Ni vile sisi wengine tukichangia kitu hatusemi, huu mchango ni moral support at personal level. Amini usiamini, japo mimi ni CCM lakini nachangia michango vyama vyote kama Sabodo!, tofauti zetu ni figures tuu, mwenzangu ni 6 figures mimi ni single or double digits!.
P
BILIONEA SABODO AFARIKI DUNIA..
Bilionea na Mchumi maarufu nchini, Mustafa Jaffer Sabodo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwakwe, Masaki jijini Dar es Salaam.
"Mzee amefariki leo alfajiri akiwa nyumbani. Taratibu za mazishi zinaendelea na atazikwa katika makaburi yaliyoko mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE," amesema Danstan.
Marehemu Sabado alizaliwa mkoani Lindi na alikuwa akifanya biashara katika nchi za Ufaransa, India, Kenya, Sudan, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania.
Atakumbukwa kwa mchango wake ulioanzisha Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery alipotoa msaada wa Sh milioni 800. Alihusika katika utoaji wa misaada kadhaa iliyohusisha kilimo, ujenzi wa visima na kusaidia wenye uhitaji.
Sabodo atazikwa leo saa 4:30 usiku.
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.
“We surely belong to Allah and to Him we shall return”
"Sisi sote ni wa Mola, na kwake tutarejea".
Paskali pia anakuaga!.
RIP Jaffar Sabodo.
P