DolphinT
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 2,371
- 3,469
Twende taratibu kabisa na nadhani utanjjibu Kwa hekima Kwa ajili ya kujenga ufahamu wangu na wako kuhusu Ushoga na ndoa za jinsia Moja na msimamo wa kanisa Katoliki:Hajamkwepa kasalimia upande wa pili hawa Mapapa ni wazee wa kubariki ushoga
1. Kanisa ni sehemu ambayo wenye dhambi wote wanaitwa Ili kumjua Mungu aliyewaumba na kutubu dhambi zao na kungeukia Mungu na kuacha dhambi zao pasina kujali wamefanya dhambi za namna Gani, kwani Kwa Mungu Kuna Msamaha wa dhambi za mwanadamu. Tusome Katika biblia
Isaya 1:18
Biblia inasema:
“Njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.”
Lakini Pope kama halifa wa Petro ambaye Kwa Imani ndivyo aliyekabidhiwa dhamana ya kanisa
Tusome
Biblia inasema:
Ana wajibu wa kuwaalika watu wote walio tayari kumjua Mungu na kuacha dhambi zao Kwa kumaanisha na kumrudia Mungu, alifanya kosa gani?“Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya huu mwamba nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.” — Mathayo 16:18 (SUV)
Mana Yesu mwenyewe anasema
:
Biblia inasema:
Kwamba Kanisa lipo Kwa ajili ya wenye dhambi na Kwa maana hiyo kanisa Lina wajibu wa kuwaalika watu Hawa Ili wabadili njia zao mbaya ba kupokea rehema za Mungu!“Yesu akajibu, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali wale walio hawawezi.” — Luka 5:31
2. Msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu ndoa Bado hamjabadilika na hautabadilika kwani upo Kwa mujibu wa Sheria za Kanisa (CANON LAWSS)
Tusome:
1. Ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke tu
Sheria ya Kanisa Katoliki inasema wazi kwamba ndoa halali haiwezi kuwepo isipokuwa kati ya mtu wa jinsia ya kiume na wa jinsia ya kike.
Canon 1055 §1: “The matrimonial covenant, by which a man and a woman establish between themselves a partnership of the whole of life... has been raised by Christ the Lord to the dignity of a sacrament between the baptized.”
2. Ndoa ni sakramenti takatifu
Kwa wabatizwa wote wa Kanisa Katoliki, ndoa ni mojawapo ya sakramenti saba. Ndoa si mkataba wa kiraia tu, bali ni tendo la neema ya kiroho.
Canon 1055 §2: “For this reason a valid matrimonial contract cannot exist between the baptized without it being by that very fact a sacrament.”
3. Ndoa ni ya kudumu na haivunjwi kwa talaka
Kanisa linafundisha kuwa ndoa halali na iliyokamilika haiwezi kufutwa na mamlaka yoyote ya kibinadamu, isipokuwa kwa kifo.
Canon 1141: “A marriage which is ratified and consummated cannot be dissolved by any human power or by any cause other than death.”
4. Kanisa linapinga ndoa za jinsia moja
Kanisa Katoliki halitambui ndoa za jinsia moja, na linatafsiri uhusiano wa aina hiyo kuwa si sawa na ndoa wala si sakramenti. Kwa msingi huo, hakuna ndoa halali kati ya watu wa jinsia moja.
Catechism of the Catholic Church (CCC) 2357: “Under no circumstances can homosexual acts be approved. They are contrary to the natural law.”
5. Malengo ya ndoa:
Kuendeleza upendo wa dhati kati ya wanandoa
Kulea watoto katika imani ya Kikristo
Kuishi katika uaminifu, msaada wa kiroho, na utakatifu
ive firmness by reason of the sacrament.”Canon 1056: “The essential properties of marriage are unity and indissolubility; in Christian marriage, they acquire a distinct
HAYA NAOMBA UTUPE USHAHIDI USIACHA SHAKA LINI KANISA KATOLIKI LILIBARIKI USHOGA NA KURIDHIA NDOA ZA JINSI MOJA NA UTAJE ANGALAU PADRE, ASKOFU AU CARDINALI AMBAYE ALIFUNGIDHA NDOA HIYO LINI NA WAPI
ILI TUJENGE UFAHAMU WA PAMOJA.