Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Status
Not open for further replies.
Nafikiri huu ndio wakati wa wakatoliki kusilimu au kurejea kwenye dini za mababu.

Sisemi kuwa miongoni mwa waislamu hakuwa watu wanao fanya mambo hayo? La haha! Mambo hayo yanafanywa na watu wa dini zote wakristu kwa waislamu. Tatizo ni pale taasisi kama taasisi ya kidini inapo yatambua mapenzi ya namna hiyo.

Poleni sana wakatoliki.

====


"Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga,"

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomuomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya maombi yaliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na kiongozi wa kiroho, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

BBC
Weka link ya source ya information yako
 
Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.
Akijibu kundi la makadinali waliomwomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".
View attachment 2770217
"Hatuwezi kuwa majaji ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga," alisema.
Aliongeza, hata hivyo, kwamba Kanisa bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya idadi iliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.
Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.
Maaskofu katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ubelgiji na Ujerumani, wameanza kuwaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, lakini msimamo wa mamlaka ya Kanisa ulibakia kutoeleweka.
Mnamo 2021, kufuatia ombi kama hilo la ufafanuzi, ofisi ya mafundisho ya Vatikani iliamua kutoruhusu zoea hilo.
Akijibu ombi la hivi punde zaidi, Papa alisema kwamba Kanisa linaelewa ndoa kuwa "muungano wa kipekee, thabiti, na usioweza kutenganishwa kati ya mwanamume na mwanamke" na inapaswa kuepuka "aina yoyote ya ibada au sakramenti ambayo inaweza kupingana na imani hii".
Lakini aliongeza kuwa "baraka inapoombwa, ni kuonyesha ombi kwa Mungu kwa msaada, dua ya kuishi bora".
"Busara ya kichungaji lazima itambue vya kutosha kama kuna aina za baraka, zinazoombwa na mtu mmoja au zaidi, ambazo hazileti dhana potofu ya ndoa," alisema.
Akionekana kupendekeza kwamba maombi ya baraka yazingatiwe kwa msingi wa kesi baada ya kesi, alisema kwamba "maamuzi ambayo yanaweza kuwa sehemu ya busara ya kichungaji katika hali fulani haipaswi kuwa kawaida".
"Sheria ya Canon haifai na haiwezi kufunika kila kitu," alisema.
Aliongeza kuwa Kanisa linapaswa kukaribia uhusiano wake na watu kila wakati kwa "fadhili, uvumilivu, ufahamu, huruma, na kutia moyo".
Mnamo Februari, kura ya viongozi wakuu katika Kanisa la Uingereza iliunga mkono mapendekezo ya kuruhusu maombi ya baraka kwa wapenzi wa jinsia moja.
Hatua hiyo ilimaanisha kwamba wanandoa wa jinsia moja wanaweza kwenda katika kanisa la Anglikana baada ya sherehe ya ndoa halali kwa ajili ya huduma zikiwemo maombi ya wakfu, shukrani, na baraka za Mungu.
sio wakanza tulitarajia hilo na naandika hapa hata makkah watakuja kukubali hii ndoa za jinsia moja

haya mambo ni kuwa nayo makini sana ni lazima tukubali tunautamaduni wa tofauti baina yetu na wazungu muhimu kila jamii izingatie utamaduni wa mazingira yao ingawa imani haibadiliki na aina maana kama ni mkatoliki basi kwa kuwa papa amepitisha hili swala basi na wewe ukatoliki wako unapotea hapana.
 
Tukiwaambia watu kwamba Mungu hayupo, ni stori za uongo zisizo na kichwa wala miguu watu hawaelewi.

Sasa dini iliyosema mungu kaumba mke na mume, leo inakuja kusema haina ubaya mume kuoa mume mwenzie na iko tayari kubariki, sasa unajiuliza huyo mungu kabadili mawazo ama ni nini?

Dini ni taasisi za kitapeli, mungu wanaemsema hayupo wala hajawahi kuwepo.
 
Daima Mungu hajawahi kumficha mnafiki bali ni suala la muda tu...... nyakati zinatubainishia mambo yaliyojificha ili wenye macho na akili timamu wapate kujionea wenyewe na sio kuhadithiwa tena...........

Vichwa watumwa wa fikra na walevi wa Imani vipo njia panda huku wakificha macho yao wasione wanachokiona....huku vichwa vya watu wenye akili timamu wakitafakari na kuanza kuchukua hatua kwani hizi ni nyakati muhimu kwao........

YULE AMBAYE HAIKUMFAA AKILI YAKE, BASI UTAMDHURU UJINGA WAKE
 
sio wakanza tulitarajia hilo na naandika hapa hata makkah watakuja kukubali hii ndoa za jinsia moja

haya mambo ni kuwa nayo makini sana ni lazima tukubali tunautamaduni wa tofauti baina yetu na wazungu muhimu kila jamii izingatie utamaduni wa mazingira yao ingawa imani haibadiliki na aina maana kama ni mkatoliki basi kwa kuwa papa amepitisha hili swala basi na wewe ukatoliki wako unapotea hapana.
Sikupingi ofisaa
 
Aliongeza, hata hivyo, kwamba Kanisa bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mbona ameruhusu kuzibariki... Kitu hukitambui au unasema ni dhambi alafu unakinariki vipi...

Kubariki maana yake umekubaliana nacho na unakitakia maisha mazuri... Yani wasiachane na waendelee
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom