!
NAONA unapromote ushoga. Bila shaka wewe Ni mmoja wao.

Badala ya kukemea unawaita unawakumbatia unawatia moyo.

Kwahiyo kwa Sasa kanisa katoliki Ni kimbilio la mashoga.
 
Na wezi wanaingia Kanisani na kupata huduma za korosho kama kawaida si ndio
Sio wezi tu hata wauwaji wanapata huduma za kiroho ila ndio huwezi kujua kuwa huyu ni muuwaji. Mkuu mie nimetoa ushauri kwamba kama mashoga wanaona jamii inawabagua na wakati wao wanaona suala la dini ni muhimu kwao basi waanzishe dini yao ambayo itahalalisha ushoga na kuwa kitu cha kawaida na hapo watapokea huduma za kiroho kwa raha kabisa kuliko kuangaika kulazimisha jamii ichukulie ushoga ni kitu cha kawaida kama vitu vyengine.
 
NAONA unapromote ushoga. Bila shaka wewe Ni mmoja wao.

Badala ya kukemea unawaita unawakumbatia unawatia moyo.

Kwahiyo kwa Sasa kanisa katoliki Ni kimbilio la mashoga.
Mashoga wanapokaribishwa kanisani inamana kuwa yale mahubiri watakayosikiliza yatakuwa yakiwabadilisha taratibu
Na jambo jingine la kuzingatia jibu hoja acha kumwingiza mtoa mada kwenye hoja, huo unaitwa ni ubakaji wa mada mara nyingi wehu ndio wanafanya hivyo lakini mwenye uelewa atajibu kwa hoja
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
ni kweli upo sahihi kabisa wapo hata husemi uongo ila kamwe huwezi kusikia eti wamepongezwa ila watalaaniwa sio kama wengine wamepewa na baraka zooote kabisa
 
Asikosolewe yeye ni Mungu? Anaongoza taasisi kubwa, anaongoza sehemu ya dunia, akisemabkasemea waumini anaowaongoza. Kwanini watu wasimkososoe kama anaenda kinyume na matakwa ya imani ya Roman Catholics, kwanini atuhalalishie tusichokitaka waumini?
Ni binadamu huyo anaweza kukosea na ni lazima akosolewe.
 
Asikosolewe yeye ni Mungu? Anaongoza taasisi kubwa, anaongoza sehemu ya dunia, akisemabkasemea waumini anaowaongoza. Kwanini watu wasimkososoe kama anaenda kinyume na matakwa ya imani ya Roman Catholics, kwanini atuhalalishie tusichokitaka waumini?
Ni binadamu huyo anaweza kukosea na ni lazima akosolewe.
Ushoga umeshamiri sana duniani kiasi kwamba takwimu zinatisha, ameamua kuwapokea tu mana mtu akishafirana hawezi kuacha tena
 
Yeye inabidi afate misingi ya dini sio nyomi then wenye imani watabaki na kanisa. Kanisa linatumika kama tawi la kueneza ajenda za kishetani na mpaka sasa shetani ameshalikamata barabara
Ukristo halisi unaenda kujidhihili ndani ya kanisa katika namna ya ajabu sana, yaliyofichwa yanaenda kufichuka,miongo hii mitatu tunaenda kutambua nyomi ya watakatifu ndani ya kanisa, mkatoliki mwenzangu tuendelee kuombea kanisa ,pale kwa papa Kuna roho mbaya anatamalaki katika madhaifu ya kibinadamu,
 
hapo sijaelewa yaani akubali wizi ili ahakikishe waumini wake ni wezi hii hatari
Maana yake ilikuwa kabla ya kumnyooshea kidole mtoto wa jirani kuwa ni mwizi hakikisha wako sio mwizi
 
Kwa hiyo hili andiko Papa halijui?

Wakorintho 5:11-13​

Neno: Bibilia Takatifu​

11. Lakini nilikuwa namaanisha kwamba msishirikiane na mtu ye yote anayejiita ndugu lakini ni mwasherati, mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu, mtukanaji, mlevi na laghai. Wala msile na mtu kama huyo.

12. Si kazi yangu kuhukumu watu walio nje ya kanisa. Je, si hao walio ndani ya kanisa mnaopaswa kuwahukumu?

13. Mungu anawa hukumu walio nje ya kanisa. “Mfukuzeni mtu mwovu atoke kutoka katika ushirika wenu.”
 
Hapa unakosea.
Kwenda kubariki ndoa ya mwanaume na mwanaume huko ni kubariki dhambi.
Wapi imeandikwa ndoa? Kuwa shoga kunahitaji ndoa? Watu wengi humu huwa hawajui mada za nyuzi, nimeona hilo mara nyingi
 
Back
Top Bottom