Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Papa Francis: Hisani ya Kichungaji itumike wapenzi wa jinsia moja wanapowaomba mapadri baraka

Status
Not open for further replies.
Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomwomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".
View attachment 2770217
"Hatuwezi kuwa majaji ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga," alisema.

Aliongeza, hata hivyo, kwamba Kanisa bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja. Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya idadi iliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.
Maaskofu katika nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ubelgiji na Ujerumani, wameanza kuwaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsia moja, lakini msimamo wa mamlaka ya Kanisa ulibakia kutoeleweka.

Mnamo 2021, kufuatia ombi kama hilo la ufafanuzi, ofisi ya mafundisho ya Vatikani iliamua kutoruhusu zoea hilo.
Akijibu ombi la hivi punde zaidi, Papa alisema kwamba Kanisa linaelewa ndoa kuwa "muungano wa kipekee, thabiti, na usioweza kutenganishwa kati ya mwanamume na mwanamke" na inapaswa kuepuka "aina yoyote ya ibada au sakramenti ambayo inaweza kupingana na imani hii".
Lakini aliongeza kuwa "baraka inapoombwa, ni kuonyesha ombi kwa Mungu kwa msaada, dua ya kuishi bora".

"Busara ya kichungaji lazima itambue vya kutosha kama kuna aina za baraka, zinazoombwa na mtu mmoja au zaidi, ambazo hazileti dhana potofu ya ndoa," alisema.

Akionekana kupendekeza kwamba maombi ya baraka yazingatiwe kwa msingi wa kesi baada ya kesi, alisema kwamba "maamuzi ambayo yanaweza kuwa sehemu ya busara ya kichungaji katika hali fulani haipaswi kuwa kawaida".
"Sheria ya Canon haifai na haiwezi kufunika kila kitu," alisema.

Aliongeza kuwa Kanisa linapaswa kukaribia uhusiano wake na watu kila wakati kwa "fadhili, uvumilivu, ufahamu, huruma, na kutia moyo".
Mnamo Februari, kura ya viongozi wakuu katika Kanisa la Uingereza iliunga mkono mapendekezo ya kuruhusu maombi ya baraka kwa wapenzi wa jinsia moja.

Hatua hiyo ilimaanisha kwamba wanandoa wa jinsia moja wanaweza kwenda katika kanisa la Anglikana baada ya sherehe ya ndoa halali kwa ajili ya huduma zikiwemo maombi ya wakfu, shukrani, na baraka za Mungu.
Warumi 1:21-28
[21]kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
Because that, when they knew God, they glorified him not as God, neither were thankful; but became vain in their imaginations, and their foolish heart was darkened.
[22]Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
Professing themselves to be wise, they became fools,
[23]wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
And changed the glory of the uncorruptible God into an image made like to corruptible man, and to birds, and fourfooted beasts, and creeping things.
[24]Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
Wherefore God also gave them up to uncleanness through the lusts of their own hearts, to dishonour their own bodies between themselves:
[25]Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
Who changed the truth of God into a lie, and worshipped and served the creature more than the Creator, who is blessed for ever. Amen.
[26]Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
For this cause God gave them up unto vile affections: for even their women did change the natural use into that which is against nature:
[27]wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
And likewise also the men, leaving the natural use of the woman, burned in their lust one toward another; men with men working that which is unseemly, and receiving in themselves that recompence of their error which was meet.
[28]Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
And even as they did not like to retain God in their knowledge, God gave them over to a reprobate mind, to do those things which are not convenient;

Unajua watu waliokwisha haribika fahamu zao kwa jinsi Mungu alivyokwisha waacha hawawezi tena kupambanua kati ya mema na batili.
Wanazitumainia hekima za binadamu badala ya hekima ya Mungu ambayo ni neno lake.
Alicholaani Mungu mwanadamu hana mamlaka ya kukibariki na alichobariki Mungu mwanadamu hana mamlaka ya kukilaani.
Katika eneo hili ndipo kanisa la kimapokeo nje ya kweli ya neno walipopigwa upofu.
 
Alichoongea Papa ni hiki ingawaje sidhani kama Ali aliruhusu hilo jambo...
 
Attachments

  • Screenshot_20231003-115703_Chrome.jpg
    Screenshot_20231003-115703_Chrome.jpg
    162 KB · Views: 1
Nafikiri huu ndio wakati wa wakatoliki kusilimu au kurejea kwenye dini za mababu.

Sisemi kuwa miongoni mwa waislamu hakuwa watu wanao fanya mambo hayo? La haha! Mambo hayo yanafanywa na watu wa dini zote wakristu kwa waislamu. Tatizo ni pale taasisi kama taasisi ya kidini inapo yatambua mapenzi ya namna hiyo.

Poleni sana wakatoliki.

====

"Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga,"

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomuomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya maombi yaliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na kiongozi wa kiroho, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

BBC
Papa ni shoga?
 
"Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga,"
Kanisa katoliki kwenye mafundisho yake kazi ya kutoa hukumu ni ya Mungu
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.
Alipendekeza wapi na nukuu ya hilo pendekezo iko wapi.
Akijibu kundi la makadinali waliomuomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".
"hisani ya kichungaji" ndio mapendekezo ya ushoga? Ina maana kataja maneno mawili tu
Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.
Kauli yake kuhusu hili iko wapi. Kwanini utoe taarifa ya kuambiwa wakati nukuu ya alichosema ipo.
Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya maombi yaliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na kiongozi wa kiroho, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

BBC
Kwenye habari haionekani kasema nini. Kauli yake mwenyewe ya kupendekeza iko wapi, sio ulete kauli za mwandishi wa habari yako.

Leta speech hiyo uliyotumia kutafsiri Wakatoliki wasome wenyewe maana akili wanazo. Sio uwatafsirie unavyotaka wewe na uchomeke maneno manne tu aliyotamka kwenye Uzi wako mzima.
 
Kanisa katoliki kwenye mafundisho yake kazi ya kutoa hukumu ni ya Mungu

Alipendekeza wapi na nukuu ya hilo pendekezo iko wapi.

"hisani ya kichungaji" ndio mapendekezo ya ushoga? Ina maana kataja maneno mawili tu

Kauli yake kuhusu hili iko wapi. Kwanini utoe taarifa ya kuambiwa wakati nukuu ya alichosema ipo.

Kwenye habari haionekani kasema nini. Kauli yake mwenyewe ya kupendekeza iko wapi, sio ulete kauli za mwandishi wa habari yako.

Leta speech hiyo uliyotumia kutafsiri Wakatoliki wasome wenyewe maana akili wanazo. Sio uwatafsirie unavyotaka wewe na uchomeke maneno manne tu aliyotamka kwenye Uzi wako mzima.
ametumia mkurupuko kuleta bandiko
 
Hi ni sawa na kusema huli Nyama ya Mbwa unakunywa supu ya nyama ya mbwa tu
Haviendani hata kidogo na nilichosema. Kanisa limeweka bayana kuwa mapenzi ya jinsia moja ni dhambi na halitambui ndoa za jinsia moja. Wanaihitaji baraka koz uenda wakabadili mienendo yao na kurudi ktk njia iliyonyooka.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom