Waziri wa Fedha tena akiwasilisha bajeti ya nchi hapaswi kutoa sifa za kuhudhuria misiba, kuwaona wafungwa, kushiriki michezo, kwenda makanisani nk na kuonesha mh Rais ni kiumbe cha kipekee. Akikuwa amebakiza kidogo sana kuinama chini na kumsujudia Rais.
Tujifunze kupongeza vitu na kusonga mbele. Ni ajabu mpk sasa tunazungumzia bwawa la umeme, ndege, SGR, elimu bure, uhakiki wa wafanyakazi. Ilitosha kupongeza mambo hayo wakati yalipoanza. Tujifunze tunapoanza au kukamilisha jambo fulani, lingine hutokea au mahitaji huenda ngazi nyingine ya juu. Ni vema kusifia lakini si vema kutumia nguvu zote kusifia na kushindwa hata kuona mambo mengine.
Rais amefanya mambo mazuri, tumsifie kidogo na tumuoneshe mahitaji mengine hata kama itabidi kumkosoa kwa namna alivofanya aliyoyafanya tayari.
Ukimsifia sana mtu, unakosa uhalali wa kumwambia amekosea. Unaanza kumwogopa!! Huenda hizi sifa ni uoga!!