Pascal Mayala from Cape to Mumbai, hadithi iliyojificha yasimuliwa

Pascal Mayala from Cape to Mumbai, hadithi iliyojificha yasimuliwa

Pascal Mayala(CCM) alipopata uwakili nilimuuliza kama atakuwa wakili wa wanaccm tu na mwanachadema ambaye siku zote ana hasira naye ataweza kumtetea? Swali langu lilitokana na dunia kuwa duara, tenda ulitendalo lakini kuna siku utakwama na kuwarudia unaowachukia.

Pasikali asiyewapenda wanachadema leo anawaomba watanzania wote(sijui kama wanachadema nao ni watanzania) bila kujali tofauti zao wamchangie pesa aweze kugombea ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki!

Huyu Paskali anachohitaji pesa tu za kumuwezesha kugombea ubunge tu na atakapoupata atawashukuru wanaccm na viongozi wake, Pascal atajipambanua yeye ni mbunge kupitia CCM na si watanzania, tukumbuke hii ni EAC.

Pascal ajue umchukiae kesho atakuja kukufaa na siasa hazihitaji chuki za binafsi.
"Pascal atajipambanua yeye ni mbunge kupitia CCM na si watanzania"hii statement yako imejaa chuki nyingi sana,kwani CCM sio ya watanzania...?
 
Sasa mbona unachanganya CCM na serikali! Mimi nilidhani serikali ni mali ya wananchi na haitatokea hata nukta moja nchi kuwa haina serikali, alipoondoka mwingereza serikali haikuondoka ilibaki ila msimamizi aliondoka na akaingia msimamizi mwingine. Hofu yangu ni kuwa akipata hatawatambua watu wote isipokuwa wanaccm.
Kwanza hata CCM yenyewe hawatampitisha kabisa . Yaani angejua kwamba CCM hawampendi asingeendelea kuwakumbatia
 
"Pascal atajipambanua yeye ni mbunge kupitia CCM na si watanzania"hii statement yako imejaa chuki nyingi sana,kwani CCM sio ya watanzania...?
CCM ingekuwa ya watanzania isingewafanyia ukatili wasio wanaccm, imeua sana na kuwatia vilema wengi huku ikilikataza jeshi la polisi kuchukua hatua.
 
Ni vile sisi wengine tukichangia kitu hatusemi, huu mchango ni moral support at personal level. Amini usiamini, japo mimi ni CCM lakini nachangia michango vyama vyote kama Sabodo!, tofauti zetu ni figures tuu, mwenzangu ni 6 figures mimi ni single or double digits!.
P
BILIONEA SABODO AFARIKI DUNIA..

Bilionea na Mchumi maarufu nchini, Mustafa Jaffer Sabodo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwakwe, Masaki jijini Dar es Salaam.

"Mzee amefariki leo alfajiri akiwa nyumbani. Taratibu za mazishi zinaendelea na atazikwa katika makaburi yaliyoko mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE," amesema Danstan.

Marehemu Sabado alizaliwa mkoani Lindi na alikuwa akifanya biashara katika nchi za Ufaransa, India, Kenya, Sudan, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania.

Atakumbukwa kwa mchango wake ulioanzisha Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery alipotoa msaada wa Sh milioni 800. Alihusika katika utoaji wa misaada kadhaa iliyohusisha kilimo, ujenzi wa visima na kusaidia wenye uhitaji.
Sabodo atazikwa leo saa 4:30 usiku.
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.
“We surely belong to Allah and to Him we shall return”
"Sisi sote ni wa Mola, na kwake tutarejea".

Paskali pia anakuaga!.
RIP Jaffar Sabodo.
 P
 
Back
Top Bottom